Wanahabari
kutoka vyombo mbalimbali wakiwasili Kambi ya Jeshi la Kujenga Taifa
Kikosi namba 832 Ruvu JKT mkoani Pwani jana kwa ajili ya kujionea
shughuli mbalimbali za uzalishaji mali. Kikosi hicho kilichaguliwa
kuiwakilisha Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), kuonyesha
mafanikio ya majeshi nchini katika shughuli mbalimbali zikiwemo za
uzalishaji mali ili kuinua uchumi wa taifa.
Mkuu
wa Utawala na Mafunzo wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Brigedia
Jenelari, Jacob Gedion Kingu, alikuwa mgeni rasmi katika ziara hiyo ya
siku moja ya waandishi wa habari kutembelea kikosi hicho. Kingu
alimwakilisha Mkuu wa JKT nchini.
Mkuu wa
Utawala na Mafunzo wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Brigedia Jenelari,
Jacob Gedion Kingu (kulia), akizungumza na wanahabari kabla ya
kutembelea miradi mbalimbali inayofanywa na kikosi hicho.
Mkuu wa Kikosi 832 Ruvu JKT, Luteni Kanali Charles Mbuge, akizungumza na waandishi wa habari wakati akimkaribisha Mkuu
wa Utawala na Mafunzo wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Brigedia
Jenelari, Jacob Gedion Kingu kuzungumza na wanahabari katika ziara hiyo.
Mkuu
wa Kikosi 832 Ruvu JKT, Luteni Kanali Charles Mbuge (kushoto),
akiwaelekeza wanahabari wakati walipofika uwanja wa gwaride kuona vijana
wa kidato cha sita wanaopitia JKT kwa mujibu wa sheria wanavyofanya
mazoezi ya gwaride la kuhitimu mafunzo yao ya miezi sita mapema mwezi
ujao.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269