Kutoka
kushoto ni Reginald Munisi, Mwenyekiti, United Nations Association of
Tazania, Mr. Alvaro Rodriguez, Mratibu Mkazi, Umoja wa Mataifa Tanzania,
Balozi Dr. Agustine Mahiga, Balozi Mstaafu wa Tazania Umoja wa Mataifa
na Mwakilishi wakiwa katika Maadhimisho ya Miaka 50 Taasisi ya Umoja wa
Matifa (UNA) pamoja na maadhimisho ya miaka 70 ya umoja wa Mataifa (UN)
yaliyofanyika leo jijini Dar es Salaam.
Reginald Munisi, Mwenyekiti wa UNA Tanzania akitoa maneno ya ufunguzi katika mkutano mkuu wa UNA Tanzania.
Washiriki katika mkutano mkuu wa UNA Tanzania.
Mr. Alvaro Rodriguez, Mwakilishi Mkazi wa Umoja wa Mataifa, na Mgeni Rasmi, Tanzania akifungua mkutano mkuu wa UNA Tanzania.
Washiriki katika picha ya pamoja.
Balozi Dr. Agustine Mahiga akizungumza na waandiahi wa habari.
Reginald Munisi, Mwenyekiti wa UNA Tanzania, akizungumza na waandishi wa habari.
Mr.
Alvaro Rodriguez, Mwakilishi Mkazi wa Umoja wa Mataifa na Mgeni Rasmi
akizindua kipengele cha “Ask the UN RC” katika wavuti ya UNA Tanzania –
www.una.or.tz
—
Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
UMOJA
wa Mataifa (UN) ni taasisi imara katika kusimamia maendeleo ya wananchi
pamoja na kutatua migogoro mbalimbali ya nchi ya vita kwa nchi
wanachama wa umoja huo.
Hayo
ameyasema leo Balozi Agustine Mahija wakati wa Maadhimisho ya Miaka 50
Taasisi ya Umoja wa Matifa (UNA) pamoja na maadhimisho ya miaka 70 ya
umoja wa Mataifa (UN) iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam.
Mahija
alisema Umoja wa Mataifa (UN) umekuwa mstari wa mbele katika kutatua
migogoro ikiwa ni kufanya wananchi waishi maisha ya amani kwa kuanzisha
baraza la usalama wa Umoja wa Matiafa ambalo limekuwa likishughulikia
migogoro mbalimbali.
Amesema
UN imeweza kuweka malengo mbalimbali ya kiuchumi kwa nchi 195 zilizo
katika umoja huo katika kuweza kuondokana na umasikini kwa kubuni miradi
ambayo yameleta tija kwa mataifa mbalimbali.
Naye
Mwenyekiti waTaasisi ya Umoja wa Mataifa UNA Tanzania. Reginald Munisi
amesema katika kuelekea uchaguzi vyombo vinavyoshughulikia ulinzi
visijihusishe na siasa ili wananchi waweze bkupiga kura kwa amani.
Munisi
amesema vyombo vya ulinzi vikijihusisha na siasa wananchi watashindwa
kushirika katika uchaguzi wa kuchagua viongozi wao ambao ndio
wanawategemea katika maendeleo ya nchi.
Aidha
alisema UNA Tanzania itatoa eli kwa vyombo vya ulinzi katika kuelekea
uchaguzi ikiwa ni lengo la kuwafanya wananchi waweze kupiga kura kwa
amini na kuweza kuwapata viongozi wao.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269