Rubani Andreas Lubitz
Rubani wa ndege ya kampuni ya
Germanywings ilioanguka katika milima ya Alps nchini Ufaransa siku ya
jumanne alitaka kuiharibu ndege hiyo kulingana na maafisa wa
Ufaransa.Kiongozi wa mashtaka katika mji wa Mersaille ,Brice Robin,
akizungumza kulingana na habari aliyopata katika kijisanduku cha kunasa
sauti katika ndege amesema kuwa rubani huyo alikuwa ndani ya chumba cha
kuendesha ndege pekee.
Rubani huyo kimakusudi aliishusha ndege hiyo kwa kasi huku rubani mwenza akiwa nje ya chumba hicho cha kuendesha ndege.BBC
Bwana Robin amesema kuwa kulikuwa na kimya kikubwa ndani ya chumba hicho wakati rubani mwenza alipojaribu kuingia kwa nguvu.
Hatahivyo abiria walisikika wakipiga nduru kabla ya kuanguka kwa ndege hiyo,aliongezea.
Mlima wa Alps ambapo ndege ya abiria ya Germanywings ilianguka
Rubani huyo kwa jina Andreas
Lubtiz,mwenye umri wa miaka 28, alikuwa hai hadi wakati ndege hiyo
ilipoanguka ,kiongozi wa mashtaka alisema.
Ndege hiyo aina ya Airbus 320 iliokuwa
ikitoka Barcelona kuelekea Duesseldorf Ujerumani iligonga mlima na
kuwauwa abiria wote 144 pamoja na wafanyikazi sita wa ndege baada ya
kushuka kwa dakika nane.
"Tunasikia rubani akimuuliza rubani
mwenza kuchukua udhibiti wa usukani wa ndege hiyo na vilevile tunasikia
sauti ya kiti kikisonga nyuma na mlio wa mlango ukifungwa,bwana Robin
aliwaeleza wanahabari.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269