Mabingwa wa ligi ya Uingereza Manchester
City watamuuza Yaya Toure msimu huu katika mpango unaolenga kuwauza
wachezaji wengine wa kilabu hiyo kwa lengo la kununua wachezaji
chipukizi watakaoongozwa na mchezaji Kevin De Bruyn wa Wolfsburg.
Kushindwa kwa kilabu hiyo na Barcelona
katika mechi ya kufuzu kwa robo fainali ya kombe la vilabu bingwa Ulaya
kumethibitisha kwamba mabadiliko makubwa yanahitajika katika kilabu
hiyo.
Katika wachezaji kumi na moja
walioanzishwa katika mechi dhidi ya Barcelona ni Sergio Aguerro mwenye
umri wa maka 26 aliye chini ya umri wa miaka 27.
Huku Aguerro,Joe Hart,Vincet
Kompany,Fernandinho na David Silva wakiwa na maisha marefu katika kilabu
hiyo ,waliosalia huenda wakauzwa.
Hii inamaanisha kwamba Yaya Toure,Bacary
Sagna,Martin Demichelis,Alkesandar Kolarov ,Samir Nasri na James Milner
ambaye kandarasi yake inaisha hatma yao haijulikani.
Kati ya wachezaji ambao hawakuanzishwa
katika uwanja wa Nou Camp siku ya jumatano usiku,Gale Clichy,Pablo
Zabaleta,Jesus Navas,Fernandinho,Steven Jovetic na Edin Dzeko huenda pia
wakauzwa.
Frank lampard amesema kuwa anaondoka ili kujiunga na kilabu ya New York City nchini Marekani.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269