Miss Kenya, Idah Nguma.
Redds Miss Tanzania 2015, Lilian Kamazima.
Redds Miss Tanzania 2015, Lilian Kamazima (kushoto), akiwa na Miss Kenya, Idah Nguma baada ya kuwatembea wagonjwa katika hospitali hiyo.
Mmoja
wa Maofisa kutoka Taasisi ya Smile Train inayofanya kazi na Miss Kenya,
Idah Nguma, Jane Ngige akizungumza na wanahabari (hawapo pichani).
Redds
Miss Tanzania 2015, Lilian Kamazima (kulia) na Miss Kenya, Idah Nguma
(kushoto), wakiwa na mmoja wa wadau wa Hospitali ya CCBR iliyopo
Msasani, baada ya kufanya ziara ya siku moja katika hospitali hiyo ya
kuwajulia hali wagonjwa pamoja na kuona huduma mbalimbali zinazotolewa
hospitali hapo Dar es Salaam leo asubuhi. Miss Kenya, Idah Nguma yupo
katika mfululizo wa ziara ya kutembelea hospitali zinazotoa matibabu ya
mdomo wazi na vistula.
Na Dotto Mwaibale
MISS
Kenya Idah Nguma ametembelea nchini Tanzania kwa ajili ya kutembelea
Hospitali ya CCBRT kuwafariji wagonjwa pamoja na kuona huduma
mbalimbali zinazotolewa hospitalini hapo.
Katika
ziara ya kutembelea hospitali hiyo Nguma aliongoza na mwenyeji wake
Redds Miss Tanzania 2015, Lilian Kamazima na mmoja wa maofisa wa kamati
ya kuratibu Miss Tanzania.
Akizungumza
wakati wa ziara hiyo Dar es Salaam leo asubuhi ,Nguma alisema
amefurahi kuja nchini hapa kwa mara ya kwanza huku lengo lake likiwa ni
kuangalia mradi wa Smile Train ambao upo swizland.
Nguma alisema mradi huo ni wakusaidia wanawake wenye festula pamoja na watu wenye matatizo ya mdomo wazi.
"Mimi
ni Balozi katika shirika hilo na nimekuja kuangalia huduma kwa
wagonjwa wa Fistula na Midomo wazi (sungura)" alisema Nguma.
Nguma
alisema amefurahishwa na huduma inayotolewa na wahudumu waliopo
katika hospitali hiyo pia atakapofika katika ziara yake ya kwa nchi ya
Uganda atawaelimisha jamii na wananchi wa Uganda kwa huduma bora
wanyopata watu wenye matatizo hayo.
Pia
hata Miss wa Tanzania Lilian Kamazima amesema kuwa wamemkaribisha kwa
furaha Miss wa Kenya hiyo yote ni kudumisha amani na upendo katika nchi
hizi mbili.
Alisema
ziara yake ya kuwaona wagonjwa ni moja ya kuonyesha kuwajali wagonjwa
na kudumisha upendo na kuwapatia faraja na kuowaongezea matumaini ya
kuona kuwa na wao ni miongoni mwa watu katika jamii.
"Nimefurahishwa na huduma inayotolewa katika hospitali hiyo hasa baada ya kuona wagonjwa wanaendelewa vizuri""alisema.
(Imeandaliwa na mtandao wa www. habari za jamii.com-simu namba 0712-727062)
(Imeandaliwa na mtandao wa www. habari za jamii.com-simu namba 0712-727062)
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269