Ratiba ya nusu fainali ya michuano hiyo imepangwa muda mfupi uliopita, huko Nyon – Uswiss.
Ratiba
inaonyesha Luis Enrique ataiongoza FC Barcelona kukipiga dhidi ya FC
Bayern Munich inayofundishwa na mchezaji mwenzie wa zamani wa Barca –
Pep Guardiola.
Guardiola na Luis Enrique walikuwa kwenye kikosi kimoja cha Barca kilichokuwa kikifundishwa na Van Gaal msimu wa 1999/2000.
Kwa
upande mwingine mabingwa watetezi wa kombe hilo, Real Madrid watacheza
dhidi ya Juventus. Mechi za raundi ya kwanza zitachezwa Mei 5 na 6 na
marudiano zitakuwa wiki moja itakayofuatia ya tarehe 12 na 13.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269