Ni mengi ambayo yamesikika kuhusu Mbunge Zitto Kabwe siku
za hivi karibuni, mojawapo ni ishu ya Mbunge huyo kusimamishwa
Uanachama wa CHADEMA na pia akaamua kwenda kuongea na Wapigakura wake
kwamba hatogombea tena nafasi hiyo.
Huenda kuna vitu hukuwahi kumsikia akizungumzia, mojawapo ni ishu ya usalama wake; “Suala
la usalama sina tatizo kabisa kwa sababu ninachokifanya ni majukumu ya
Kikatiba.. Wananchi wanachagua kundi la Wabunge 350 kwa ajili ya kazi
tatu.. uwakilishi, kutunga Sheria na kuisimamia Serikali.. Hamjawahi
kunisikia nalalamika kuhusu usalama, likitokea limetokea huwezi jua
binadamu wanapanga nini…”
Zitto Kabwe anazungumzia miaka miwili ambayo ilikuwa migumu sana kwake kwenye siasa; “Kwanza 2007 wakati nimetoa hoja ya BUZWAGI.. Kipindi
kile ilikuwa ni vigumu sana kwa Mbunge kusimama na kumwambia Waziri wa
Serikali kamba umesema uongo.. Nikasimamishwa Ubunge kwa miezi minne..“
2014
pia ulikuwa ni mwaka mgumu na una sababu mbalimbali. Kwa mara ya kwanza
nilijikuta nakwenda Mahakamani kwa ajili ya kutetea haki yangu
kuhusiana na uanachama wangu kwenye chama.. Lakini ndio mwaka huo huo
ambao nikawa na hoja nzito sana kwenye Bunge, hoja ya Escrow..“– Zitto KABWE.
Zitto Kabwe "Wakati
wa sakata la Escrow bungeni, kuna mjumbe mmoja wa PAC aliitwa na vinara
wa watuhumiwa wa Escrow na kutakiwa kusema uongo bungeni kuhusu mimi
kwa ahadi ya kupewa donge nono,
mjumbe huyo alikataa, na hapo ndipo vinara hao wa Escrow wakaapa
kutenga Shilingi Milion 500 kwa kila jimbo la kila mjumbe wa PAC
kuhakikisha kuwa wajumbe hao wote hawarudi bungeni.
Kwahiyo nahisi kuwa hiki kilichonitokea sasa ni sehemu ya mkakati huo maana sakata la escrow limegusa wengi, hadi majaji wamo.”
Kwahiyo nahisi kuwa hiki kilichonitokea sasa ni sehemu ya mkakati huo maana sakata la escrow limegusa wengi, hadi majaji wamo.”
Zitto Kabwe“Kama
Katiba ingebadilishwa kabla ya uchaguzi mkuu 2015 na ikaruhusu mgombea
urais mwenye umri chini ya miaka 40, ningegombea urais, nahitaji
kuongoza nchi, kwa ubunge imetosha, lakini kwa kuwa haiwezekani, nitagombea ubunge lakini si Kigoma Kaskazini, nitatafuta jimbo linguine la kugombea ili nao nikawatumikie, Kigoma Kaskazini nimeshafanya kila kitu, sitakuwa na jipya”
Hii ni sehemu ya mahojiiano ya Mbunge huyo kwenye kipindi cha Dakika 45 cha ITV kilichoruka March 16.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269