Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Said Meck Sadiki na
Mbunge wa Ubungo Mhe. John Mnyika wakifungua maji ya bomba kwenye
Zahanati ya Kijiji cha Mpiji Magohe mara baada ya kuzindua mradi wa maji
katika kijiji hicho manispaa ya Kinondani jijini Dar es Salaam.(Photo zote na Aron Msigwa-MAELEZO)
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Said Meck Sadiki akizindua Tenki la kuhifadhia maji katika
kijiji cha Mpiji Magohe, manispaa ya Kinondani jijini Dar es salaam leo
wakati wa mwendelezo wa maadhimisho ya Wiki ya Maji yanayoendelea
mkoani Dar es salaam.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Said Meck Sadiki akizindua Tenki la kuhifadhia maji katika
kijiji cha Mpiji Magohe, manispaa ya Kinondani jijini Dar es salaam leo
wakati wa mwendelezo wa maadhimisho ya Wiki ya Maji yanayoendelea
mkoani Dar es salaam.
Mkuu
wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Said Meck Sadiki akizungumza na wakazi wa
kijiji cha Mpiji Magohe Kata ya Mbezi, manispaa ya Kinondoni jijini Dar
es salaam mara baada ya kuzindua mradi wa maji wa kijiji hicho leo.
Mbunge
wa Ubungo Mhe. John Mnyika akizungumza na wa kijiji cha Mpiji Magohe
Kata ya Mbezi, manispaa ya Kinondoni jijini Dar es salaam mara baada ya
kuzindua mradi wa maji wa kijiji hicho leo.
Na Aron Msigwa – MAELEZO
19/3/2015.
Dar es Salaam.
Wakazi
wa kijiji cha Mpiji Magohe, Kata ya Mbezi wilayani Kinondoni jijini Dar
es salaam wamekubali kuyatoa maeneo ya ardhi wanayomiliki bila fidia
ili yaweze kutumiwa na Shirika la Ugavi wa Umeme nchini (TANESCO)
kupitisha nguzo za umeme kuelekea mahali ilipo pampu ya kusukuma maji kwenye chanzo cha maji kijijini hapo ili waweze kupata huduma ya uhakika ya maji kutokana na chanzo hicho kutumia umeme wa jenereta.
Wananchi
hao wametoa uamuzi huo leo mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe.
Saidi Meck Sadiki ambaye alikuwa mgeni rasmi wakati wa maadhimisho ya
Wiki ya Maji kijijini hapo, yaliyoambatana na uzinduzi wa mradi
wa maji wa kijiji hicho uliogharimu kiasi cha fedha za kitanzania zaidi ya shilingi milioni 460.
Akizungumza na wakazi hao, Mhe. Sadiki amesema kuwa kukamilika
kwa mradi ni moja ya juhudi za Serikali za kuhakikisha wananchi
wanapata maji safi katika maeneo yao na kuongeza kuwa mradi huo utawanufaisha zaidi ya watu 6600 wa kijiji hicho na kuondoa kero ya kupata maji safi iliyodumu kwa zaidi ya miaka 20.
Amesema
kuwa uamuzi walioufanya wananchi hao kuruhusu maeneo yao kupitisha
nguzo za umeme bila kudai fidia ni wa kipekee na unafaa kuigwa na
wananchi wa maeneo mengine ili kurahisisha upatikanaji wa huduma zao za
msingi na kuwaahidi wananchi hao kuwa atawasiliana na mamlaka husika ili
umeme wa TANESCO uweze kufika katika chanzo chao cha maji kupunguza
gharama za uendeshaji na kuharakisha kukamilishwa kwa mradi huo.
Ameitaka
kamati ya maji inayosimamia mradi wa kijiji hicho kuhakikisha kuwa
inafanya kazi kwa ufanisi, uadilifu na uwazi ili kuondoa migogoro ya
uongozi na wananchi hali inayoweza kutishia uhai wa mradi huo.
“Natoa
agizo kwa viongozi wa kamati ya maji ya kijiji hiki muhakikishe kuwa
mnafanya kazi zenu kwa ufanisi mkubwa, uadilifu, mzingatie sheria na
kuhakikisha taarifa za fedha za mradi hasa mapato na matumizi mnazitoa
kwa wananchi kila baada ya miezi 3 kulingana na mwongozo uliopo”
Amesisitiza.
Kuhusu
maadhimisho hayo ya wiki ya Wiki ya Maji ambayo huadhimishwa duniani
kote kila ifikapo Machi 16 hadi 22 kila mwaka kuanzia ngazi ya taifa,
mkoa na wilaya amesema kwa mwaka huu jijini Dar es salaam maadhimisho
hayo yameambatana na uzinduzi wa miradi ya maji katika maeneo
mbalimbali, utoaji wa elimu kuhusu huduma za maji , utunzaji wa vyanzo
vya maji na miundombinu ya maji kote nchini.
Amesema maadhimisho
ya mwaka huu pia yanawakutanisha wananchi na taasisi za uendeshaji
huduma, usimamizi na usambazaji wa maji ambazo hutoa elimu kuhusu huduma
za maji wanazotoa, kupokea maoni na kero za wananchi na kuendesha
operesheni mbalimbali za kuwakamata baadhi ya watu wanaoiba maji na
kuhujumu miundominu ya maji nchini.
Kuhusu
usambazaji wa maji katika maeneo mengine amesema kuwa uchimbaji wa
visima 20 awamu ya kwanza imeanza na itakamilika mwezi Agosti mwaka huu
ikihusisha upanuzi wa mtandao wa usambazaji wa maji katika maeneo yaliyo
kandokando ya mabomba makuu kutoka Ruvu chini na Ruvu juu na
kuvinufaisha vitongoji vilivyopo kati ya mji wa Bagamoyo hadi eneo la
Tegeta-Mpiji na vitongoji vilivyopo kati ya mji wa Mlandizi –Kiluvya na
maeneo ya Mbezi, Kimara na Goba.
Awamu
ya pili itahusisha upanuzi wa mfumo wa usambazaji wa maji katika maeneo
yote ya jiji yatakayopata maji kutoka Kimbiji na Mpera na maeneo
mengine ya jiji yasiyo na mabomba ya usambazaji wa maji.
Kwa
upande wake Mbunge wa jimbo la Ubungo Mhe. John Mnyika akizungumza na
wakazi wa Mpiji Magohe ameishukuru Serikali na wananchi wa kijiji cha
Mpiji Magohe kwa kutoa ushirikiano ambao umefanikisha kukamilika kwa mradi huo.
Amesema yeye kama mbunge wa eneo hilo ataendelea kushirikiana na viongozi wa Serikali
wa mkoa wa Dar es salaam kuhamasisha maendeleo ya wananchi kushirikiana
kikamilifu katika ujenzi wa miundombinu ya barabara na maji na kutoa
wito kwa wananchi kuhakikisha wanalinda vyanzo vya maji na kutunza
miundombinu iliyowekwa ili iendelee kuwa na manufaa kwa kipindi kirefu.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269