Rais Jakaya Kikwete akikabidhi
tuzo ya Meya Bora Tanzania kwa Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuph
Mwenda baada ya kushinda tuzo hiyo kitaifa iliyoandaliwa na Jumuiya ya
Tawala za Mitaa nchini (ALAT) katika hafla iliyofanyika Dar es Salaam
juzi. Kulia ni Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (TAMISEMI),
Agrey Mwanri.
Rais Jakaya Kikwete akizungumza
baada ya kukabidhi Tuzo ya Meya Bora Tanzania, Yusuph Mwenda (kulia)
baada ya kushinda tuzo hizo zilizoandaliwa na Jumuiya ya Tawala za Mitaa
nchini (ALAT) katika hafla iliyofanyika Dar es Salaam juzi. Kushoto ni
Ofisa Mtendaji Mkuu wa benki ya NMB, Tom Boghols na Waziri wa Nchi,
Ofisi ya Waziri Mkuu (TAMISEMI), Hawa Ghasia (wa pili kushoto).
Rais Jakaya Kikwete akitoa
maelekezo kwa Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuph Mwenda (kulia)
kuhusu namna bora ya matumizi ya trekta baada ya kumkabidhi Meya huyo
baada ya kushinda Tuzo ya Meya Bora Tanzania kwenye hafla iliyofanyika
Dar es Salaam hivi karibuni. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,
Saidi Meck Sadiki na Ofisa Mtendaji Mkuu wa benki ya NMB, Tom Boghols
(wa pili kulia).
Meya wa Manispaa ya Kinondoni,
Yusuph Mwenda akijaribu kuendesha trekta alilokabidhiwa na Rais Jakaya
Kikwete baada ya kushinda tuzo ya Meya Bora Tanzania.
…………………………………………………………………
Na Mwandishi Maalum,
Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuph Mwenda ameshinda Tuzo ya Meya Bora Tanzania na kuzishinda Halmashauri 168 zote nchini.
Akizungumza mara baada ya
kukabidhiwa tuzo hiyo na Rais Jakaya Kikwete ambaye alikuwa mgeni rasmi
katika hafla hiyo, Meya wa Manispaa hiyo, Yusuph Mwenda amesema siti ya
kushinda tuzo hiyo ni kufanya kazi kwa pamoja kati yake Madiwani,
Watendaji na kuwahsirikisha wananchi wake.
Meya Mwenda alisema kuwa
Halmashauri yake imekuwa ikifanya kazi kwa uwazi zaidi kwa
kuwashirikisha wananchi wake katika mikakati ya kimaendeleo ikiwemo
kuwashirikisha katika miadi mbalimbali ya Halmashauri hiyo na hivyo
kujikuta kazi yake inakuwa rahisi na kupata mafanikio makubwa kwa muda
mfupi.
Mwenda alisema kuwa Manispa yake
imekuwa mstari wa mbele katika kusimamia na kuitekeleza miradi yake kwa
bidii kubwa ikiwemo ukusanyaji mapato na usimamizi mzuri wa matumizi ya
mapato hayo katika miradi hiyo.
“Ushirikiano ‘team work’ kati
yangu na madiwani, Madiwani na Watendaji, Ofisi ya Mkuu wa Wialaya na
Mkuu wa Mkoandio siri ya mafanikio. Lakini kubwa zaidi ni wananchi
wenyewe, kupitia wao tumeweza kuwa na mendeleo zaidi.” Alisema Mwenda.
Aidha Meya Mwenda alisema kuwa
Halmashauri yake imefanikiwa kufikia malengo yake kutoka na kuongezeka
kwa mapato ya ndani kwa aslimia 360 kutoka shilingi Bilioni 10 mwaka
2011/ 2011 mpaka kufikia Bilioni 36 mwaka jana na kuiwezesha Manispaa
hiyo kusimamia vema miradi yake yenyewe.
Aliitaja miradi hiyo ni pamoja na
ujenzi wa Barabara, Madara, Zahanati, Shule, matumizi ya Teknohama
pamoja na ujenzi wa Kituo kikubwa cha daladala cha kisasa cha Sinza
ambacho ujenzi wake umegharimu shilingi bilioni 4.06.
Aidha alisema Halmashauri yake
imeweza kuongeza fedha za miradi yake ya maendeleo kutoka Bilioni 3.2
kwa mwaka 2011 mpaka kufikia Bilioni 16 na hivyo kuifanya kuwa ya kwanza
nchini kusimamia miradi yake kwa fedha za mapato ya ndani kwa asilimia
kubwa.
Hii ni mara ya kwanza kufanyika
kwa shindano la Tuzo za Meya Bora Tanzania chini ya Jumuiya ya Serikali
za Mitaa nchini (ALAT) ambazo zilikuwa katika makundi mawili makuu
ambayo ni Tuzo ya Maendeleo ya Halmashauri na Tuzo ya Jumla ambazo
zilifanyika juzi na kuhudhuriwa na Rais Jakaya Kikwete.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269