Breaking News

Your Ad Spot

Apr 7, 2015

ZIMAMOTO IRINGA WATOA MISAADA KWA WATOTO YATIMA

1
Kamanda wa jeshi la zimamoto mkoa wa iringa akikabidhi mbuzi kwa kaimu mkuu wa kituo cha Sister Theresa, Sister Sister  Winfrida Mhongole  katika makabidhiano yaliyofanyika kituoni hapo,
2
Kamanda wa Zimamoto akiwa na mmoja wa watoto wanaolelewa na kituo hicho cha sister Theresa.
3
Mmoja wa Askari wa jeshi la Zimamoto Eshter Aidan akiwa na watoto wanaolelewa katika kituo cha sister Theresa.
………………………………………………..
NA DENIS MLOWE,IRINGA
JESHI la Zimamoto mkoani Iringa limesheherekea sikukuu ya pasaka  na watoto  wanaoishi katika kituo cha kulea yatima cha Sister Theresia  kilichoko Tosamaganga mkoani Iringa kwa kuwapatia misaada mbalimbali.
Akikabidhi msaada huo Kamanda wa Jeshi la Zimamoto mkoa wa Iringa Inspekta Kennedy Komba alisema lengo kubwa la jeshi hilo ni kuwa karibu zaidi na jamii katika kutoa misaada ambayo itawasaidia yatima walioko katika vituo mbalimbali mkoani hapa.
Alisema yatima wanakabiliana na mazingira magumu katika kupata mahitaji muhimu hasa chakula, afya na malazi hivyo ni jukumu la kila mmoja kuweza kuwasaidia kuondokana na hali ya utegemezi.
“Tumeamua kugawa msaada huu kwa kuguswa na matatizo mbalimbali wanayokabiliana nao vituo vingi vya kulelea watoto hapa nchini katika harakati zetu za kuhahikisha watoto yatima wanapata mahitaji muhimu katika maisha yao ya kil siku huu ni mwanzo tu wa jeshi la zimamoto katika kuwa karibu na jamii na hii tunafanya kila mwaka kuweza kurudisha pia katika jamii kile ambacho jeshi hilo linapata” alisema Komba
Alisema msaada uliotolewa wa mchele kilo hamsini, mbuzi, mafuta ya kupikia, sabuni na kuwapatia kifaa cha kuzimia moto (Fire extinguisher) baada ya kuwapa mafunzo ya jinsi ya kutumia vyote vikiwa na jumla ya thamani ya shilingi laki 250,000.
Komba alisema jeshi la zimamoto litakuwa likitoa msaada wa aina hiyo kila mara ili kujiweka karibu na jamii kuweza kutambua shughuli wanazofanya na kuwataka wadau wengine kuiga jeshi hilo katika kuwasaidia watoto yatima.
“Jamii ya Kitanzania yatakiwa kuunga mkono tabia ya kuwasaidia watoto yatima na kuwaimiza kupenda masomo yao na jamii kutowatumia kama watoto wa kazi za ndani na kuwahudumia kwa kila jambo wanalofanya kuliko kutumia muda mwingi katika matumizi ya anasa” alisema Komba
Kwa upande wake kaimu msimamizi wa kituo hicho Sister  Winfrida Mhongole  alilishukuru jeshi la zimamoto kwa msaada huo na kuwataka wadau wengine wawe na moyo wa kujitolea kwa watoto yatima wanaolelewa katika vituo tofauti mkoani hapa.
Alisema kituo kina jumla ya watoto 280 ambao mbali na hao watoto 72 wanaishi kituoni hapo na wengine wako katika shule mbalimbali wakisoma zikiwemo za msingi na sekondari.
Alisema watoto hao wamepokelewa kutoka mikoa mbalimbali ikiwemo ya Iringa, Mbeya, Njombe, Morogoro, Dar es Salaam na Morogoro.
“Mbali na mapato yatokanayo na shughuli za kilimo tunazozifanya kama kituo, kituo hiki kinaendeshwa kwa michango ya wahisani mbalimbali wa ndani na nje. Kwa kweli hatuna wafadhili wa kudumu,” alisema na kuomba wahisani waendelee kujitokeza kuwasaidia.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages