Mhandisi Happiness Mgalulla,
Naibu Katibu Mtendaji, Ofisi ya Rais Tume ya Mipango (aliyesimama)
akisoma hotuba wakati wa ufunguzi wa mkutano huo. Kushoto kwake ni Bw.
Maduka Kessy, Naibu Katibu Mtendaji, Ofisi ya Rais Tume ya Mipango.
Wengine ni Bibi Florence Mwanri, Naibu Katibu Mtendaji, Ofisi ya Rais
Tume ya Mipango (wa kwanza kulia), Bw. Paul Sangawe, Naibu Katibu
Mtendaji, Ofisi ya Rais Tume ya Mipango (wa tatu kulia).
Na: Thomas Nyindo
Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango
Ujumbe kutoka Serikali ya Tanzania wakifuatilia hotuba ya ufunguzi kutoka kwa kiongozi wa ujumbe huo MhandisiHappiness Mgalulla, Naibu Katibu Mtendaji, Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango.
Ujumbe kutoka Serikali ya Japan
ambao unajumuisha Ubalozi wa Japan nchini Tanzania, JICA – Tanzania,
Makao Makuu ya JICA- Japan na Wizara ya Mambo ya Nje ya Japan
wakifuatilia mjadala kwa makini.
Wajumbe wakifuatilia majadiliano hayo kwa umakini yatari kwa kutoa michango yao juu ya mada iliyoko mezani.
Bw. Masaharu Yoshinda, Balozi
wa Japan nchini Tanzania (wa pili kushoto) akisistiza jambo wakati wa
mkutano huo. Wengine pamoja nae ni wajumbe kutoka Serikali ya Japan.
………………………………………………………………….
Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango,
pamoja na majukumu mengine, inajukumu pia la kuratibu miradi ya
maendeleo kwa ajili ya ufadhili wa serikali ya Japan kila mwaka.
Maandalizi ya mwaka huu yameshakamilika na mkutano wa majadiliano kati
ya Serikali ya Jamhuri ya Muuungano ya Tanzania na Serikali ya Japan
ulifanyika mwishoni mwa wiki iliyopita katika Hotel ya Hyatt Regeny, The
Kilimanjaro, Dar es Salaam. Majadiliano hayo kwa upande wa Serikali ya
Japan yaliongozwa na Bw. Masaharu Yoshinda, Balozi wa Japan nchini
Tanzania, kwa upande wa Tanzania yaliongozwa na Mhandisi Happiness
Mgalulla, Naibu Katibu Mtendaji, Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango.
Malengo ya mkutano huo ni kujua
hatua iliyofikiwa katika maombi ya ufadhili wa miradi ya maendeleo
kutoka Serikali ya Japan kwa mwaka 2014/15, kuwasilisha miradi ya
maendeleo kwa ajili ya ufadhili kwa mwaka 2015/16, kujadiliana
changamoto zinazojitokeza katika utekelezaji wa miradi na kupendekeza
hatua za kuchukuliwa ili kuboresha ushirikiano baina ya Serikali hizi
mbili. Pia Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, iliwasilisha mawazo ya awali
ya Mpango wa Pili wa Maendeleo wa Miaka Mitano (FYDP II).
Wizara zilizoshiriki katika
Mkutano huo ni pamoja na Ofisi Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma,
Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Wizara ya
Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, na Wizara ya Fedha.
Wizara zingine ni pamoja na
Wizara ya Nishati na Madini, Wizara ya Ujenzi, Wizara ya Uchukuzi,
Wizara ya Kilimo, Wizara ya Chakula na Ushirika, Wizara ya Mifugo na
Mendeleo ya Uvuvi, Wizara ya Viwanda na Biashara, Wizara ya Maji na
Umwagiliaji, na Tume ya Mipango – Zanzibar.
Kwa upande wa Serikali ya Japani
taasisi zilizohudhuria ni pamoja na Ubalozi wa Japan nchini Tanzania,
JICA – Tanzania, Makao Makuu ya JICA- Japan na Wizara ya Mambo ya Nje ya
Japan.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269