Breaking News

Your Ad Spot

Apr 7, 2015

MICHUANO YA CHAN MAKUNDI YA PANGWA



Timu ya Uganda The Cranes
Tanzania itachuana na Uganda wakati Kenya itakipiga na Ethiopia katika michuano ya kufuzu ya Afrika kwa wachezaji wa ndani (CHAN) kufuatia ratiba ya michuano hiyo iliyotolewa na Shirikisho la mpira wa miguu barani Afrika, (CAF),
Mechi hiyo ya awali itachezwa kati ya Juni 19-21 wakati ile ya marudiano itachezwa kati ya July 3-5 mwaka huu.
Fainali za CHAN zitafanyika nchini Rwanda kuanzia January 16 mpaka February 7, 2016.
Michuano hiyo, kwa mujibu wa ratiba ya CAF, itashirikisha timu 42, ambazo zitashindana katika kanda 6 na fainali zake zitachezwa na nchi 16 tu wakiwemo timu mwenyeji.
Uganda kwa sasa ipo nafasi katika nafasi ya 84 ya viwango vya FIFA, wakati Tanzania ipo nafasi ya 100.
Ratiba ya kufuzu ya CHAN ni kama ifuatavyo
Kanda ya Magharibi A.
Guinea Bissau vs Mali
Mauritania vs Sierra Leone
Guinea vs Liberia
Senegal vs Gambia
Kanda ya Magharibi B
Ghana vs Ivory Coast
Nigeria vs Burkina Faso
Niger vs Togo
Kanda ya kati
DR Congo vs Jamhri ya Kati (CAR)
Cameroon vs Congo
Chad vs Gabon
Kanda ya Kati Mashariki
Hatua ya awali
Tanzania vs Uganda
Djibouti vs Burundi
Ethiopia vs Kenya
Kanda ya Kusini
Zimbabwe vs Visiwa vya Comoro
Lesotho vs Botswana
Namibia vs Zambia
Msumbiji vs Seychelles
Afrika ya Kusini vs Mauritius
Swaziland vs Angola
Kanda ya Kaskazini
M1 Libya vs Tunisia
M2 Morocco vs Libya

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages