Balozi wa Marekani nchini Tanzania
Mark Childress akisisitiza jambo wakati wa ufungaji wa mafunzo ya
uongozi bora kwa vijana yaliyoanzishwa na Rais wa Marekani, Barrack
Obama kuptia taasisi ya Mandela Felloship, Ohio University na Institute
for International Journalism.
Mkurugenzi wa mafunzo ya Yali Connect Camp, Dk Yusuf Kalyango akizungumza na wahitimu 18 wa mafunzo hayo.
Mbunge wa Jimbo la Arumeru Mashariki kupitia chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Mh Joshua Nassari akipozi katika picha na Balozi wa Marekani nchini Tanzania, Mark Childress mara baada ya kukabidhiwa cheti cha uhitimu.
Vijana kutoka mataifa manne
wakimsikiliza Balozi wa Marekani nchini Tanzania (hayupo pichani) wakati
wa hafla ya kufunga mafunzo ya uongozi bora kwa viongozi vijana wa
baadaye yaiyomalizika hivi karibuni jijini.
………………………………………………………………………………..
Na Mwandishi wetu
Jumla ya vijana 18 kutoka nchi za
Kenya, Uganda, Mauritius, Seychelles na Tanzania wemehitimu mafunzo ya
wiki mbili ya uongozi bora yaliyoanzishwa na Rais wa Marekani, Barrack
Obama.
Mafunzo hayo yaliendeshwa nchini
chini ya programu ya Connect Camp chini ya Mandela Washington
Fellowship, Chuo Kikuu cha Ohio na Taasisi ya Kimataifa ya Uandishi wa
Habari (Institute for International Journalism) yenye malengo ya kuwapa
uwezo vijana wa kuwa viongozi bora wa baadaye.
Akizungumza wakati wa ufungaji wa
mafunzo hayo, Balozi wa Marekani nchini Tanzania Mark Childress
aliwataka vijana hao kutumia mafunzo hayo kwa mafanufaa katika fani zao
na nchi husika kwani ni nyenzo ya kuwa viongozi bora wa baadaye hapa
duniani.
Childress alisema kuwa Rais Obama
ameanzisha mafunzo hayo kutokana na kutambua umuhimu wa uongozi bora na
kuamini kuwa vijana ndiyo taifa la kesho.
“Nimefurahishwa na mwamko wa
mafunzo haya, nawaomba myatumie kwa ajili ya maendeleo yenu na kwa nchi
husika, hii ni nyenzo pekee katika kufikia lengo mlilojiwekea,” alisema
Childress.
Mafunzo hayo yanayojuliana kwa
jina la ‘Young African Leadership Initiative (Yali) yalishirikisha
vijana nane (8) wa Kitanzania, wanne Uganda, huku Kenya, Mauritius na
Seychelles zikiwakilishwa na watu wawili wawili.
Mmoja wa wahitimu wa mafunzo hayo
ni Mbunge wa Chadema jimbo la Arumeru Mashariki, Joshua Nasari ambaye
alisema atatumia mafunzo hayo kujihimarisha kisiasa na kushinda kiti ha
ubunge katika jimbo hilo.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269