Tume ya
taifa ya uchaguzi nchini NEC imetishia kusitisha zoezi la uandikishaji
wananchi katika daftari la kudumu la wapiga kura katika miji ya Arusha
na Kilimanjaro endapo viongozi wa kisiasa wataendelea kuingilia mchakato
huo na kuwa vyanzo vya vurugu katika vituo vya kuandikishia.
Ni
mwenyekiti wa tume ya taifa ya uchaguzi NEC Jaji Mstaafu Damiani Lubuva
akielezea masikitiko ya tume kufuatilia kile alichokiita ni kuingiliwa
kwa maafisa wa tume katika kazi zao za uandikishaji katika miji ya
Arusha na Kilimanjaro jambao lililopelekea kuzuka kwa vurugu katika
baadhi ya vituo ndani ya mikoa hiyo.
Jaji
Damian amesema katika mahojiano yake maalum na ITV jijini Dar es Salaam,
kuwa tangu kaunza kwa zoezi la uandikishaji kumekuwa na changamoto
kadha ambazo hata hivyo tume ilijitahidi kuzitatua lakini kwa hali ya
Arusha na Kilimanjaro huenda tume ikalazimika kufanya maamuzi magumu.
Amesisitiza
kuwa ni vema viongozi wa kisiasa wakahakikisha wanakuwa mstari wa mbele
katika kufanikisha zoezi hilo ambalo kwasasa limekwisha kukamilika kwa
zaidi ya asilimia 85, ambapo pia amesisitiza kuwa kwa hali ilivyo hivi
sasa uchaguzi utafanyika kama ulivyopangwa kwani kila kitu kiko katika
hali ya ukamilifu.
Katika
mahojaino hayo pia jaji Lubuva amezungumzia suala la uandikishwaji kwa
upande wa Zanzibar ambapo anasema zoezi hilo linatarajia kuanza muda
wowote akuanzia sasa huku akisisitiza utulivu wakati wa zoezi hilo.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269