Katibu Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Anna Maembe, akifuatilia hitimisho la Mkutano wa 59 wa Kamisheni kuhusu Hadhi ya Wanawake. Kushoto ni Ndugu, Jaji Angela Kileo
------------------------
Na Mwandishi Maalum, New York
Mkutano wa 59 wa Kamisheni kuhusu Hadhi ya Wanawake umemalizika kwa kutoka na maazimio mbalimbali likiwamo linalobainisha kuwa tofauti zote za usawa wa kijinsia zinamalizwa ifikapo mwaka 2030.
Mkutano huo wa wiki mbili na ambao umehudhuriwa na mamia ya wawakilishi kutoka mataifa ambayo ni wanachama wa Umoja wa Mataifa, Taasisi za UM na Asasi zisizo za Kiserikali pia ulipitisha kwa kauli moja tamko la kisiasa ambalo limeainsha na kuazimia mambo kadha kwa kadha yanayohusu fursa sawa za kijinsia na uwezeshaji wa mwanamke.
Ujumbe wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Mkutano huu, uliongozwa na Mhe. Sophia Simba ( Mb), Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto.
Kupitia mkutano huo wajumbe hao walijadiliana na kubadilishana mawazo kuhusu mafanikio katika utelekezaji wa maazimio mbalimbali yaliyokubalika wakati wa Mkutano wa kihistoria wa wanawake uliofanyika Beijing mwaka 1995 pamoja na changamoto zake.
Akihitimisha mkutano huo Katibu Mkuu Msaidizi Mwandamizi na Mkurugenzi Mtendaji wa UN- Women, Bibi. Phumbzile Malambo-Ngacuka amesema mwaka 2030 lazima uwe hitimisho la utofauti wa kijinsia jukumu linalotakiwa kufanyiwa kazi kuanzia ngazi ya familia, kijamii, kisiasa na kiuchumi.
Naye Mwenyekiti wa Kamisheni Bi Kandra Vajarabhaya akizungumzia mwenendo mzima wa mkutano huo anamesema, kwa wajumbe kupitisha kwa kauli moja tamko la kisiasa, kamisheni hiyo imerejea wajibu wake wa kuchagiza na kufanikisha upatikanaji wa fursa sawa za kijinsia, uwezeshaji wa wanawake pamoja na kuhakikisha haki za wanawake na watoto wa kike.
Akatoa pia tathimini ya utekelezaji wa maazimio pamoja na Jukwaa la utekelezaji wa mkutano wa Beijing pamoja na changamoto zilizobakia.
Kupitia mchakato huu Bi Vajarabhaya amesema wajumbe wamemejifunza kwamba bado kuna changamoto , na kwamba mkutano wa kamisheni hiyo umetoka na mapendekezo kadhaa ya kuimarisha utendaji wa chombo hicho.
Pamoja na majadilianao ya ajenda mbalimbali mkutano huo umepitisha maazimio manne likiwano linalohusu namna ya kuwasaidia wanawake wa Palestina, azimio hilo lilipitishwa kwa kupigiwa kura ambapo kura 27 ziliunga mkono azimio hilo huku mbili ( Israel na Marekani ) zikilipinga.
Mwakilishi wa Kudumu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, Balozi Tuvako Manongi akiwa na wajumbe wa Tanzania waliohudhuria na kushiriki Mkutano wa 59 wa Kamisheni kuhusu Hadhi ya Wanawake ( CSW) mara baada ya kufungwa kwa mkutano huo wa wiki mbili jana Ijumaa ya wiki iliyopita.
Naibu Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, Balozi Ramadhan Mwinyi akiwa na wajumbe kutoka Zanzibar waliohudhuria mkutano wa 59 wa CSW
Baadhi ya ya Ujumbe uliotoka Tanzania, wakifuatilia uhitimishwaji wa Mkutano wa 59 wa CSW
Your Ad Spot
Mar 25, 2015
Home
Unlabelled
MWAKA 2030 UWE MWISHO WA TOFAUTI YA USAWA WA KIJINSIA-UN
MWAKA 2030 UWE MWISHO WA TOFAUTI YA USAWA WA KIJINSIA-UN
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post Top Ad
Your Ad Spot
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269