Mbunge wa
viti maalumu Iringa mjini RITTA KABATI
Mbunge wa viti maalumu Iringa mjini RITTA KABATI
NA MARIAM MATUNDUIRINGA
Mbunge wa viti maalumu Iringa mjini RITTA KABATI amewataka wakinamama kujitokeza kwa wingi kugombea nafasi mbalimbali katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwezi wa kumi mwaka huu.
Mbunge wa viti maalumu Iringa mjini RITTA KABATI
NA MARIAM MATUNDUIRINGA
Mbunge wa viti maalumu Iringa mjini RITTA KABATI amewataka wakinamama kujitokeza kwa wingi kugombea nafasi mbalimbali katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwezi wa kumi mwaka huu.
KABATI
ameeleza kuwa wanawake waondoe hofu ya kugombea hasa kukiwa na ushindani wa
wagombea wanaume kwa kuogopa kuchafuliwa kwa mambo yasiyokuwepo.
Ameendelea
kusema kuwa wananchi wasishawishiwe na propaganda za wanasiasa na badala yake
wachague viongozi bora wenye uwezo wa kuongoza kutoka katika chama chochote.
Aidha ameongeza
kuwa viongozi wawe na sera za kutekelezeka ili kuwatendea haki wapiga kura wao
hali itakayowafanya waaminike katika jamii.
KABATI
amesema kuwa wanawake wawemstari wa mbele kuchukua fomu za kugombea na kwamba
wasikatishwe tamaa na baadhi ya watu wanaodhani kwamba wanawake hawawezi
kugombea na kuongoza katika nafasi mbalimbali.
Aidha
ameongeza kuwa Jamii iachane na mitazamo tofauti kwa wanawake wanao jitokeza
kugombea nafasi za uongozi na kuwaasa wanawake wawe na misimamo pindi
wanapoingia madarakani, kujiamini na kutokubali kutumiwa
kama chombo cha starehe.
Mbali na
hayo KABATI amewakumbusha vijana kutokubali kutumiwa na baadhi ya wanasiasa
katika kuleta vurugu hasa katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu na
badala yake wachague kiongozi mwenye weredi na sifa za kuwa kiongozi kutokana
na sera za chama chake.
Ameendelea
kusema kuwa vijana wajotokeze kwa wingi katika kupiga kura ndiyo katika katiba
iliyopendekezwa ili kuweza kufanya uchaguzi ulio wa haki na amani pia
kujitokeza katika kujiandikisha katika daftari la wapiga kura pamoja na kupiga
kura.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269