Na
Wananchi wa Mtaa wa Mamboleo B,kata ya Temeke wameiomba Serikali kuingilia kati suala la jirani yao anayedaiwa kutumia cheo cha ndugu yake anayedaiwa kufanya kazi ngazi za juu Serikalini kuwanyanyasa jirani zake.
Wakizungumza
na Jambo leo Dar es Saalam jana,kwa niaba ya wenzao mmoja wa mkazi wa
hapo Kristna Julius alisema anatumia wadhifa wa ndugu yake huyo ili
kuwanyanyasa majirani zake.
Kristina alisema alikuwa anadai majirani zake wamezika mtoto mwenye umri wa mwaka(1) pembezoni mwa nyumba yake wakati si kweli.
Mkazi
huyo aliendelea kuwa ilikuwa kama mida ya saa saba mchana ndipo
alipowaona maaskari wanakuja kwenye eneo lao na yule Mzee akawaonyesha
sehemu aliyodai kwamba kuna mtoto amezikwa pembezoni mwa nyumba yake.
"Walipofika waliomba majembe na kuanza kuchimbua lakini hawakukuta kitu na walipomaliza waliacha hivyohivyo wazi na kuondoka",alisema Kristina.
"Walipofika waliomba majembe na kuanza kuchimbua lakini hawakukuta kitu na walipomaliza waliacha hivyohivyo wazi na kuondoka",alisema Kristina.
Mkazi
mwingine wa mtaa huo Mohamed Bakari alisema aliona askari wanakuja na
kufukua katika shimo,kwakuwa na aliwapigia simu askari hao kuwa kuna
mtoto amefukiwa.
"Huyu
Mzee baada ya askari kumaliza kuchimbua hilo shimo akauchukua mchanga
na kusema anaupeleka kwa mkemia mkuu ili ukapimwe kama hauna
kitu"alisema Mayao.
Naye,Mwenyekiti
wa Serikali ya mtaa huo Zuberi Kabumaye alisema suala la mzee huyo
kuwasumbua majirani zake nila muda mrefu,na kwamba alishawahi kusumbua
huko nyuma na wakamfungulia kesi.
Mwenyekiti
aliendelea katika kesi hiyo iliyofunguliwa na mmoja wa majirani
aitwaye Anderson Mhogole(marehemu) na ilikuwa kwenye vyombo vya sheria
jambo lililomfanya mpaka akahama baada ya jirani huyo kuisimamia kidete
lakini aliposikia tu amefariki alirudi tena.
"Mwaka juzi ndipo aliporudi upya na kuanza kutishia watu maisha bila sababu ya msingi",alisema Kabumaye.
Alisema
katika tukio mojawapo Mzee huyo alimng'ata jirani yake kwa meno,na
kumfanya aende kushitaki polisi huku akiwa na vielelezo vyote kutoka kwa
daktari lakini mtuhumiwa hajakamatwa na kesi haifuatiliwi.
Hata
hivyo alisema katika tukio la kufukiwa mtoto alipata taarifa kuwa kuna
askari wamekuja kufukua shimo la mtoto aliyezikwa hapo kitendo
kilichomfanya Afisa Mtendaji wake aitwaye Regina Gaihwa kuwasili eneo
la tukio na kukuta si kweli.
"Askari wakiongozwa na Afande
Godluck Lema walichimbua hilo shimo bila kuwasiliana na Serikali ya
mtaa jambo ambalo si sahihi",alisema.
Mwenyekiti
huyo alisema baada ya tukio hilo mzee huyo aliwageuzia jirani zake
kibao kwa kutoa ripoti polisi na kuwafungulia mashtaka na kufanya
majirani zake wapatao kumi wakamatwe na polisi.
Haidha
Mwenyekiti huyo alisema alihangaika kuwatoa wananchi hao polisi lakini
ilishindikana kutokana na nguvu ya ndugu anayedaiwa wa mzee huyo.
Mwenyekiti
huyo alisema alifanikiwa kuwawekea dhamana watu hao kumi kwa kutumia
kadi yake ya benki ndipo wakatolewa huku kesi ikitegemewa kusikilizwa
tena katika mahakama ya kisutu tarehe 30 mwezi huu.
Wakati
huo huo, Mzee huyo aitwaye Joseph Lyapinda Mzee anayedaiwa kuwanyanyasa
jirani zake alisema majirani zake hawawezi kumfanya chochote kwani ana
ndugu yake aliyeko ngazi za juu Serikalini.
"Hakuna anayeweza kunifanya chochote kwani nina watu Serikalini",alisema Mzee huyo.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269