Tukio la chatu mwenye urefu wa futi 10 akimmeza mbuzi mzimamzima limewatia
hofu wakazi wa Kijiji cha Garkhuta kilichopo Magharibi mwa Bengal nchini
India.
Tukio
hilo lilinaswa na Mpigapicha, Roni Choudhury hivi karibuni wakati
akitembea jirani na Hifadhi ya Msitu wa Sonakhali nchini India.
Kitendo hicho kiliwafanya wanakijiji waingiwe na hofu huku Ofisa Misitu wa Wilaya, Vidyut Sarkar akisema kuwa: 'Iwapo chatu huyo alimkamata mbuzi, anaweza pia kumuua hata mwanaume au mtoto'.
Tukio
hilo lilivuta hisia za watu wengi ambao hawakuonyesha kumuogopa sana
chatu huyo aliyekuwa akimmeza mbuzi na badala yake kushuhudia tukio
zima. Ilimchukua chatu huyo saa nne kummeza mbuzi huyo.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269