Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya
Mawasiliano,Sayansi na Teknolojia John Mngodo akiwasalimia wajumbe wa
warsha ya kupitia marejeo ya mfumo wa Taifa wa sayansi,teknolojia na
ubunifu ulioandaliwa na Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia,
kushoto ni Mkurugenzi wa Sayansi na Teknolojia Prof. Evelyn Mbede .
Mkurugenzi wa Sayansi na
Teknolojia Prof. Evelyn Mbede, akiwasalimia wajumbe wa warsha ya kupitia
marejeo ya mfumo wa Taifa wa sayansi,teknolojia na ubunifu ulioandaliwa
na Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, kulia kwake ni Katibu
Mkuu wa Wizara ya Mawasiliano,Sayansi na Teknolojia Prof. Patrick
Makungu, Katika ni Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue na wa mwisho
kulia ni Naibu katibu Mkuu waWizara ya Mawasiliano, Sayansi na
Teknolojia John Mngodo .
Katibu Mkuu wa Wizara ya
Mawasiliano,Sayansi na Teknolojia Prof. Patrick Makungu, akisema hotuba
ya kumakribisha mgeni rasmi Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni
Sefue(Hayupo pichani) wakati wa ufunguzi wa warsha ya ubunifu wa sera ya
Taifa katika Sayansi na Teknolojia iliandaliwa na Wizara ya
Mawasilano,Sayansi na Teknolojia jijini Dar es Salaam.
Mgeni rasmi Katibu Mkuu Kiongozi
Balozi Ombeni Sefue akiongea na wajumbe wa warsha wakati wa ufunguzi wa
warsha hiyo ya ubunifu wa sera ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia
iliyoandaliwa na Wizara ya Mawasilano,Sayansi na Teknolojia jijini Dar
es Salaam.
Mgeni rasmi katika ufunguzi wa
warsha ya ubunifu wa sera ya Taifa katika Sayansi na Teknolojia Katibu
Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue(katika) akiwa na Katibu Mkuu wa Wizara
ya Mawasiliano,Sayansi na Teknolojia Prof. Patrick Makungu(kushoto), na
Naibu Katibu Mkuu wa Hiyo John Mngodo,warsha hito iliandaliwa
iliandaliwa na Wizara ya Mawasilano,Sayansi na Teknolojia jijini Dar es
Salaam.
Wadau mbalimbali ambao ni wajumbe
wa mkutano wa ubunifu wa sera ya taifa ya Sayansi na teknolojia
ilifanyika katika hoteli ya Kunduchi jijini Dar es Salaam iliyoandaliwa
na Wizara ya Mawasiliano,Sayansi na Teknolojia.
(Picha na Lorietha Laurence- Maelezo)
Na May-Zuhura Simba
Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue amesema kuwa ili jamii
iweze kukua kwa kasi na kupata maendeleo haina budi kuwekeza katika
sayansi na teknolojia.
Aliongea hayo jana jijini Dar es Salaam wakati wa ufunguzi wa
warsha ya kupitia marejeo ya mfumo wa Taifa wa sayansi,teknolojia na
ubunifu ulioandaliwa na Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia.
“ubunifu katika sayansi na teknolojia ni kitu muhimu katika
kupata uvumbuzi wa vitu mbalimbali muhimu vinavyoleta maendelao kwa
jamii husika hivyo kuna umuhimu wa kuwafungia wanasayansi katika atamizi
ili kupata matokeo mazuri ya utafiti” alisema Balozi Sefue
Aidha aliongeza kuwa nchi kama Korea na Singapore waliwekeza
katika sayansi,technologia na ubunifu na hivyo kujikwamua kiuchumi na
kuleta maendeleo kwa jamii zao
Vilevile alisisitiza kuwa ubunifu ukisimamiwa dhabiti utasaidia
katika kuleta mageuzi kwenye sekta muhimu ikiwemo elimu,
afya,biashara,kilimo na miundombinu na hivyo kutatua matatizo ya
kijamii.
“Mfano mzuri ni Max malipo ambalo ni zao la vijana wa kitanzania
waliokuwa wamewekwa katika atamizi na kuleta uvumbuzi huu kwa kutumia
sayansi na teknolojia ” alisema Balozi Sefue.
Aidha aliwataka wadau mbalimbali wa maendeleo,makampuni binafsi,
na serikali kushirikiana kwa pamoja kufungua vituo atamizi
zitakavyosaidia vijana kuvumbua teknolojia mbalimbali.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269