Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama
Cha Mapinduzi (CCM), Nape Nnauye ambaye ameambatana na Katibu Mkuu wa
chama hicho, Abdulrahman Kinana katika ziara ya Mkoa wa Arusha,
akihutubia jioni ya leo katika mkutano wa hadhara uliofanyika mjini
Karatu. (Picha zote na Kamanda Richard Mwaikednda wa Kamanda wa Matukio
Blog)
Katibu Mkuu wa CCM,
Abdulrahman Kinana akihutubia katika mkutano wa hadhara mjini Karatu
jioni ya leo, ambapo aliwasihi wananchi wa wilaya hiyo ambayo
inaoongozwa na Chadema, kuachana nacho kwani kwa muda wa miaka kumi na
mitano iliyoongoza hakuna maendeleo yoyote waliyowaletea zaidi kutumia
ovyo fedha zinazopekwa na Serikali wilayani humo kwa ajili ya miradi ya
maendeleo.Halmashauri ya Wilaya hiyo inaoongwa na Chadema.
Kinana ambaye yupo mkoani Arusha kwa
ziara ya kuimarisha uhai wa chama, kukagua miradi inayotekelezwa kwa
kufuata Ilani ya Uchaguzi ya CCM, pamoja na kusikiliza kero za Wananchi
na kuzitafutia ufumbuzi, alishuhudia Halmashauri ya Karatu inayoongozwa
na Chadema imekataa kutoa sh. mil 60 zilizotolewa na Serikali Kuu kwa
ajili ya ujenzi wa Kituo cha Afya cha Baray Mbuga Nyekundu, kisa Kata
hiyo inaongozwa na Diwani wa CCM.
Nape akihutubia katika mkutano huo uliofurika watu kwenye Uwanja wa Mazingira mjini Karatu.
Wananchi wakishangilia wakati wa mapokezi ya Komredi Kinana alipowasili Wilaya ya Karatu akitokea Wilaya ya Ngorongoro.
Wananchi wakishangilia wakati wa mapokezi ya Komredi Kinana alipowasili Wilaya ya Karatu akitokea Wilaya ya Ngorongoro.
|
Wananchi wakimshangilia Katibu wa
Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye alipokuwa akihutubia katika Kata
ya Baray, ambapo Komrdi Kinana alishiriki ujenzi wa Kituo cha Afya cha
Baray, ambacho fedha zilizotengwa na Serikali Kuu sh. mil 60 kwa ajili
ya ujenzi huo zilizuiwa na Halmashauri ya Wilaya ya Karatu inaoongozwa
na Chadema kwa madai kwamba Kata hiyo inaoongozwa na CCM.
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman
Kinana akihutubia baada ya kushiriki ujenzi wa Jengo la Upasuaji ala
kituo cha Afya cha Baray, ambapo alikemea kitendo cha Uongozi wa
Halmashauri ya Wilaya ya Karatu kuzuia sh. mil. 60 zilizotolewa na
Serikali Kuu za ujenzi wa jengo hilo na kuwataka waache kabisa tabia
hiyo.
Komredi Kinana akishiriki ujenzi wa jengo la upasuaji katika Kituo cha Afya cha Baray.
Komredi Kinana akivuka kwenye
kidaraja alipokuwa akienda kukagua mfereji wa umwagiliaji mashamba ya
vitunguu na kushiriki kupanda zao hilo katika Kata ya Mang'ola, wilayani
Karatu.
Kinana akishiriki kupanda zao la
vitunguu katika mashamba ya Mang'ola.Mango'ola inaongoza kwa uzalishaji
wa vitunguu vizuri Afrika Mashariki na Kati.
Kinana na viongozi wengine wa chama na Seriksli wakielekea kwenye mkutano wa hadhara katika Kata ya Mang'ola.
Komredi Kinana akihutubia katika
mkutano huo uliofanyika katika Kata ya Mang'ola, inayoongozwa na
Chadema, ambapo wananchi wa eneo hilo walimuomba awatatulie matatizo
mbalimbali yanayowakabili ambayo kwa asilimia kubwa yamesababishwa na
uongozi wa Chadema.
Wananchi wakimkaribisha Komredi Kinana kushiriki ujenzi wa jengo la CCM, Tawi Kilimatembo, wilayani Karatu.
Komredi Kinana akiteremka kwenye ngazi baada ya kushiriki ujenzi wa jengo la tawi hilo.
Komredi Kinana akitoka kukagua jengo la Serikali ya Kijiji cha Kilimatembo Kata ya Rhotia, wilayani Karatu.
Wananchi wakimkaribisha Komredi Kinana kwa shangwe alipofika kufungua rasmi jengo la CCM Tawi la Rhotia.
Komredi Kinana akihutubia wananchi baada ya kufungua rasmi jengo la kitegauchumi la CCM Tawi la Rhotia.
Nape Nnauye akihutubia katika mkutano wa hadhara uliofanyika leo kwenye Uwanja wa Mazingira mjini Karatu. |
Vijana wa Green Guard wa CCM,
wakijadiliana jambo walipokuwa wakingalia kwenye simu picha zilizopigwa
wakati wa mkutano huo wa hadhara.
|
Sehemu ya umati wa watu katika mkutano huo.
Mmoja wa wanachama wapya wa CCM
walioihama Chadema, akielezea jinsi chama hicho kilivyowatesa kwa
takribani miaka mitano kwa kutowaletea maendeleo.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269