Waandaaji
wa mbio za kimataifa za Ngorongoro Maratahoni katika mkutano na
wanahabari kuzungumzia maandalizi ya mwisho ya mbio hizo zinazotarajia
kufanyika Aprili 18 mwaka huu ,Karatu mkoani Arusha.
Mkurugenzi
wa Zara Tanzania Adventure na Zara Charity,Zainab Ansel akizungumza na
wanahabari kuhusu maandalizi ya mbio hizo ambazo zinadhaminiwa na
Shirika lisilo la kiserikali la Zara Charity.
Mratibu
wa Mbio za Kilimanjaro Marathoni Meta Peter akizungumzuia wanariadha wa
Tanzania ambao wanartarajia kushiriki Mbio hizo huku akisema mbio za
mwaka huu zitashirikisha wanariadha walioshiriki mbio za dunia za Nyika
mwaka huu watakao toana jasho na wakimbiaji kutoka nchini Kenya,Uganda
na Malawi.(P.T)
Muongozaji wa Mbio hizo kutoka kampuni ya Zara Tour ,Frances Kilawe akizungumza historia ya Mbio hizo.
Mwakilishi
wa shirika lisilo la kiserikali la Zara Charity Datus Mmary
akizungumzia lengo la mbo hizo ambao awali ilikuwa ni kuchangia katika
kutokomeza Marelia na mbio za mwaka huu zitakuwa ni kwa ajili ya
kuchangia elimu hasa kwa watoto wa jamii ya wafugaji.
Mwakilishi
wa kampuni ya Bonite Bottlers ,Leonard Makule akizungumzia juu ya
udhamini wa kampuni hiyo katika mbio za kimataifa za Ngorongoro
Marathoni 2015.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269