Breaking News

Your Ad Spot

May 10, 2015

FILIKUNJOMBE AKABIDHI MSAADA WA TSH MILIONI 40 KIJIJI CHA MAVANGA ASEMA CCM SI MBAYA WABAYA WATU

Mbunge  wa  jimbo la  Ludewa  Deo  Filikunjombe akiwhutubia  wakazi  wa  kijiji  cha Mavanga  wilayani Ludewa  muda mfupi  baada ya  kukabidhi msaada wa  vitu mbali mbali  vya  ujenzi vyenye thamani ya Tsh milioni 40 katika  kijiji hicho
 
  Viongozi  wa  kijiji  cha Mavanga  akiwemo mwenyekiti wa kijiji Bw Hilmar Mpambichaka ( Chadema )kulia  wakipokea  misaada  ya vifaa vya  ujenzi  toka kwa mbunge Filikunjombe kushoto.
 Wananchi  wa Mavanga  wakiwa  wamepanda  juu ya magari na  miti kumwona  mbunge  Filikunjombe.
 Wananchi  wakiwa juu ya miti  wakifuatilia  hotuba ya  mbunge  wao  Deo Filikunjombe.

 Mbunge  Filikunjombe  akifurahia  jambo  wakati  mkazi  wa  Mavanga akimtaka kuwa  mbunge hadi atakapochoka yeye

 Mwanahabari  wa  kituo cha Radio  Best  Ludewa Deo  Nyoni  akiwa makini  kufuatilia matukio
 Wananchi  wa Mavanga  wakiwa wamebeba  kitanda  cha  kujifungulia  wanawake  wajawazito kilichotolewa na mbunge  Filikunjombe kitanda  chenye thamani ya Tsh milioni 5.2

 Mwenyekiti  wa kijiji  Cha Mavanga Bw Hilmar Mpambichaka ( Chadema )akimpongeza  mbunge Filikunjombe kwa  misaada  yake
 Paroko  wa kanisa la Anglicana   kushoto  akipokea  msaada  wa bati  300  kutoka kwa mbunge  Deo Filikunjombe
 
 Mbunge Filikunjombe  kati  akikabidhi  saruji kwa ajili ya shule ya  msingi kijiji  cha Mavanga
 Saruji   iliyotolewa na  mbunge  Filikunjombe Mavanga
 Mbunge Filikunjombe akikabidhi  kitanda cha  wanawake wajawazito  kujifungulia
 Mbunge  Filikunjombe akiwakabidhi  wajawazito  kitanda  cha  kujifungulia
 Mwenyekiti  wa  kijiji  cha Mavanga Bw Hilmar Mpambichaka ( Chadema )akiwa  amepokea msaada wa Darubini toka kwa mbunge Deo  Filikunjombe
 Filikunjombe  akiwahutubia  wananchi  wa Mavanga
 Wananchi  Mavanga  wakiwa katika   foleni ya  kuuliza maswali na  kumpongeza  mbunge wao
 Mbunge  Filikunjombe akimkabidhi mpira  kijana wa Chadema kijiji  cha Mavanga
 Kijana  wa  Chadema  akimpongeza mbunge Filikunjombe
 Wananchi  Mavanga  wakimkabidhi  zawadi ya  kuku mbunge  wao Filikunjombe
 Mbunge Filikunjombe akipokea zawadi  ya  mbuzi toka kwa  vingozi wa kanisa la Anglicana  baada ya kuwasaidia bati 300 za  ujenzi wa kanisa
 Mwenyekiti  wa  kijiji  cha Mavanga Bw Hilmar Mpambichaka ( Chadema )akimongeza mbunge Filikunjombe
 Filikunjombe akizungumza na mlemavu  aliyefika  katika mkutano  wake
 Wananchi  wa  kijiji  cha Mavanga  wakiwa  wamembeba mbunge  wa Ludewa  Deo Filikunjombe
 Msafara  wa  mbunge  Filikunjombe kijiji  cha Mavanga
 Mbunge wa  Ludewa  Deo Filikunjombe akiwapungia mikono  wananchi wa kata ya Mavanga
 Waendesha  boda  boda  wakiongoza msafara wa mbunge Filikunjombe kwa mbwembwe
 Mbunge  Filikunjombe akiwasikiliza wanafunzi katika  kijiji  cha Mavanga
 Mbunge Filikunjombe akicheza mpira na  wanafunzi  hao  baada ya kuwapa msaada wa mpira na sukari kwa mwaka  mzima
 Wasanii  wa ngoma katika  kijiji  cha Mavanga  wakishiriki kupiga ngoma na mbunge wa Ludewa Deo Filikunjombe kushoto
 Katibu  mwenezi mkoa wa Njombe Honoratus  Mgaya akishiriki  kucheza  ngoma
Mbunge Filikunnjombe na katibu mwenezi wa CCM mkoa wa Njombe Bw Mgaya  wakicheza ngoma
 
………………………………………………………………………
Na MatukiodaimaBlog
MBUNGE
wa jimbo la Ludewa mkoani Njombe Deo Filikunjombe asema baadhi ya
wabunge ,mawaziri na watendaji wabovu serikalini wanakichafua chama cha
mapinduzi ( CCM )
Filikunjombe alisema kuwa
Ccm ni chama makini na kinachopendwa sana ila shida ipo kwa baadhi ya
watu waliopo ndani ya Ccm na serikali ni bomu
mbunge
huyo alitoa kauli hiyo leo  katika kijiji cha Mavanga wakati akijibu
maswali ya wananchi na viongozi wa vyama vinavyounda katiba ya wananchi (
Ukawa) kuhusiana na Ccm kuwateulia wananchi viongozi wasio na sifa
kugombea nafasi mbali mbali.
Alisema kama kila
mmoja angetimiza wajibu wake katika nafasi yake hakuna mpinzani ambae
angechaguliwa ila kuchaguliwa kwa wapinzani ni kushindwa kwa wale
waliowaamini kutoka Ccm kushindwa kuwajibika kwa wananchi waliowaamini
Filikunjombe
alisema atakuwa mbunge wa mwisho kunyoshewa kidole na watanzania
wakiwemo wananchi wake wa Ludewa kwa kushindwa kuwatumikia wananchi na
chama chake cha Ccm .
Kwani
alisema hakuomba ubunge kwa ajili ya kujinufaisha binafsi ila aliamua
kugombea ili kuwatumikia wana Ludewa kwa kuwapelekea maendeleo hivyo
Kazi Yake kwa sasa hadi mwisho wa ubunge wake ni kuleta maendeleo kwa
wananchi wake na kuona ahadi zake zinatimia kwa muda uliopangwa na si
kujinufaisha kwa wakati.
Naomba kwanza mtambue kuwa wabunge wote tulipo fika bungeni kwa mara ya
kwanza tulikopeshwa Tsh milioni 90 kwa ajili ya kununua gari la
kutembelea na Mimi kwa kuwa nilikuwa na gari pesa hizo niliamua kununua
gari la wagonjwa Mlangali ambao hawakuwa na gari la wagonjwa
….lengo langu kutumikia wananchi na kuwatatulia kero zao si
vinginevyo”
Akielezea msaada huo wa vitu mbali
mbali vyenye thamani ya Tsh milioni 40 alivyotoa alisema ni pamoja na
kitanda cha kujifungulia wajawazito chenye thamani ya Tsh milioni
5.2,Darubini ,pesa ya taslimu Tsh milioni 1 bati zaidi ya 500 ,rangi
debe 20 ,saruji zaidi 525 na vifaa vingine vingi kwa ajili ya
kuchangia ujenzi wa miradi mbali mbali ya kijiji na ujenzi wa
makanisa,shule na wodi la wazazi
Awali
viongozi ukawa wa kijiji cha Mavanga kata kata ya Mavanga walimpingeza
mbunge Filikunjombe kwa kuwa mbunge wa mfano Ludewa japo wapo viongozi
wengi ndani ya chama chake ni wabovu.
Mwenyekiti
wa Ukawa Mavanga John Mligo akishukuru kwa msaada huo wa vifaa na
fedha toka kwa mbunge Filikunjombe alisema kama wabunge na viongozi wote
wangefanya kama Filikunjombe kamwe wananchi wasingechukia chama
hicho.
Akizungumza
katika mkutano huo mwenyekiti huyo wa Ukawa na mwenyekiti wa serikali
ya Kijiji cha Mavanga Bw Hilmar Mpambichaka ( Chadema ) walisema wao
kama viongozi wa upinzani hawana shaka na uwakilishi wa mbunge
Filikunjombe ndani ya jimbo hilo na nje ya jimbo hilo”
Tumekuwa na wabunge 7 ambao wametangulia kabla ya Filikunjombe ila
uwakilishi wake umekuwa wa kuigwa na wabunge wengine na kama wabunge
kote nchini wangekuwa watendaji hivyo huenda upinzani nchini
usingekuwepo”alisema Mligo
Kwani
alisema kuwa Chanzo cha kijiji hicho kuchagua mwenyekiti wa Serikali ya
kijiji kutoka Chadema ni baada ya viongozi wa ccm kuonyesha kuwa mbali
na wananchi na baadhi Yao kutafuna pesa za michango ya wananchi .
Bw
Mligo alisema shida ndani ya Ccm ni vita ya wenyewe kwa wenyewe ndio
ambayo imekuwa ikiwachanganya wananchi na kujikuta wananchi wanaingia
katika
mgawanyiko na kuchagua wapinzani
Alisema
wakati wa kampeni hata wasio na sifa wanataka kuchaguliwa kwa kutumia
rushwa ,hivyo kutaka kwa Ludewa kutambua wazi mbunge anayekubalika ni
Filikunjombe pekee na kuwa hawahitaji mtu zaidi ya mbunge wao
aliyewavusha katika maendeleo
Huku
mwenyekiti wa serikali ya kijiji hicho Bw Mpambichaka akiwataka
wananchi wa Ludewa kuacha kuonja sumu kwa kubadili wabunge na kuwa
utendaji wa Filikunjombe hakuna wa kumfananisha nae
Alisema
kuwa wamepata kushuhudia utendaji wake ndani ya bunge kupitia kamati ya
PAC kwa kupambana na ufisadi kupitia Escrow na kuwafanya mawaziri zaidi
ya watatu kujiuzulu
Pia
kupitia utendaji wake ndani ya jimbo amefanikiwa kuwavuta wana Ludewa
ambao siku zote walikuwa wakiona aibu kuweka wazi kuwa ni wakazi wa
Ludewa na badala Yake kudanganya kuwa wao ni wazaliwa wa Mkoa wa Ruvuma
kutokana na awali
Ludewa kuwa nyuma kwa maendeleo .

Toka Filikunjombe ameingia madarakani mwaka 2010 na kuwepo kwa kasi ya
maendeleo ndio tunashuhudia wana Ludewa wakirejea Nyumbani na
kujitangaza kuwa wao ni wakazi wa Ludewa tofauti na zamani wengi
walikuwa wakijificha kwa aibu “
Hata
hivyo alisema wapo wabunge ambao wamekaa majimboni muda mwingi kama
akina Mzindakaya huko Sumbawanga ila siku zote ni mtu wa kueleza jinsi
alivyofanya Kazi na Mwl Julius Nyerere ila si kujipambanua namna gani
alivyoleta maendeleo jimboni
Kuhusu
misaada mbali mbali iliyotolewa na mbunge huyo kijijini hapo mwenyekiti
huyo alisema kwa mara ya kwanza toka wabunge 7 waliopita kijiji hicho
kimepata kupata misaada mingi kutoka kwa mbunge

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages