Lori la mchana likiwa limepinduka baada ya ajali
Ajali
hiyo imetokea leo jioni eneo la Boma mbuzi pasua katika barabara
iendayo kiwanda cha sukari TPC,imehusisha magari mawili ambayo ni Toyota
haice yenye namba za usajili SU 37299 mali ya chuo cha mafunzo ya
ufundi VETA lililogongana uso kwa uso na Tipa la mchanga lenye namba za
usajili T 202 BFT na kusababisha tipa hilo kupinduka.
Kwa
mujibu wa maelezo ya askari wa barabarani aliyefika katika eneo la
tukio,aliyepata majeraha makubwa ni dereva (mwanafunzi) ambaye jina lake
halijafahamika na amewahishwa kupata matibabu.
Kwa
upande wa dereva wa lori hilo bwana Victor mbaye amepata mshituko katika
mguu wake wa kulia ameelezea chanzo cha ajali hiyo kuwa ni dereva wa
haice kuingia kwa kasi katika barabara hiyo akitokea upande wa kushoto
wa barabara hiyo hivyo na kushindwa kulimudu gari na hatimaye kulifuata
lori hilo.
Kushoto
ni dereva wa Lori akiongea na askari wa barabarani ,aliyejishika kifuani
ni mwalimu wa VETA aliyekuwa akiwaongoza wanafunzi katika haice
iliyohusika katika ajali
Utingo wa lori akikusanya mchanga uliomwagika baada ya ajali
“Mimi
nilikuwa nikipandisha kutokea upande wa Serengeti (breweries) kwa
kawaida nilitegemea derevawa haice angesubiri nipite kwani nilikuwa
upande wake wa kulia lakini cha kushangaza aliingia bila kutoa ishara na
gari ilipomshinda alikuja upande wangu,nilijaribu kumkwepa lakini
ilishindikana kwani alisha karibia sana na baada ya kugongana gari langu
lipinduka kutokana na uzito wa mchanga niliyokuwa nimebeba”.
Askari wa barabarani akijaribu kuwatuliza wananchi walitaka kumpiga mwalimu wa VETA
Hali ya
tafrani ilizuka mara baada ya mwalimu wa VETA kumueleza askari wa
usalama wa barabarani waliofika eneo hilo kuwa yeye pamoja na wanafunzi
wake walikuwa wakitokea upande wa mjini jambo lililopingwa vikali na
mashuhuda wa ajali hiyo kitendo kilichopelekea askari kuwatuliza
wananchi hao ambao walitaka kumpiga mwalimu huyo.
Akizungumza
na mwandishi wetu huku akiwa haoneshi ushirikiano wa kutosha mwalimu
aliyekuwa akiwasimamia wanafunzi hao wa VETA (hakutaja jina) alieleza
kuwa ndani ya haice kulikuwemo na wanafunzi ishirini akiwemo
aliyejeruhiwa(dereva).
Askari wa barabarani wakifanya vipimo katika ajali
“Huyu
mwalimu ndiyo mwenye makosa ,huwezi kumruhusu mwanafunzi aingize gari
barabarani katika hali kama ile” alieleza bwana Hamis Mbwana mmoja wa
mashuhuda wa ajali hiyo.
Wananchi waliokuwa wakishuhudia matukio yaliyojiri eneo la tukio
Hadi
mwandishi wetu anaondoka eneo la tukio gari maalum kwa ajili ya kuvuta
na kuondoa magari hayo lilifika ili kuruhusu shughuli nyingine za
matumizi ya barabara kuendelea.
Habari,Picha Na Dickson Mulashani
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269