Picha ya Pamoja ya DC Makonda, Viongozi wa BASATA, Viongozi wa NHIF na Wasanii
Baadhi ya Viongozi wa Vyama vya Wasanii waliokabidhiwa kadi za NHIF wakiwa na Mgeni rasmi DC Makonda
Baadhi ya wasanii wakifuatilia mada
Mkuu wa Wilaya ya Kindondoni akihutubia wasanii
……………………………………………………………………………
Awataka kutumia taaluma yao kuhamasisha wengine kujiunga:
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Paul
Makonda amesema wakati sasa umefika kwa wasanii kujiunga na Mfuko wa
Taifa wa Bima ya Afya, badala ya kuendelea kuchangishana fedha za
matibabu kila wanapougua.
Amesema kutokana na kupanda kwa
gharama za maisha hivi sasa zikiwemo za matibabu, wasaani wana kila
sababu ya kuona umuhimu wa kujiunga na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya
ili wanapougua watibiwe kwa kutumia kadi badala ya kuhangaika kutafuta
fedha taslimu.
Makonda alikuwa akizungumza
wakati wa ufunguzi wa semina kuhusu huduma za matibabu kupitia mpango
maalumu wa bima ya afya kwa wajasiliamali na vikundi vilivyosajiliwa
unaojulikana kama KIKOA.
Amesema hivi sasa wasanii wengi
wanahangaika kupata matibabu katika mazingira yasiyoridhisha kwa kuwa
hawana bima za afya hivyo ni muhimu kwao wachangamke fursa hiyo ambayo
itawawezesha kuchangia kabla ya kuugua na hivyo kuwa na uhakika wa
kutibiwa hata kama hawana fedha mfukoni.
Naye Mwakilishi wa Kaimu
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya, Eugen Mikongoti
amesema NHIF imeanzisha utaratibu huo wa kuchangia kwa kundi la
wajasiliamali ili kuwapa uhakika wa matibabu wakati wote wanapokua
katika shughuli zao za kuelimisha na kuhamasisha jamii katika masuala
mbalimbali ya kisiasa, kiuchumi na kijamii.
Amesema kwa kuchangia 76,800
mwanachama wa KIKOA atakuwa na uhakika wa kutibiwa mwaka mzima katika
vituo vya matibabu zaidi ya 6000 vilivyosajiliwa na Mfuko nchini nzima.
Mikongoti amesema NHIF itawatumia
wasanii hao katika kuelimisha umma ili kuhakikisha kuwa ujumbe wa
umuhimu wa wananchi kujiunga na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya unaenea
nchini nzima.
Katika semina hiyo iliyoandaliwa
kwa pamoja na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) na Baraza la Wasanii
Tanzania (BASATA), viongozi wanne wa Shirikisho la Wasanii
walikabidhiwa kadi zao za bima ya afya zinazowawezesha kupata matibabu
wakati wowote watakapougua.
Mpango wa bima ya afya kwa
wajasiliamali – KIKOA- unawalenga wajasiliamali walio katika vikundi
vilivyosajiliwa, ambapo hadi sasa zaidi ya vikundi mia moja vyenye
wanachama zaidi ya elfu ishirini vimejiunga na Bima ya Afya.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269