Mkuu
wa Chuo cha Takwimu Mashariki mwa Afrika (EASTC) Prof. Innocent
Ngalinda akizungumza na Waandishi wa Habari leo jijini Dar es Salaam
kuhusu kukamilika kwa maadalizi ya kutiliana saini ya Mkataba wa
Makubaliano ya Mafunzo ya Watalaam wa Takwimu wa chuo hicho na Chuo cha
Takwimu cha nchini India utakaosainiwa tarehe 28 Machi, 2015. (Picha
zote na Veronica Kazimoto)
Naibu
Balozi wa India nchini Balvinder Humpal akiwaelezea Waandishi wa Habari
jinsi alivyofurahishwa na maadalizi ya kutiliana saini ya Mkataba wa
Makubaliano ya Mafunzo ya Watalaam wa Takwimu wa Chuo cha Takwimu
Mashariki mwa Afrika na Chuo cha Takwimu cha nchini India utakaosainiwa
tarehe 28 Machi, 2015.
Naibu
Balozi wa India nchini Balvinder Humpal akimsalimia mwanafunzi wa
Udhamili katika Takwimu Rasmi Happiness Katuma wakati akikagua baadhi ya
vitu mbalimbali
kama maadalizi ya kutiliana saini ya Mkataba wa Makubaliano ya Mafunzo
ya Watalaam wa Takwimu wa Chuo cha Takwimu Mashariki mwa Afrika na Chuo
cha Takwimu cha nchini India utakaosainiwa tarehe 28 Machi, 2015.
Naibu
Balozi wa India nchini Balvinder Humpal akipitishwa katika maeneo
mbalimbali ya Chuo cha Takwimu Mashariki mwa Afrika kama maadalizi ya
kutiliana saini ya Mkataba wa Makubaliano ya Mafunzo ya Watalaam wa
Takwimu wa chuo hicho na Chuo cha Takwimu cha nchini India utakaosainiwa
tarehe 28 Machi, 2015.
Naibu
Balozi wa India nchini Balvinder Humpal akiangalia vitabu mbalimbali
vilivyopo katika maktaba ya Chuo cha Takwimu Mashariki mwa Afrika wakati
wa kuangalia maadalizi ya kutiliana saini ya Mkataba wa Makubaliano ya
Mafunzo ya Watalaam wa Takwimu wa Chuo cha Takwimu Mashariki mwa Afrika
na Chuo cha Takwimu cha nchini India utakaosainiwa tarehe 28 Machi,
2015.
Naibu
Balozi wa India nchini Balvinder Humpal akisoma moja ya vitabu
kilivyopo katika maktaba ya Chuo cha Takwimu Mashariki mwa Afrika wakati
wa kuangalia maadalizi ya kutiliana saini ya Mkataba wa Makubaliano ya
Mafunzo ya Watalaam wa Takwimu wa Chuo cha Takwimu Mashariki mwa Afrika
na Chuo cha Takwimu cha nchini India utakaosainiwa tarehe 28 Machi,
2015.
Mkuu
wa Chuo cha Takwimu Mashariki mwa Afrika (EASTC) Prof. Innocent
Ngalinda akimwelezea Naibu Balozi wa India nchini Balvinder Humpal
kuhusu chumba cha kompyuta kilichopo chuoni hapo wakati wa kuangalia
maadalizi ya kutiliana saini ya Mkataba wa Makubaliano ya Mafunzo ya
Watalaam wa Takwimu wa Chuo cha Takwimu Mashariki mwa Afrika na Chuo cha
Takwimu cha nchini India utakaosainiwa tarehe 28 Machi, 2015.
Na Veronica Kazimoto
Dar es Salaam,
17 Machi, 2015.
CHUO
cha Takwimu Mashariki mwa Afrika (EASTC) kimekamilisha maadalizi ya
kutiliana saini ya mkataba wa makubaliano ya mafunzo ya Watalaam wa
Takwimu na Chuo cha Takwimu cha nchini India.
Akizungumza
na Waandishi wa Habari leo jijini Dar es Salaam Mkuu wa Chuo cha EASTC
Prof. Innocent Ngalinda amesema mkataba huo utasainiwa tarehe 28 Machi,
2015.
“Maandalizi
ya kutiliana saini ya Mkataba wa Makubaliano ya Mafunzo ya Watalaam wa
Takwimu na Chuo cha Takwimu cha nchini India yamekamilika kwa kiasi
kikubwa na ndio maana hapa mbele yenu mnamuona Naibu Balozi wa Ubalozi
wa India hapa nchini amefika kwa ajili ya kujirizisha”, amesema Prof.
Ngalinda.
Prof.
Ngalinda amesema kuwa mkataba huo una manufaa makubwa kwa kuwa
utasaidia kuongezeka kwa wataalam wengi katika tasnia ya takwimu hapa
nchini.
Pamoja
na ongezeko la watalaam wa takwimu hasa wakufunzi, kutakuwa na
ukarabati wa miundombinu katika chuo hicho ambapo mabweni ya wanafunzi
pamoja na ofisi za chuo hicho zitakarabatiwa.
Prof.
Innocent Ngalinda amefafanua kuwa katika mkataba huo, kutakuwa na
mpango wa kubadilishana wanafunzi katika vyuo hivyo viwili ili kupanua
uelewa wa wanafunzi ikiwa ni pamoja na kuongeza ujuzi zaidi katika
masuala ya kitakwimu.
Kwa
upande wake Naibu Balozi wa India nchini Balvinder Humpal amefurahishwa
na maandalizi yaliyofanyika na kusema kuwa nchi yake iko tayari
kutiliana saini ya mkataba wa makubaliano ya mafunzo ya Watalaam wa
Takwimu kutoka chuo cha Takwimu Mashariki mwa Afrika na chuo cha Takwimu
cha nchini India.
“Nimefurahishwa
na maandalizi yaliyofanyika katika chuo hiki na sasa tunamsubiri Waziri
wa mambo ya Nje wa nchini India kwa ajili ya kutiliana saini ya mkataba
huu ifikapo tarehe 28 Machi, 2015,” amesema Naibu Balozi Humpal.
Chuo
cha Takwimu Mashariki mwa Afrika kilichopo Changanyikeni jijini Dar es
Salaam na chuo cha Takwimu cha India vimekuwa vikishirikiana tangu mwaka
2012 lakini ushirikiano huo haukuwa rasmi hivyo vyuo hivyo vimeamua
kusaini mkataba wa makubaliano kwa ajili kufanya ushirikiano huo kuwa
rasmi.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269