Mabingwa watetezi wa ligi kuu ya Tanzania bara, Azam FC,
leo March 16, 2015,wamefanikiwa kutinga katika kilele cha ligi hiyo
baada ya kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya wageni wao Ndanda FC
kutoka Mtwara.
Azam
FC walipata bao lao kupitia kwa kinara wa kufumania nyavu katika ligi
kwa sasa, Didier Kavumbagu, kunako dakika ya 24 kipindi cha kwanza baada
ya kumalizia kazi safi iliyofanywa na Muivory Coast, Kipre Herman
Tchetche.
Kufatia
bao hilo la Kavumbagu, Mshambuliaji huyo wa Timu ya Taifa ya Burundi,
anakuwa anazidi kujichimbia katika kusaka kiatu cha mcheka na nyavu
(Mfungaji bora wa ligi) akiwa amefikisha mabao 10 sasa.
Azam FC ilikuwa ikiongozwa na Kocha George ‘Best’ Nsimbe pamoja na Msaidizi wake, Denis Kitambi,
hii ni baada ya Uongozi wa Matajili hao kumtimua aliyekuwa kocha mkuu,
Mcameroon Joseph Omog, Siku chache aliposhindwa kuibakisha Azam FC
katika michuano ya Klabu B ingwa Afrika dhidi ya El Merreikh ya Sudan.
Kwa ushindi huo Azam FC wanakuwa wamejikita katika usikani wa ligi wakiwa na pointi 33 mbele ya Yanga SC wenye pointi 31 na Simba SC wenye alama 29.
|
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269