Ofisa
Uhusiano Mwandamizi wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Doris Malulu
(kulia), akikabidhi mfano wa hundi ya sh Milioni 69 kwa Mwenyekiti wa
Serikali ya Mtaa wa Vituka, Bi. Amina Rashid Simba kwa ajili ya kuchimba
visima vya maji katika maeneo ya Vituka na Mwembeladu, Manispaa ya
Temeke, Dar es Salaam jana. Wengine katika picha ni Katibu wa Diwani Bw.
Ismail Ng'ombo (wa pili kulia), Bw. Kassimu Makoa na Bi. Zubeda Ali
Ligubike aliyetoa eneo la mradi huo. (Na Mpigapicha Wetu)
Mwenyekiti
wa Serikali ya Mtaa wa Vituka, Bi. Amina Simba (kulia), akikabidhi
mfano wa hundi ya sh. milioni 69 kwa Mhandisi Mo Resources Ltd Bw.
Onesmo Sigala zilizotolewa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), kwa ajili
ya mradi wa maji katika mitaa ya Vituka na Mwembeladu, Manispaa ya
Temeke, Dar es Salaam jana. Kulia ni Ofisa Uhusiano Mwandamizi wa TBL,
Bi. Doris Malulu, Katibu wa Diwani Bw. Ismail Ng'ombo (wa pili kulia),
Bw. Kassimu Makoa na Bi. Zubeda Ali Ligubike aliyetoa kiwanja cha mradi
huo. (PICHA NA MDAU WA UJIJIRAHAA BLOG)
Ofisa
Uhusiano Mwandamizi wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Doris Malulu
akimpongeza Bi. Zubeda Ligubike kwa kutoa kiwanja kwa ajili ya kuchimba
kisima cha maji.
Ofisa
Uhusiano Mwandamizi wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Doris Malulu
akizungumza na wakazi wa Mitaa ya Vituka na Mwembeladu, Manispaa ya
Temeke, Dar es Salaam baada ya kukabidhi mfano wa Hundi ya sh. milioni
69 zilizotolewa na TBL kwa ajili ya mradi wa maji.
Malulu akikagua mitambo ya kuchimba kisima
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269