Na Woinde
Shizza, Arusha
Bendi ya FM Academia 'Wazee wa Ngwasuma
wanatarajiwa kuwasha moto ndani ya ukumbi mpya wa kisasa
ujulikanao kwa jina la Flomena uliopo wilayani hai mkoani
Kilimanjaro usiku wa
jumatatu ya pasaka .
Akizungumza na waandishi wa habari
muandaaji wa onyesho hilo Swaum kileo alisema kuwa ameamua
kuwaleta
bendi hiyo katika uzinduzi huo ili kuweza kuwafurahisha wananchi wa mkoa wa
kilimanjaro na mikoa jirani katika sikukuu hiii ya pasaka
.
Alisema kuwa bendi hii inamda
mrefu sana aijafika wilayani hai ivyo wameamu kuileta ili wakazi wa wilaya hiyo
nao wafurahie mziki wa dance unaofanywa na bendi hiyo
.
Alitaja kiingilio cha onyesho hiyo kuwa ni
shilingi 10000 za kitanzania
huku akiwataja wathamini wa onyesho hilo kuwa ni Swaum fashion ,Tbl , libeneke
la kaskazini blog pamoja , faraja saloon pamoja na Radio
five.
Kwa upande wa meneja wa bendi ya FM
Academia kelvin mkinga aliema kuwa wamejipanga vyema kuwapa
burudani ya kutosha wakazi wa wilaya ya hai mkoa mzima wa Kilimanjaro pamoja na
mikoa jirani na kwa upendeleo
watawatambulisha nyimbo zao mbalimbali mpya ambazo wameziandaa na wanatarajia
kuzi zindua hivi karibuni.
Alisema kuwa pia wapenzi wake watakuwa na
bahati zaidi kwani show hii ndio itakuwa ya kwanza mara
baada
ya kutoka katika shindano lao na bendi
ya twanga pepeta
kwa upande wa Rais wa bendi hiyo Nyoshi El-Sadat alisema kuwa timu yake yote
imejipanga
vyema kuwapa burudani ya nguvu wakazi wa wilaya ya hai na mkoa mzima huku
akisema kuwa atawapa staili zote za
gwasuma ikiwemo ile ya vundesa ambapo alisema kuwa wameiboresha na
imekuwa ya kiufasaha zaidi na ina vinjonjo vingi zaidi ,staili
tamu pamoja na maneno
matamu.
“tunatarajia kufanya show ya kihistoria ambayo aijawai
kufanyika mkoani Kilimanjaro nah iii yote ni kwa ajili
ya kuwaburudisha wapenzi wetu wa mziki wa dance wapenzi wetu wa bendi yetu ya
fm academia”alisema nyoshi
Aidha alisema kuwa amewaandalia zawadi kubwa
wapenzi wake wa mkoa wa huo pamoja na
mikoa jirani kwani watamuoana akiwa na muonekano mpya ambao hawajawai
kuuona.
ni pamoja na
kuwaelewesha wapenzi wao nyimbo
mpya na kuakikisha wapenzi wao wanajua staili zao zote za nyimbo hizo
na sio ivyo tu pia alisema kuwa kwa kipindi hiki wanataka kuwa
wakazi wa arusha zawadi ya kuwaletea wasanii wote wa bendi hiyo ambapo alisema
wapo 32 na wote watafika jijini Arusha
chanzo :libeneke la kaskazini blog
chanzo :libeneke la kaskazini blog
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269