Hyon (kulia) alichaguliwa mwaka 2012 kuwa Waziri wa Ulinzi wa Korea ya Kaskazini.
Uchunguzi umeonyesha kwamba watu wengi waliuawa kwa kutumia njia hiyo ya kikatili katika kambi hiyo mwezi Oktoba mwaka jana.
Hyon Yong-Chol aliyeuawa kwa kusinzia wakati wa hafla ya kijeshi.
WAZIRI wa
Ulinzi wa Korea ya Kaskazini, Hyon Yong-Chol, ameuawa kwa kupigwa na
bunduki ya kutungulia ndege aina ya ZPU-4 kwa kusinzia kwenye hafla ya
kijeshi. Waziri huyo aliuawa kutokana na amri ya kiongozi wa nchi hiyo,
Kim Jong-Un.
Bunduki ya kutungulia ndege aina ya ZPU-4 iliyotumika kumuua Hyon.
Sababu
nyingine iliyomfanya waziri huyo aliyekuwa na umri wa miaka 66 na
aliyekuwa kiongozi wa jeshi la nchi hiyo tangu mwaka 2012 auawe, ni
kutoa kauli za kumpinga kiongozi wa nchi hiyo, Kim Jong-Un katika
matukio kadhaa.
Hyon
aliuawa mbele ya mamia ya maofisa wa serikali na jeshi katika kambi moja
mjini Pyongyang tarehe 30 Aprili mwaka huu ambapo aliyemuua alisimama
umbali wa futi 100 tu akitumia bunduki hiyo ambayo inaweza kufika umbali
wa futi 26,000
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269