Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed
Shein akisalimiana na Mwenyekiti wa Kampuni ya Vigor Turky Salim Hassan
Turky wakati alipofika kufungua Hospitali ya Global Hospital iliyopo Mtaa
wa Vuga Mjini Unguja leo. (Picha zote na Ikulu)
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed
Shein akifungua pazia kufungua Hospitali ya Global Hospital
iliyopo Mtaa wa Vuga Mjini Unguja leo. Wa pili kulia ni Mwenyekiti wa Kampuni ya
Vigor Turky Salim Hassan Turky
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed
Shein akipeana mkono wa pongezi na Mwenyekiti wa Kampuni ya Vigor Turky
Salim Hassan Turky baada kuifungua Hospitali ya Global Hospital iliyopo
Mtaa wa Vuga Mjini Unguja leo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed
Shein akikata utepekuifungua Hospitali ya Global Hospital iliyopo Mtaa wa
Vuga Mjini Unguja leo (kushoto ni Dkt. K. Ravindranath Daktari Mkuu na Mwenyekiti
wa Kampuni ya Global Hospital (kulia) Mwenyekiti wa Kampuni ya Vigor
Turky Salim Hassan Turky.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed
Shein (wa pili kulia) akipata maelezo alipotembelea mashine ya Xray baada ya kuifungua Hospitali ya
Global Hospital iliyopo Mtaa wa Vuga Mjini Unguja leo (wa kwanza kulia)
Dkt. K. Ravindranath Daktari Mkuu na Mwenyekiti wa Kampuni ya Global Hospital.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed
Shein (katikati) akiwa na Daktari Mkuu na Mwenyekiti wa Kampuni ya Global
Hospital Dkt. K. Ravindranath (wa pili kulia)
na Mwenyekiti wa Kampuni ya Vigor Turky Salim Hassan Turky
wakiangalia mashine ya kufanyia Upasuaji wakati alipotembelea Hospitali ya Global
Hospital iliyopo Mtaa wa Vuga Mjini Unguja leo baada ya kuifungua rasmi.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed
Shein akifuatana na Daktari Mkuu na Mwenyekiti wa Kampuni ya Global
Hospital Dkt. K. Ravindranath (kulia), wakati alipotembelea
sehemu mbali mbali za kutoa huduma katika Hospitali ya Global
Hospital iliyopo Mtaa wa Vuga Mjini Unguja leo baada ya kuifungua rasmi.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed
Shein (wa pili kushoto) akipata maelezo kutoka kwa Mwakilishi wa Mwakilishi wa
Kampuni ya Global Hospital ya India Dkt. Nagesh Rao (kulia), wakati alipotembelea
katika vyumba vya upasuaji vyenye mashine za kisasa baada ya kuifungua Hospitali ya
Global Hospital iliyopo Mtaa wa Vuga Mjini Unguja leo (katikati) Mwenyekiti wa Kampuni ya Vigor Turky Salim
Hassan Turky.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed
Shein (wa pili kushoto), akipata maelezo kutoka kwa Daktari Mkuu na Mwenyekiti
wa Kampuni ya Global Hospital ya India Dkt. K. Ravindranath
(katikati) wakati alipotembelea chumba cha wagonjwa
mahututi (Theatre) baada ya kuifungua Hospitali ya Global Hospital
iliyopo Mtaa wa Vuga Mjini Unguja leo (kulia) Mkurugenzi wa Hospitali ya
Mnazi Mmoja Dk.Jamala A.Taibu.
Baadhi ya Madaktar na waalikwa katika sherehe ya ufunguzi wa Hospitali ya Global
Hospital iliyopo Mtaa wa Vuga Mjini Unguja wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na
Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein (hayupo pichani)
alipokuwa akitoa hutuba yake ya ufunguzi wa Hospitali hiyo leo.
Baadhi ya waalikwa mbali mbali katika sherehe ya ufunguzi wa Hospitali ya Global
Hospital iliyopo Mtaa wa Vuga Mjini Unguja wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na
Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein (hayupo pichani)
alipokuwa akitoa hutuba yake ya ufunguzi wa Hospitali hiyo leo.
Mwenyekiti wa Kampuni ya Vigor Turky Salim Hassan Turky akitoa
salamu zake mbele ya mgeni rasmi Rais wa Zanzibar na
Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein (hayupo pichani)
baada kuifungua Hospitali ya Global Hospital iliyopo Mtaa wa Vuga Mjini
Unguja leo.
Kaimu Waziri wa Fedha na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Ikulu na Utawala
Bora Dkt. Mwinyihaji Makame Mwadini akisema machache na kumkaribisha mgeni rasmi Rais wa Zanzibar na
Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani) kuzungumza na wananchi
baada ya kuifungua Hospitali ya Global Hospital iliyopo Mtaa
wa Vuga Mjini Unguja leo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed
Shein (kulia) alipokuwa akitoa hutuba yake wakati wa sherehe za ufunguzi wa Hospitali ya Global
Hospital iliyopo Mtaa wa Vuga Mjini Unguja leo inayomilikiwa na Kampuni ya
Vigor Turky ya hapa Zanzibar ambayo itatoa huduma za Maradhi mbali mbali.
Baadhi ya Viongozi wa Serikali na taasisi mbali mbali
na waalikwa wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na
Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani)
alipokuwa akitoa hutuba yake wakati wa sherehe za ufunguzi wa Hospitali
ya Global Hospital iliyopo Mtaa wa Vuga Mjini Unguja leo inayomilikiwa na
Kampuni ya Vigor Turky ya hapa Zanzibar ambayo itatoa huduma za Maradhi mbali
mbali.
Na Said Ameir, Zanzibar
28 Machi, 2015
RAIS
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein
amesisitiza kuwa Zanzibar kama zilivyo nchi nyingine inatambua sekta za
Afya na Elimu kuwa ndizo msingi wa maendeleo na ukuaji wa sekta nyingine
za kiuchumi na kijamii ndio maana wakati wote imekuwa ikichukuwa hatua
mbalimbali za kuziimarisha sekta hizo.
Dk.
Shein amesema hayo leo mara baada ya kuzindua rasmi hospitali mpya na
ya kisasa ya TASAKHTAA iliyopo Vuga mjini Unguja ambayo imejengwa kwa
ushirikiano kati ya kundi la makampuni ya Vigor Turkey Group ya Zanzibar
na Global hospitals ya India.
“Serikali
ya Mapinduzi ya Zanzibar inatambua umuhimu wa sekta hizi kwa ustawi wa
wananchi wa Zanzibar, ndio maana, tumeelekeza juhudi kubwa katika
kuziimarisha kwa kuzifanyia mabadiliko, kutunga sera na sheria madhubuti
na kuongeza bajeti ya mwaka kwa sekta hizi kila mwaka” Dk. Shein
alisema.
Aliwaeleza
viongozi na wageni waliohudhuria hafla hiyo kuwa amefurahishwa na
uwekezaji huo wa aina yake katika sekta ya afya na kueleza matumaini
yake kuwa hatua hiyo itazidi kuimarisha utoaji wa huduma bora za afya
nchini.
Dk.
Shein alisisitiza kuwa azma ya serikali ni kuwa na miradi mingi mikubwa
kama hiyo katika sekta zote na kwamba mswada mpya wa sheria
uliopitishwa hivi karibuni kuhusu uanzishaji na uendeshaji ushirikiano
baina ya Sekta ya Umma na Binafsi ni hatua muhimu katika kufikia azma
hiyo.
Alitoa
wito kuwepo ushirikiano wa karibu kati ya sekta binafsi na sekta ya
umma katika afya na kutolea mfano kuwa hospitali hiyo ya TASAKHTAA kuwa
na mashirikiano na hospitali kuu ya Mnazi mmoja.
“hospitali
yenu itahitaji msaada mkubwa kutoka hospitali ya Mnazi Mmoja na kinyume
chake hivyo mnahitaji kushirikiana”alieleza Dk. Shein na kuongeza kuwa
hospitali hizo hazitakuwa washindani.
Katika
hotuba yake hiyo alizidi kubainisha kuwa Serikali inaendelea
kukamilisha mpango wake wa kuifanya hospitali ya Mnazi Mmoja kuwa ya
rufaa ili iweze kutoa huduma nyingi zaidi na bora zaidi kwa wananchi.
Aliongeza
kuwa kuimarika kwa huduma za afya nchini kutasaidia kupunguza idadi
kubwa ya wagonjwa wanaopelekwa nchi za nje kupata matibabu mara kwa
mara.
Dk.
Shein ambaye kabla ya kuizindua hospitali hiyo alitembelea vitengo
mbalimbali vya hospitali hiyo, alieleza kuvutiwa na vifaa na utalaamu
uliopo lakini alisisitiza lugha na mahusiano mazuri kati ya watumishi wa
hospitali na wagonjwa.
“Hospitali
kama hii inatarajiwa kutoa huduma bora na nzuri, kufanya tafiti, na
kuchunguza maradhi pamoja na kuwapa faraja wagonjwa kwa kuwahudumia kwa
lugha nzuri” Dk. Shein alieleza.
Akizungumza
katika hafla hiyo Waziri wa Afya Rashid Seif Suleiman alisema Wizara
imeupokea mradi huo kwa mikono miwili na kuutaka uongozi wa hospitali
kuzingatia sheria na kanuni za uendeshaji wa hospitali zikiwemo za
usajili wa watumishi wake katika bodi husika za kitalaamu pamoja na zile
zinazohusu madawa.
Naye
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Ikulu na Utawala Bora Dk. Mwinyihaji
Makame Mwadini kwa niaba ya Waziri wa Fedha alisema sekta ya afya imo
katika mpango kabambe wa serikali wa kutoa vivutio maalum vya uwekezaji
ili kuvutia wawekezaji zaidi.
Alibainisha
kuwa hadi sasa sekta hiyo iko nyuma katika kuvutia wawekezaji tofauti
na sekta nyingine kama ya utalii ambapo nchi inahitaji sana huduma
katika sekta ya afya hivyo Serikali itaweka jitihada za
makusudi kuondoa hali hiyo.
“Inawezekana
hatujaitangaza sana lakini pia yawezekana ni kutokana na ukosefu wa
wataalamu na gharama kubwa za uwekezaji”alisema Dk. Mwinyi na kuongeza
kuwa mradi wa TASAKHTAA umeonesha mfano katika uwekezaji katika sekta
hiyo.
Kwa
upande wake, Mwenyekiti wa kundi la makampuni ya Vigor Turkey Bwana
Salim Turky aliwahakikishia viongozi na wageni waliohudhuria hafla hiyo
kuwa uongozi wa hospitali hiyo umedhamiria kutoa huduma bora na na kwa
gharama nafuu kwa wananchi wote.
“tutahakikisha
wananchi wote wanapata huduma za matibabu na tayari baadhi ya
wafanyabiashara wameahidi kusaidia gharama za wananchi ambao hawatakuwa
na uwezo kabisa ili wasikose huduma”alibainisha Bwana Turky.
Alisema
nia ya hospitali hiyo ni kushirikiana na watoa huduma wengine katika
sekta hiyo zikiwemo hospitali za umma hivyo wakati wote.
Alizishukuru
mamlaka mbalimbali za serikali kwa ushirikiano wao ambao hatimae
hospitali hiyo imeweza kukamilika na kuzinduliwa tayari kuanza kutoka
huduma kwa wananchi.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269