Mtu moja aliyetambulika kwa jina la YONA MWAMWERE ameteketezwa
kwa moto na wananchi wenye hasira kali baada ya kumpasua kichwa mtoto
wa dada yake na kufariki dunia papo hapo kwa kutumia sururu ,ambae
alikua akiishi naye maeneo ya Nsalaga Uyole
TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI “PRESS RELEASE” TAREHE 16.03.2015.
MTOTO MWENYE UMRI WA MIAKA MITANO AUAWA KWA KUKATWA KICHWA KWA SULULU NA MJOMBA WAKE.
MTOTO MWENYE UMRI WA MIAKA 05 ALIYETAMBULIKA KWA JINA LA JONSON MWAMWERE, MKAZI WA NSALAGA JIJINI MBEYA, ALIUAWA KWA KUPIGWA SULULU KICHWANI NA KUTENGANISHWA KICHWA NA KIWILIWILI NA MJOMBA WAKE AITWAYE YONA MWAMWERE (38) MKAZI WA NSALAGA.
TUKIO HILO LIMETOKEA MNAMO TAREHE 16.03.2015 MAJIRA YASAA 11:00 ASUBUHI HUKO KATIKA MTAA WA NSALAGA-UYOLE, KATA YA NSALAGA, TARAFA YA IYUNGA, JIJI NA MKOA WA MBEYA.
AWALI INADAIWA KUWA, YONA MWAMWERE ALIKUWA
ANAMFUKUZA MTOTO HUYO AMBAYE NI MJOMBA WAKE KUTOKA NYUMBANI NA
ALIKIMBILIA KWENYE JENGO LILILOPO JIRANI NA NYUMBANI KWAO AMBALO BADO
LIPO KWENYE UJENZI.
HATA HIVYO TAARIFA ZINADAI KUWA, YONA MWAMWEREALIPOFIKA
KWENYE JENGO HILO ALIWATISHIA MAFUNDI WALIOKUWA WANAJENGA NA WOTE
WALIKIMBIA, HIVYO ALIMUUA MJOMBA WAKE HUYO KWA KUMPIGA KICHWANI KWA
SULULU NA KUTENGANISHA KICHWA NA KIWILIWILI.
KUFUATIA
TUKIO HILO MAFUNDI WALIOKUWA WAKIENDELEA NA UJENZI WALIPIGA KELELE ZA
KUOMBA MSAADA, HIVYO KUNDI LA WANANCHI WALIOAMUA KUJICHUKULIA SHERIA
MKONONI WALIJITOKEZA NA KUMSHAMBULIA MTUHUMIWA KWA KUMPIGA HADI KUFA NA
KISHA KUUCHOMA MOTO MWILI WAKE.
MAREHEMU
WOTE WALIKUWA NI NDUGU WANAOISHI NYUMBA MOJA, MIILI YAO IMEHIFADHIWA
HOSPITALI YA RUFAA MBEYA. CHANZO CHA TUKIO HILI KINACHUNGUZWA INGAWA
UCHUNGUZI WA AWALI UNAONYESHA KUWA MAREHEMU YONA MWAMWEREALIKUWA NA MATATIZO YA AKILI.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA
POLE KWA FAMILIA YA MAREHEMU KUTOKANA NA TUKIO HILO. AIDHA ANATOA WITO
KWA JAMII/WANANCHI KUACHA TABIA YA KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI KWANI NI
KINYUME CHA SHERIA NA BADALA YAKE WAJENGE TABIA YA KUWAFIKISHA KATIKA
MAMLAKA HUSIKA WATUHUMIWA WANAOWAKAMATA KWA TUHUMA MBALIMBALI KWA HATUA
ZAIDI ZA KISHERIA.
Imesainiwa na:
[AHMED Z. MSANGI – SACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269