NA MARYAM KIDIKO/MWANAISHA MOH’D Viongozi mbali mbali pamoja na Wananchi wamehuzuria katika Dua maalum yakumuombea muasisi wa Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar marehemu Mzee Abeid Amani Karume huko Afisi Kuu ya CCM Kisiwandui Mjini Zanzibar.Dua hiyo ilijumuisha viongozi wa Dini tofauti kwa lengo la kumkumbuka jemedari mkuu wa Zanzibar aliyefanya mengi mazuri yaliyopelekea Nchi kuwa katika hali ya Amani na utulivu.Hata hivyo maendeleo mbali mbali yanaonekanwa ikiwemo Elimu, maji, makaazi ambayo hupelekea jamii kuyakumbuka.Nae kwa upande wake aliyekua Mke wa muasisi wa Mapinduzi Bi. Fatma Karume amewaomba Wananchi wa Zanzibar kuendeleza Amani, Upendo na Mshikamano uliopo Nchini.Bi. Fatma amesema ni vyema viongozi walioko madarakani kuiga mfano wa kiongozi wa awamu ya kwanza ambaye alikua anakemea suala zima la ubaguzi ili wananchi waweze kuwa kitu kimoja. Kwa upande wake Waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa Kimataifa Mhe. Bernard K. Membe amesema kiongozi huyo alikuwa ni mtu mwenye kujali na kutetea wananchi wake.Membe amesema kiongozi huyo ni wapekee kwa wema aliyoutenda kwa kuunganisha Tanzania na Zanzibar kuwa kitu kimoja kilichopelekea kuwepo udugu. Ni miaka Arubaini na tatu (43) tangu kifo chake kutokea hivyo kila ifikapo tarehe 7 mwezi wa 4 kila mwaka hukumbukwa na Wananchi kwa kumsomea Dua.
HITMA YA MAREHEMU MZEE KARUME.
Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed
Shein akisalimiana na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Vuai Ali Vuai maara
alipowasili katika viwanja vya Ofisi Kuu ya CCM Kisiwandui Mjini Unguja
kubhudhuria katika Hitma ya Rais wa Kwanza wa Zanzibar Marehemu Mzee
Abeid Amani Karume Iliyofanyika leo asubuhi.[Picha na Ikulu.] Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed
Shein(katikati) akiwaongoza Viongozi mbali mbali pamoja na Wananchi
katika Kisomo cha hitma ya aliyekuwa Rais wa Kwanza wa Zanzibar Marehemu Mzee Abeid Amani Karume katika ukumbi wa Ofisi Kuu ya CCM Kisiwandui Mjini Unguja Iliyofanyika leo asubuhi.[Picha na Ikulu.] Baadhi ya Viongozo wakisoma hitma akiwemo aliyekuwa Rais wa Kwanza wa Zanzibar Marehemu Mzee Abeid Amani Karume(kushoto) Balozi Ali Karume katika ukumbi
wa Ofisi Kuu ya CCM Kisiwandui Mjini Unguja Iliyofanyika leo asubuhi.[Picha na Ikulu.] Waislamu na wananchi mbali mbali wakiwa katika kisomo cha hitma ya aliyekuwa Rais wa Kwanza wa Zanzibar Marehemu Mzee Abeid Amani Karume katika ukumbi wa Ofisi Kuu ya CCM Kisiwandui Mjini Unguja Iliyofanyika leo asubuhi.[Picha na Ikulu.] Akinamama wa Mitaa mbali mbali ya Mji wa Unguja wakiwa katika kisomo cha Hitma ya aliyekuwa Rais wa Kwanza wa Zanzibar Marehemu Mzee Abeid Amani Karume katika ukumbi wa Ofisi Kuu ya CCM Kisiwandui Mjini Unguja Iliyofanyika leo asubuhi.[Picha na Ikulu.] Mke wa Rais Zanzibar Mama Mwanamwema Shein(katikati) akiwa na Mama Shadya Karume Mke wa Rais Mstaafu wa Zanzibar(wa tatu kulia) Mama Fatma Karume (wa pili kulia) Mke wa Makamo wa Rais wa Jamhuri ya Muungano Mama Zakia Bilali (kushoto) Bi Khadija Aboud (wa pili kushoto)Mjumbe wa Kamati Kuu wa CCM,katika hitma ya kumuombea dua Rais wa kwanza wa Zanzibar Marehemu Mzee Abeid Amani Karume,iliyosomwa leo katika ukumbi wa Ofisi ya CCM Kisiwandui Mjini Unguja,[Picha na Ikulu.] Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein akiweka shada la mauwa katika kaburi la Marehemu Rais wa kwanza wa Zanzibar Mzee Abeid Amani Karume,baada ya kisomo cha hitma na dua iliyoombwa na wananchi wa Zanzibar katika Ofisi ya CCM Kisiwandui Mjini Zanzibar leo asubuhi,[Picha na Ikulu.] Makamo wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilali
akiweka shada la mauwa katika kaburi la Marehemu Rais wa kwanza wa Zanzibar Mzee Abeid Amani Karume,baada ya kisomo cha hitma na dua iliyoombwa na wananchi wa Zanzibar katika Ofisi ya CCM Kisiwandui Mjini Zanzibar leo asubuhi,[Picha na Ikulu.] Muasisi wa Mapinduzi ya Zanzibar Mzee Hamid Ameir akiweka shada la mauwa katika kaburi la Marehemu Rais wa kwanza wa Zanzibar Mzee Abeid Amani Karume,baada ya kisomo cha hitma na dua iliyoombwa na wananchi wa Zanzibar katika Ofisi ya CCM Kisiwandui Mjini Zanzibar leo asubuhi,[Picha na Ikulu.] Balozi Ali Karume (Mtototo) kwa niaba ya familia akiweka shada la mauwa katika kaburi la Marehemu Rais wa kwanza wa Zanzibar Mzee Abeid Amani Karume,baada ya kisomo cha hitma na dua iliyoombwa na wananchi wa Zanzibar katika Ofisi ya CCM Kisiwandui Mjini Zanzibar leo asubuhi,[Picha na Ikulu.]

Wake
wa Viongozi wakiitikia dua iliyoombwa katika kaburi la Marehemu
MzeeAbeid Amani Karume baada ya hitma iliyosomwa leo katika ukumbi wa
Ofisi ya CCM Kisiwandui Mjini Unguja na kuhudhuriwa na waislamu mbali
mbali Mjni na Vijijini,[Picha na Ikulu.] Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed
Shein pamoja na Viongizi wengine wakiitikia Dua iliyoombwa na Mufti Mkuu
wa zanzibar Sheikh Saleh Omar Kabi (kulia) baada ya kisomo cha hitma
iliyosomwa leo katika ukumbi wa Ofisi ya CCM Kisiwandui Mjini Unguja.[Picha na Ikulu.] Baba
Askofu wa Anglikan wa Kanisa la Mkunazini Michael Hafidh akiomba dua
wakati Viongozi mbali mbali waliofika katika kaburi la aliyekua Rais wa
Kwanza wa Zanzibar Marehemu Mzee Abeid Amani Karume,baada ya kisomo cha hitma iliyosomwa leo katika ukumbi wa Ofisi ya CCM Kisiwandui Mjini
Na Rajab Mkasaba, Ikulu Zanzibar
Na Rajab Mkasaba, Ikulu Zanzibar
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi
Alhaj Dk. Ali Mohamed Shein leo ameongoza hitma ya kumuombea dua Rais wa Kwanza
wa Zanzibar Marehemu mzee Abeid Amani Karume, iliyofanyika Afisi Kuu ya CCM
Kisiwandui mjini Zanzibar.
Hitma hiyo, ilihudhuriwa na viongozi mbali mbali akiwemo Makamu wa Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Mohammed Kharib Bilal, Rais mstaafu wa Serikali
ya Mapinduzi ya Zanzibar Awamu ya Sita, Mhe. Amani Abeid Karume, Makamo wa
Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad na Makamu wa Pili wa Rais
wa Zanzibar Balozi Seif Ali Idd.
Viongozi wengine walihudhuria katika hitma hiyo ni Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Saleh Omar
Kabhi, Kadhi Mkuu wa Zanzibar Sheikh Khamis Haji, Sheikh wa Mkoa wa Dar-es-
Salam Sheikh Mussa Salum na viongozi wengineo.
Wengine ni viongozi wa serikali zote mbili na viongozi wastaafu, viongozi
wa vyama vya siasa, Masheikh kutoka Zanzibar na Tanzania Bara, Wabunge na
Wawakilishi, wananchi kutoka sehemu mbali mbali pamoja na Mabalozi wadogo
waliopo hapa Zanzibar.
Hitma hiyo ya kumuombea dua Marehemu Mzee Abeid Amani Karume pia ni
miongoni mwa maadhimisho ya Siku ya Mashujaa ilitanguliwa na Qur-an tukufu,
iliyosomwa na Ustadh Sharif Muhidin na kuongozwa na Sheikh Jafar kutoka Masjid
Noor Mohammad,iliopo Kwa Mchina Mwanzo.
Mara baada ya hitma hiyo, Sheikh Mkoa wa Dar-es-Salaam, Sheikh Mussa Salum
alitoa mawaidha na kumuelezea marehemu mzee Abeid Amani Karume kuwa ni kiongozi
aliyepigania maendeleo ya wananchi wa Zanzibar na kumuombea MwenyeziMungu ampe
makaazi mema Peponi.
Akieleza kuhuhu umuhimu wa siku hii, Sheikh Mussa alisema kuwa siku ya leo
ni muhimu sana kwa Zanzibar na Tanzania kwa ujumla kwa lengo la kumuombea dua
Marehemu Karume pamoja na mashujaa wengine.
Aidha, Sheikh Mussa alitumia fursa hiyo kukumbusha juu ya umauti na
kusisitiza kuwa ni jambo ambalo litafika
kwa kila kiumbe alichokiumba MwenyeziMungu na kusisitiza kuwa ni vizuri
mwanaadamu akakumbuka asili yake na hatma yake.
“Kifo ni onyo, kifo ni mawaidha na kifo ni mazingatio...kutokana na hali
hiyo kuna kila sababu ya kutenda mema, kuwa na mahaba, kuwa na udugu wa kiimani..
huku tukiendelea kumuombea dua mzee wetu huyu kwani yeye ameonja umauti kama
ilivyoeleza Qur-an ikiwa na maana kuwa roho yake bado iko hai” alisema Sheikh
Mussa.
Pamoja na hayo, Sheikh Mussa katika kutilia mkazo suala zima la udugu wa
kiimani alitoa pongezi kwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein kwa kuendelea kusimamia Serikali ya
Mapindui ya Zanzibar yenye muundo wa Umoja wa Kitaifa ambayo imewafanya
Wazanzibari kuimarisha udugu wao na kuwa kitu kimoja kama Uislamu unavyotaka.
Alisema kuwa hatua hiyo imezidisha umoja sambamba na kuimarisha amani na
utulivu uliopo na kuifanya Zanzibar kuwa tulivu na kusisitiza kuwa huo ndio
udugu wa kiimani.
Baada ya kisomo hicho cha hitma ambacho hufanyika kila mwaka inapofika
tarehe 7, Aprili, viongozi hao na wananchi waliohudhuria katika hitma hiyo
walimuombea dua, marehemu mzee Abeid Karume katika kaburi lake lililopo
pembezoni mwa afisi hiyo ya CCM Kisiwandui dua iliyoongozwa na viongozi wa dini
tofauti akiwemo Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Omar Kabhi, Askofu Michael Hafidh
kutoka Kanisa la Anglikana Zanzibar na Bhaguan Suria (Mshamba) aliyesoma kwa
niaba ya Wahindu.
Viongozi na wanafamilia waliweka mashada ya maua katika kaburi la marehemu
mzee Abeid Amani Karume akiwemo Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi Alhaj Dk. Ali Mohamed Shein, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mhe. Dk. Mohammed Kharib Bilal, Mzee Hamid Ameir aliyeweka shada la
maua akiwakilisha wazee walioshiriki Mapinduzi ya Januari 12, 1964.
Mwakilishi wa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi ya Wananchi wa Tanzania Luteni
Jeneral S.A. Ndomba, Balozi Ali Karume aliyewakilisha familia ya Marehemu Sheikh
Abeid Amani Karume na Balozi mdogo wa China anayefanya kazi zake hapa Zanzibar Mhe.
Xie Yualing aliyewawakilisha Mabalozi wenzake wa hapa nchini.
Aidha, Mama Mwanamwema Shein aliungana na akina mama wengine katika hitma
hiyo katika Afisi hiyo ya CCM Kisiwandui, akiwemo mjane wa marehemu mzee Abeid Karume,
Mama Fatma Karume, Mama Asha Bilali,Mama Zakia Bilal, Mama Asha Balozi na Mama
Pili Balozi, Mama Shadya Karume na viongozi wengine wanawake wa kitaifa
wakiwemo Mawaziri, Wabunge, Wawakilishini na wananchi kutoka sehemu mbali mbali
ya Zanzibar na Tanzania Bara.
April 7, 1972 ndiyo siku aliyouawa Rais wa Kwanza wa Zanzibar marehemu Mzee
Abeid Amani Karume na wapinga maendeleo nchini ambapo hivi leo imetimia miaka
43 tokea utokee msiba huo.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269