Breaking News

Your Ad Spot

Mar 16, 2015

MADAKTARI KUTOKA KATIKA CHAMA CHA MADAKTARI WA KINYWA NA MENO TANZANIA WAMETOA HUDUMA YA BURE KWA WATOTO MIA TATU NA THELATHINI NA SABA WENYE ULEMAVU WA NGOZI,VIZIVI NA WASIOONA WANAOLELEWA KATIKA KITUO CHA BUHANGIJA KILICHOKO MKOANI SHINYANGA NA HII NI KATIKA KUELEKEA KILELE CHA MADHIMISHO YA KILELE CHA SIKU AFYA YA KINYA NA MENO DUNIANI INAYO ADHIMISHWA KILA TAREHE 20 YA MWEZI WA 3 KILA MWAKA

  chama chao  Madaktari Wakinywa na Meno Tanzania toka mikoa mbalimbali wa kiongozwa na Raisi Mstaafu wa Chama cha  Madaktari wa Kinywa na Meno na Daktari Bingwa wa Watoto  Rachel Mhavile  toka Hospitali ya Taifa  Muhimbili ,waitembelea Shule ya Msingi ya Buhangija iliyopo Shinyanga  katika Kuadhimisho  wiki ya  kinywa na Meno ambapo kila  Mwaka huadhimishwa Duniani kote 20 Machi.Wakiwa katika picha ya pamoja walipotembelea  Manispa ya  Shinyanga .
Madaktari wakiwa katika picha ya pamoja na Mganga Mkuu wa Hospitali ya Mkoa  Shinyanga Dr.Ntuli Kapologwe, mara walipo ripoti katika Hospitali hiyo.
Matroni  Digna Mwacha,akiwa  na watoto hao wa ulemavu wa ngozi ambao ni wageni walio fikishwa kituoni hapo kwa usalama zaidi ,watoto hao ni Joice Maona (12)  na mdogo wake Suzan Maona (2)
Pendo Sengerema, akiwa  pichani katika kituo hicho cha kulelea watoto wenye uleamavu wa Ngozi  ambaye akikatwa Mkono wake waka 2014 huko Kaliua Tabora,  
Raisi Mstaafu wa Chama cha  Madaktari wa Kinywa na Meno na Daktari Bingwa wa Watoto  Rachel Mhavile  toka Hospitali ya Taifa  Muhimbili, akifanya ukaguzi wa kinywa na Meno kwa Janeth Peter katika kituo Buhangija kilichopo Shinyanga  na  wengine kushuhudia elimu hiyo

Maria Michael mweuono hafifu akifatilia jambo wakati ilipokuwa ikitolewa huduma hiyo
Daktari wa Meno wa Wilaya ya Ngara -Kagera Devid Mapunda akiwa amewabeba watoto hao
Watoto hao wakiwa wanacheza
Raisi Mstaafu wa Chama cha  Madaktari wa Kinywa na Meno na Daktari Bingwa wa Watoto  Rachel Mhavile  toka Hospitali ya Taifa  Muhimbili, akimwangalia Mmoja wa Mtoto Mwenye ulemavu wa kutosikia Samira  Fadhili  wakati wa wiki ya Kinywa na Meno ambaye anasoma katika shule ya Buhangija ,wakwanza kulia ni  Mkuu wa Kitengo wa watoto Wenye Ulemavu wa kuto sikia na  mwalimu wa Shule hiyo   Loyce Daudi , akitoa tofasili kwa watoto hao wasio sikia waweze elewa kinacho endelea hapo

Wakisubiri kupata huduma ya Kinywa na Meno
Raisi Mstaafu wa Chama cha  Madaktari wa Kinywa na Meno na Daktari Bingwa wa Watoto  Rachel Mhavile  toka Hospitali ya Taifa  Muhimbili, akitoa elimu kwa watoto wakuto sikia na kulia kwake ni    Mkuu wa Kitengo wa watoto Wenye Ulemavu wa kuto sikia na  mwalimu wa Shule hiyo   Loyce Daudi , akitoa tofasili kwa watoto hao wasio sikia waweze elewa kinacho endelea hapo
Vijana hao Wakiosha Vinywa vyao baada ya kupata huduma ya Kinywa na Meno toka kwa Madaktari Wachama hicho
Kaimu Mganga wa  Meno Mkoa Shinyanga Dr. Maguja Daniel, akiongea na Timu ya  Chama cha Madaktari wa Kinywa na Meno walipofika katika Hospitali ya Mkoa Shinyanga.
Daktari wa Kinywa na Meno akimtibia Mtoto Mwenye ulemavu wa Ngozi waliopo katika kituo cha Buhangija









    MADAKTARI KUTOKA KATIKA CHAMA CHA MADAKTARI WA KINYWA NA MENO TANZANIA WAMETOA HUDUMA YA BURE KWA WATOTO MIA TATU NA THELATHINI NA SABA WENYE ULEMAVU WA NGOZI,VIZIVI NA WASIOONA WANAOLELEWA KATIKA KITUO CHA BUHANGIJA KILICHOKO MKOANI SHINYANGA NA HII NI KATIKA KUELEKEA KILELE CHA MADHIMISHO YA KILELE CHA SIKU AFYA YA KINYA NA MENO DUNIANI INAYO ADHIMISHWA KILA TAREHE 20 YA MWEZI WA 3 KILA MWAKA.

KHAMISI MUSSA, nikiripoti kutoka SHINYANGA.


AKIZUNGUMZA NA ITV KIONGOZI WA MSAFARA WA MADAKTARI WATAALAM WA KINYWA NA MENO Dr. RACHEL MHAVULLE AMESEMA LENGO LA KUTEMBELEA KITUO HIKI NI KUTOA ELIMU JUU YA KUTUNZA KINYWA NA MENO PAMOJA NA KUWATIBU KWAKUA KUNDI HILI NI KUNDI LILIKLOKO PEMBEZONI NA LIMESAHAULIKA HIVYO AMEWAOMBA WADAU WENGINE KUTEMBELEA KITUO HIKI NA KUTOA MSAADA WAO ILI KUTUNZA AFYA ZA WATOTO HAO WANAOISHI KATIKA MAZINGIRA MAGUMU.

Dr. Rachel Mhaville Kiongozi wa msafara wa madaktari wa afya ya kinywa na meno.


NAYE MKUU WA KITUO CHA KULELEA WALEMAVU HAO Bw. PETER AJALI AMESEMA MBALI NA CHANGAMOTO NYINGI ZINAZOKIKABILI KITUO HICHO WAZAZI WENGI WAMETELEKEZA WATOTO BAADA YA KUWAFIKISHA KITUONI HALI INAYOSABABISHA WATOTO KUTESEKA KWA MAGONJWA MBALIMBALI YAKIWEMO YA KINYWA NA MENO HUKU MLEZI WA KITUO HICHO AMBAYE NAYE NI MLEMAVU WA NGOZI DIGNA MWACHA AMESEMA KITUO KIMEFARIJIKA  SANA KUFIKIWA NA MADAKTARI HAO KUTOKA KATIKA CHAMA CHA MADAKTARI WA KINYWA NA MENO KWAKUWA NI TATIZO LINALOSUMBUA SANA WATOTO KITUONI HAPO  KWAHIYO UJIO WAO UTASAIDIA KUPUNGUZA SANA MATATIZO HAYO.

Peter Ajali mkuu wa kituo na Digna Mwacha mlezi katika kituo cha buhangija.


NAO WATOTO WALIOPATA HUDUMA HIYO WAMEONYESHA FARAJA YAO BAADA YA KUPATA HUDUMA NA WAMEIOMBA SERIKALI NA WADAU WENGINE KUENDELEA KUWAPA HUDUMA WATOTO WENYE ULEMAVU KWAKUWA WANAHITAJI HUDUMA KAMA WATOTO WENGINE.

 PICHA ZOTE na ujijirahaa Blog na theNkoromo Blog.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages