Breaking News

Your Ad Spot

Apr 13, 2015

MBOWE AKABIDHI AMBULANCE MBLI KWA HOSPITALI YA WILAYA YA HAI NA HOSPITALI YA MACHAME

 
Magari mawili ya kubebea wagonjwa(Ambulance) yaliyotolewa na Mbunge wa jimbo
la Hai,Freeman Mbowe yakiwasili katika viwanja vya soko la Kuni kwa
ajili ya kukabidhiwa kwa viongozi wa hosptali ya wilaya ya Hai pamoja
na hosptali ya Machame inayosimamiwa na kanisa la
KKKT.
Haya ni maneno yaliyoandikwa katika magari hayo.
Mbunge wa jimbo la Hai,Freeman Mbowe akiwa amembeba mtoto mara baada ya
kuwasili katika viwanja vya Kuni na kulakiwa na wananchi katika jimbo
hilo.
Magari ya wagonjwa yaliyotolewa na Mbunge wa Jimbo la Hai kwa ajili ya
wagonjwa jimboni humo.
Mbunge Mbowe akiwa amembeba moja ya watoto waliofika uwanjani hapo kwa ajili ya kushuhudia msaada wa magari ya wagonjwa yaliyotolewa na mbunge huyo
kwa watu wa jimbo la Hai.
Muonekano wa ndani wa magari hayo ya kubebea wagonjwa
Baadhi ya viongozi mbalimbali waliohudhuria shighuli ya makabidhiano
iliyofanyika katika uwanja wa Kuni ,Bomang’ombe wilayani
Hai.
Wananchi wakiwa wamezingira magari hayo wakiyatizama kwa
karibu.
Mbunge wa jimbo la Hai ,akiuzungumza juu ya msaada huo kwa watu wa jimbo la
Hai.
Mbunge wa jimbo la Hai,Freeman Mbowe akikabidhi nyaraka mbalimbali za magari
hayo kwa Baba Mchungaji Asanterabi Swai ambaye pia ni mkuu wa jimbo
kwa niaba ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheli Tanzania
(KKKT).
Mmoja wa viongozi wa Machame Hosptal ,Swai akifurahia msaada wa gari hilo la
wagonjwa kwa hosptali yake.
Mbunge wa jimbo la Hai,Freeman Mbowe akikabidhi funguo wa gari kwa mganga mkuu wa wilaya ya Hai,Dkt Paul Chawote ,msada uliotolewa kwa ajili ya
hosptali ya wilaya ya Hai.
Watumishi wa hosptali ya wilaya ya Hai,wakiondoka katika
viwanja hivyo mara baada ya kukabidhiwa gari hilo.
Wananchi wakifurahia msaada huo.
Baadhi ya wananchi waliofika kushuhudia makabidhiano ya msaada huo wa magari
ya kubebea wagonjwa.
Mbunge wa Jimbo la Hai ,Freeeman Mbowe akizungumza na wananchi mara baada ya kukabidhi msaada wa magari mawili ya kubebea
wagonjwa.
 

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages