Waziri Nyalandu |
SIKU ya Mkesha wa Mwaka Mpya, Desemba
31, 2014, nilikaribishwa kushiriki ibada ya Mkesha na Baba Mchungaji Kiongozi
wa Kanisa la Ephata, Josephat Mwingira, iliyofanyika Kibaha mkoani Pwani.
Mkesha huo ulitangazwa moja kwa moja
kwenye kituo cha luninga cha Star TV na kuhudhuriwa na maelfu ya watu.
Katika Mkesha huo, nilipewa fursa ya
kuwasalimia waumini na kushirikiana nao katika neno la Mungu, ambapo huku nilieza
matumaini yangu kwa Taifa letu na ushiriki wa vijana katika uongozi wa nchi,
kama yanenanvyo maandiko 'vijana wenu wataona maono na wazee wenu wataona
ndoto'.
Hata hivyo, jana nimesikitishwa sana
na kuumizwa na habari ambazo hazina mashiko, za uzushi na za kutunga zenye
lengo la kunipaka matope kwa kunihusisha na maneno ambayo kinywa changu
hakikuyatamka wala kuyafanyia rejea. Nimeshangazwa sana.
Katika maisha yangu kama mtanzania,
kiongozi na mkristo, kamwe sijawahi na sitarajii kutoa kauli hasi dhidi ya
imani za dini ningine, ikiwepo dini ya kiislamu. Nisisitize kuwa ninawapenda
watu wa dini zote na makabila yote na kamwe sina ubaguzi kama inavyojaribu
kuwekwa ili kunipaka matope katika jamii. Naamini taarifa hizo potofu zina
malengo binafsi na watu wasionitakia mema.
Katika jimbo langu la Singida
Kaskazini, nimeshiriki kusaidia ujenzi wa nyumba za ibada ikiwemo makanisa na
misikiti kwa uwazi kwa kuboresha miundombinu na kuziwezesha taasisi hizi kutoa
mchango katika elimu.
Sio hivyo tu, kuonyesha ninachojaribu
kuzungumzwa kuwa ni uongo na uzushi mtupu, katika Jimbo la Singida Kaskazini,
nimepeleka masheikh wa vijijini mbalimbali kwa ajili ya kuhiji Mecca, mpango
ambao ni endelevu kwa zaidi ya miaka 10 sasa.
Ni muhimu demokrasia ikaendelezwa
kwa kuhimiza mijadala ya kuwaletea wananchi maendeleo na sio kwa kueneza chuki za
kidini, kijinsia au kikabila.
Mungu ameliweka Taifa letu kuwa heri
katikati ya mataifa na ni muhimu sote kudumisha amani na mshikamano badala ya
kusingiziana uongo. Imeandikwa katika vitabu, usimsingizie jirani yako uongo'.
Imetolewa
na
Lazaro
Nyalandu,
MNEC,
CCM
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269