Breaking News

Your Ad Spot

May 10, 2015

MZEE MANGULA, NAPE WAHANI MSIBA WA MTOTO WA MWALIMU NYERERE, KAPTENI JOHN NYERERE

Marehemu Kapteni John Nyerere (pichani), aliyefariki dunia jana katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es Salaam. alikokuwa akipatiwa matibabu. John alizaliwa mwaka 1957 jijini Dar es Salaam na enzi za uhai wake aliwahi kuwa mtumishi wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) akiwa rubani wa kurusha ndege za kivita.
  John alishiriki vita ya kumng'oa Nduli Idd Amini nchini Uganda.

   Kwa mujibu wa mmoja wa wanafamilia Kapteni John amefariki kutokana na  kusumbuliwa na maradhi ya mapafu na kisukari kwa muda mrefu.
 Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara) Philip Mangula akisaini kitabu cha rambi rambi nyumbani kwa Baba wa Taifa Msasani jijini Dar es Salaam ambapo alifika kumpa pole Mama Maria Nyerere na familia yake kufuatia msiba wa mtoto wa Baba wa Taifa John Nyerere.
 Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara) Philip Mangula akizungumza na Katibu wa Itikadi na Uenezi Nape Nnauye walipokutana nyumbani kwa Baba wa Taifa Msasani jijini Dar es Salaam kuhani msiba wa John Nyerere.

Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akisaini kitabu cha rambirambi ya msiba wa John Nyerere.
 Ndugu akitoa pole kwa Mama Maria Nyerere.
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akimpa mkono wa pole Mama Maria Nyerere kufuatia msiba wa mtoto wake John Nyerere kilichotokea jana jijini Dar es salaam.
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akizungumza na Mama Maria Nyerere alipofika nyumbani kwake kumpa pole kufuatia msiba wa mtoto wake John Nyerere, wengine pichani ni Makongoro Nyerere (kushoto), Mwenezi wa CCM mkoa wa Dar es salaam Juma Simba Gadafi, na Anna Nyerere.
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akizungumza na Makongoro Nyerere Msasani nyumbani kwa Baba wa Taifa wakati wa kuhani msiba wa John Nyerere.
(Picha zote na Adam Mzee)


No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages