"Karibu" ndiyo anavyosema Mwakilishi wa Kudumu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, Balozi Tuvako Manongi wakati akimkaribisha mgeni wake Mwakilishi wa Kudumu wa Jamhuri ya Ujerumani katika Umoja wa Mataifa Balozi Harld Braun alipofika kwa mazungumzo katika Uwakilishi wa Tanzania siku ya jumatatu.
Wawakilishi hao wawili walizungumzia masuala mbalimbali yenye maslani kwa mataifa hayo mawili, na moja ya masuala hayo ni namna gani Tanzania na Ujerumani kama sehemu ya kundi la nchi ambazo ziko mstari wa mbele kupinga na kukemea uharamia dhidi ya wanyamapori zitakavyoshirikiana katika majadiliano na maandalizi ya rasimu ya Azimio kuhusu uharamia dhidi ya wanyama pori.
Katika mazungumzo hayo Balozi Harld Braun alitambua juhudi kubwa zinazofanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete za kuongoza na kusimamia mipango ya serikali katika kudhibiti uwindaji haramu wa wanyamapori na hususani Tembo. Ni kwa kutambua Juhudi hizo za Rais Kikwete ndiyo maana Ujerumani inaiomba Tanzania kupitia Uwakilishi wake wa Kudumu kuwa moja na nchi zitakazo dhamini Azimio hilo
Your Ad Spot
Jan 13, 2015
Home
Unlabelled
TANZANIA NA UJERUMANI ZAJADILIANA UHARAMIA DHIDI YA WANYAMAPORI
TANZANIA NA UJERUMANI ZAJADILIANA UHARAMIA DHIDI YA WANYAMAPORI
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post Top Ad
Your Ad Spot
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269