…………………………………………
Chama cha Demokrasia na Maendeleo Kanda ya Kaskazini
kimezindua rasmi mpango wa kuchangia chama hicho kupitia simu za mkononi
ili kukiwezesha chama hicho kushinda katika Uchaguzi mkuu wa taifa
utakaofanyika Octoba mwaka huu.
Akizungumza na Waandishi wa Habari katika Ofisi za mkoa za
chama hicho ,Katibu wa Chadema kanda ya Kaskazini Amani Golugwa amesema
kuwa michango itakayokusanywa na wanachama na wapenzi wa chama hicho
itawawezesha kufanya kampeni nchi nzima na kuikomboa nchi hii kwa
kupata viongozi bora.
Golugwa alisema kuwa kutokana na watanzania wengi kuchoshwa
na uongozi mbovu wa CCM wanahitaji kukichangia chama hicho ambacho
ndicho tumaini la pekee kwa Watanzania la kuleta mabadiliko ya kweli.
“Hatutaki tushindwe kufanya kampeni kwasababu hatuna fedha
hivyo tunawaomba wanachama na mashabiki wa chama hicho kukichangia chama
hicho kupitia simu zao za mikononi kwa kupitia namba maalumu
tutakayowapatia” Golugwa
Alisema kuwa mpango huo umeanza rasmi na unakubalika kwa
mujibu wa sheria za usajili wa vyama vya siasa kuwa chama kitapata
mapato yake kupitia michango mbali mbali kwa wanachama.
Katibu huyo wa Kanda ya Kaskazini Amani Golugwa amewataka
polisi na vyombo vya usalama pamoja na tume ya uchaguzi kuhakikisha
kuwa wanafanya kazi kwa misingi ya haki na ukweli hasa katika kipindi
ambacho nchi inaelekea kwenye uchaguzi ili kuepuka kuhatarisha amani.
“Tusifanye masihara na amani ,tunahitaji tume huru na yenye
uadilifu itakayofanya kazi yake vizuri bila kuegemea upande wowote”
Alisema Golugwa
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269