Kaimu mkurugenzi wa fedha na
utawala wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Yahaya Ally, akitoa taarifa ya
fedha ya Mfuko huo wakati wa mkutano wa nne wa wanachama na wadau wa
PSPF, mjini Dodoma. Mkutano huo ulioanza Februari 18, umefungwa leo
Alhamisi Februari 19, 2015
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa
Pensheni wa PSPF, Adam Mayingu, akisikiliza kwa makini majadiliano ya
wanachama na wadau wa Mfuko huo wakati wa mkutano mkuu wa nne wa
wanachama na wadau wa PSPF mjini Dodoma ,
Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya Posta,
Sabasaba Moshingi, akitoa mada, kuhusu benki hiyo inavyoweza kuwasaidia
wanachama wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, kutokana na ushikiano wa
kibiashara baina ya taasisi nhizo mbili, wakati wa mkutani mkuu wa nne
wa wanachama na wadau wa PSPF mjini Dodoma.
Dkt.Bill Kiwia, akijibu hoja
mbalimbali za washiriki wa mkutano mkuu wa nne wa wanachama na wadau wa
Mfuko wa Pensehni wa PSPF kuhusu ushindani wa mifuko ya hifadhi ya jamii
na tahadhari ya kuchukua a,kitolea mfano wa Tanzania mjini Dodoma leo
Alhamisi Februari 19, 2015.
Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Mfuko
wa Pensheni wa PSPF, Neema Muro, akitoa mada kuhusu huduma zitolewazo na
Mfuko huo kwa wanachama wake, wakati wa mkutano mkuu wa nne wa
wanachama na wadau mjini Dodoma.
Kikundi cha wasanii mkoani Dodoma,
kikitoa burudani kwa wajumbe wa mkutano mkuu wa nne wa wanachama na
wadau wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, mjini Dodoma. Mkutano huo
umemalizika leo Alhamisi Feb 19, 2015.
Baadhi ya wajumbe wa kamati ya
maandalizi ya mkutano mkuu wa nne wa Wanachama wa Mfuko wa Pensheni wa
PSPF, wakiongozwa na Meneja wa Masoko na Mawasiliano wa Mfuko huo,
Costantina Martin (wapili kushoto), wakiwa katika picha ya pamoja baada
ya kufanikisha mkutano huo kwa mafanikio makubwa. Mkutano huo
umemalizika leo Alhamisi Februari 19, 2015.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269