Meya wa Manispaa ya Kinondoni Yusuf Mwenda akipanda mti katika maadhimisho hayo.
Mratibu
wa mazingira kutoka Taasisi ya EBPA, Charles Lugenga (kushoto), akitoa
maelezo mbele ya mkuu wa mkoa na viongozi wengine wa Manispaa Kinondoni
jinsi ya upandaji wa mimea mbalimbali pamoja na miti kwa kutumia matairi
ya magari yaliyotumika.
Wanafunzi wa shule hiyo wakiwa wamebeba miche ya miti wakielekea kuipanda katika maeneo mbalimbali shuleni hapo.
Wananchi mbalimbali waliohudhuria maadhimisho hayo ya upandaji miti.
Wanafunzi wa shule hiyo wakiwa kwenye sherehe hiyo.
Msanii akitoa burudani kwenye maadhimisho hayo.
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni akipanda mti.
Diwani wa Kata ya Mabwepande, Clement Bocco akipanda mti katika eneo la shule ya Mji Mpya.
Mratibu
wa mazingira kutoka Taasisi ya EBPA, Charles Lugenga (kushoto),
akimpatia Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Saidi Sadiki kikapu
kilichotengenezwa kwa matairi yaliyotumika baada ya maadhimisho hayo.
Wasanii wakitoa burudani.
Maofisa wa Manispaa ya Kinondoni wakiwa kwenye
maadhimisho hayo.
Meya
wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuf Mwenda (kushoto), na Mkuu wa Wilaya ya
Kinondoni, Paul Makonda wakiserebuka pamoja na wananchi katika
maadhimisho hayo ya upandaji miti mkoa wa Dar es Salaam yaliyofanyika
leo viwanja vya Shule ya Msingi Mji Mpya iliyopo Mabwepande.
Wananchi wakicheza segere baada ya kumalizika kwa zoezi
hilo la upandaji miti.
………………………………………………….
Na Dotto Mwaibale
SERIKALI imesema waathirika wa
mafuriko ya mto Msimbazi walioondoka baada ya kupewa viwanja maeneo ya
Mabwepande na kurudi eneo la Msimbazi watanyang’anywa viwanja hivyo.Kauli
hiyo ilitolewa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Sadiki kwenye
maadhimisho ya kilele cha wiki ya upandaji miti Mkoa wa Dar es Salaam
yaliyofikia tamati leo kwa upandaji miti kwenye viwanja vya Shule ya
Msingi ya Mji Mpya iliyopo Mabwepande ambapo Wilaya ya Kinondoni ilikuwa
mwenyeji.“Natoa maagizo kuwa wale wote waliopewa
viwanja na serikali hapa Mabwepande ambao wameondoka viwanja vyao
wanyang’anywe kwani ni wasariti na wale waliouziwa imekula kwao kwani
serikali haiwatambui” alisema Sadiki.
Sadiki alitoa mwito kwa wananchi kubadilika kwa kuacha
kutumia nishati ya miti na mkaa badala yake watumie gesi ambayo
inapatikana kwa wingi kutokana na jitihada za serikali ili kulinda
mazingira.
Aliongeza kuwa suala la upandaji miti ni endelevu hivyo kila
mtu mahali alipo apande mti walau mmoja na kuitunza kwani miti ni uhai.
Meya wa Manispaa ya Kinondoni Yusuf Mwenda alisema Manispaa
hiyo inabustani kubwa maeneo ya Kilongawima hivyo wanajipanga kuanzisha
mashindano ya ukuzaji na upandaji wa miti kwa kata zake 34 na mshindi
atapatiwa zawadi.
Katika hatua nyingine amesema halmshauri hiyo itawakopesha
fedha wananchi waishio Mabwepande ambao waliathiriwa na mafuriko kwa
ajili ya kukamilisha upatikanaji wa hati za umiliki wa viwanja vyao
kabla ya mwezi wa sita badala ya kusubiri fedha kutoka ofisi ya Waziri
Mkuu.
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda alisema changamoto
ya kukamilika kwa nyumba za askari polisi na kituo cha polisi katika
eneo hilo itakwisha katika kipindi kifupi kijacho
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269