Waziri wa
Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi akiwasili katika
uwanja wa ndege wa Mjini Sumbawanga leo tarehe 25/03/2013 kwa ajili ya
ziara ya siku mbili Mkoani Rukwa moja ikiwa kufuatilia migogoro sugu ya
ardhi ukiwemo wa shamba la Skaungu ambapo ameonana na
wananchi na viongozi wa vijiji kumi vinavyolizunguka shamba hilo ambalo
lina mgogoro wa muda mrefu kati ya Mmiliki Ephata Ministry na wananchi
hao. Lengo la pili la ziara yake ni kuweka jiwe la msingi katika nyumba
za makazi zinazojengwa na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) katikati ya
Mji wa Sumbawanga.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mhe. Eng. Stella Manyanya (kulia) akimtambulisha Waziri wa Ardhi Mhe. William Lukuvi kwa viongozi wa Serikali na Chama Mkoa wa Rukwa muda mfupi baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Sumbawanga.
Katika
msafara wake Mhe. Waziri aliongozana na Mbunge wa Jimbo la Sumbawanga
Mjini Mhe. Aeshi Hillal (Pichani na Mdau Juddy Ngonyani wa Channel Ten),
Mbunge wa Jimbo la Kwela Mhe. Ignas Malocha na Mkuu wa Mkoa wa Rukwa
Mhe. Eng. Stella Manyanya.
Waziri
wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi akizungumza
na viongozi wa Vijiji kumi vya kata za Mollo na Msandamuungano
vinavyozunguka sahamba la Skaungu lenye Mgogoro wa muda mrefu kati ya
muwekezaji Ephata Ministry na wananchi wa vijiji hivyo. Mhe. Waziri
amesema lengo la kufika kwake Mkoani Rukwa ni kuona maeneo ya mgogoro
huo pamoja na kuwasikiliza wananchi na baadae kuonana na muwekezaji huyo
kabla ya Serikali kufanya uamuzi wa hatma ya shamba hilo ambalo
linadaiwa na wananchi kumega maeneo ya vijiji na hivyo kukosa maeneo ya
kulima kutokana na ongezeko la watu. Alieleza kuwa taarifa zote kuhusu
shamba hilo zimeshaifikia ofisi yake na kilichobaki ni kutoa uamuzi wa
Serikali wa kumaliza Mgogogoro huo.
Waziri wa
Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi alipofika katika
Kijiji cha Skaungu kuongea na wananchi alipokelewa na mabango yenye
ujumbe mbalimbali unaolenga kuiomba Serikali kusaidia upatikanaji wa
ardhi yao ambayo ipo ndani ya shamba la Muwekezaji Ephata Ministry. Mhe.
Lukuvi amewatoa hofu wananchi hao kuwa mgogoro huo utapata ufumbuzi
kabla ya Serikali ya awamu ya nne haijamaliza muda wake.
Ujumbe mwingine uliokuwa kwenye mabango hayo.
Ujumbe
mwingine ukinyesha kuwa toka Kijiji hicho kianzishwe mwaka 2008 na
kupewa hati wananchi hao wamekuwa hawana haki na sehemu ya ardhi yao
ambayo ipo ndani ya shamba la Muwekezaji huyo.
Mkuu wa
Mkoa wa Rukwa Eng. Stella Manyanya akizungumza na wananchi wa Kijiji cha
Skaungu muda mfupi kabla ya kumkaribisha Waziri wa Ardhi Mhe. William
Lukuvi kuzungumzia lengo la ziara yake katika Kijiji hicho, alisema ni
muda sasa kumaliza mgogoro huo.
Waziri
wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi (kulia)
akizungumza na Wananchi wa Kijiji cha Skaungu leo tarehe 25/03/2015.
Alisema kuwa mgogoro huo unawanyima usingizi viongozi wa Serikali na
imefika wakati sasa kuumaliza. Aliongeza kuwa iwapo Serikali itaamua
sehemu ya shamba hilo irudi kwa wananchi basi halitagawiwa kiholela na
badala yake utatumika utaratibu maalum kwa kushirikisha Halmashauri na
Serikali ya Kijiji kwa kuanza kuwatambua wale wenye hitajio kubwa la
ardhi na baadae kuwaangalia wananchi wengine wenye haki ya kupatiwa
maeneo hayo.
Wadau wa
Habari Mkoa wa Rukwa wakitoka kuchukua matukio katika Kijiji cha
Skaungu, Kutoka kulia ni Juddy Ngonyani (Channel Ten), Nswima Errrrrnest
(TBC), Joshua Joel (ITV), Peti Siame (Habari Leo/Daily News), Gurian
Adolph Ndingala FM na Mussa Mwangoka (Mwananchi).
Bi. Anna Msafiri Mwananchi wa Kijiji cha Mawenzusi akitoa kero yake kwa Mhe. Waziri wa Ardhi.
Sehemu ya wananchi wa kijiji cha Mawenzusi ambao pia walipata fursa ya kupaza sauti zao kwa Waziri wa Ardhi Mhe. William Lukuvi.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269