Mkurugenzi
Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Dk. Tausi
Kida (katikati) akimlaki Mgeni rasmi Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri
Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mh. Hawa Ghasia
(kushoto) mara baada ya kuwasili katika hoteli ya Ngurdoto jijini Arusha
kufungua warsha ya uwasilishwaji wa ripoti ya Maendeleo ya Binadamu
Tanzania ya Mwaka 2014 iliyoandaliwa na Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi
na Kijamii (ESRF) chini ya ufadhili wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa
Mataifa (UNDP). Kulia
ni Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa
Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez. (Picha zote na
Zainul Mzige wa Modewjiblog)
Mgeni rasmi Waziri wa Nchi,
Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI),
Mh. Hawa Ghasia (kushoto) akiwa ameongozana na Mkurugenzi Mtendaji wa
Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF) Dk. Tausi Kida
(katikati) pamoja Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na
Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez
kuelekea sehemu maalum ya mapumziko kabla ya kuingia katika ukumbi wa
mikutano.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Dk. Tausi
Kida akifafanua jambo kuhusu warsha ya uwasilishwaji wa ripoti ya
Maendeleo ya Binadamu Tanzania ya Mwaka 2014 iliyoandaliwa na ESRF kwa
mgeni rasmi (aliyeipa mgongo kamera) na meza kuu kabla ya kuingia kwenye
ukumbi wa mikutano.
Mgeni
rasmi Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali
za Mitaa, Mh. Hawa Ghasia akitoa hotuba ya ufunguzi wa warsha ya
uwasilishaji wa Ripoti ya Maendeleo ya Binadamu Tanzania ya Mwaka 2014
kwa Viongozi wa Mikoa na Wilaya iliyofanyika jijini Arusha katika hoteli
ya Ngurdoto.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF) Dk. Tausi
Kida (katikati) pamoja Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na
Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez
wakifuatilia kwa ukaribu hotuba ya mgeni rasmi (hayupo pichani).
Mkurugenzi
Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Dk. Tausi
Kida akitoa neno la ukaribisho kwa washiriki wa warsha ya
uwasilishwaji wa ripoti ya Maendeleo ya Binadamu Tanzania ya Mwaka 2014
iliyoandaliwa na Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF) chini
ya ufadhili wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP).
Mratibu
Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la
Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez akizungumza katika warsha
ya uwasilishwaji wa ripoti ya Maendeleo ya Binadamu Tanzania ya Mwaka
2014 na Wakuu wa mikoa, wilaya pamoja na Makatibu Tawala wa mikoa
iliyofanyika katika hoteli ya Ngurdoto jijini Arusha.
Naibu
Mkurugenzi Mkazi, Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP)
nchini, Amon Manyama akiwasilisha mada ya Mageuzi ya kiuchumi
yanayoendelea: kuangalia zaidi ukaji wa uchumi wakati wa warsha ya
uwasilishwaji wa ripoti ya Maendeleo ya Binadamu Tanzania ya Mwaka 2014
iliyoandaliwa kwa Wakuu wa mikoa, wilaya pamoja na Makatibu Tawala wa
mikoa katika hoteli ya Ngurdoto jijini Arusha.
Mkuu
wa mkoa wa Singida, Dkt. Parseko Kone (kushoto) wakifuatilia kwa
umakini na viongozi wenzake wakati mada mbalimbali zizokuwa
zikiwasilishwa kwenye warsha ya uwasilishwaji wa ripoti ya Maendeleo ya
Binadamu Tanzania ya Mwaka 2014 iliyoandaliwa na Taasisi ya Utafiti wa
Kiuchumi na Kijamii (ESRF) chini ya ufadhili wa Shirika la Maendeleo la
Umoja wa Mataifa (UNDP) kwa Wakuu wa Mikoa, Wilaya pamoja na Makatibu
Tawala wa Mikoa jijini Arusha.
Pichani
juu na chini ni Wakuu wa Mikoa, Wilaya pamoja na Makatibu Tawala wa
Mikoa waliohudhuria warsha ya uwasilishwaji wa ripoti ya Maendeleo ya
Binadamu Tanzania ya Mwaka 2014 iliyoandaliwa na Taasisi ya Utafiti wa
Kiuchumi na Kijamii (ESRF) chini ya ufadhili wa Shirika la Maendeleo la
Umoja wa Mataifa (UNDP).
Mkurugenzi
Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Dk. Tausi
Kida (kushoto) katika picha ukumbusho na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Chiku
Galawa (katikati) na Mkuu wa wilaya ya Urambo mkoani Tabora, Queen Mlozi
(kulia).
Mkuu
wa wilaya ya Mvomero, Betty Mkwasa (kushoto) katika picha ya ukumbusho
na Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Sophia Mjema nje ya ukumbi wa mikutano
Ngurdoto Mountain Lodge.
Pichani juu na chini Mgeni rasmi Waziri wa Nchi,
Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI),
Mh. Hawa Ghasia na meza kuu katika picha ya pamoja na Wakuu wa Mikoa na
Wilaya pamoja na Makatibu Tawala wa Mikoa waliodhuria warsha ya
uwasilishwaji wa ripoti ya Maendeleo ya Binadamu Tanzania ya Mwaka 2014
iliyoandaliwa na Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF) chini
ya ufadhili wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP).
Mgeni rasmi na meza kuu katika picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF).
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Dk. Tausi Kida akiteta jambo na mgeni rasmi Waziri wa Nchi,
Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI),
Mh. Hawa Ghasia mara baada ya zoezi la picha ya pamoja.
Na Mwandishi wetu, Arusha
SERIKALI
imesema itazingatia ushauri uliotolewa katika Ripoti ya Maendeleo ya
Binadamu ya Tanzania ya Mwaka 2014 iliyowasilishwa kwa Viongozi wa Mikoa
na Wilaya katika warsha yao iliyofanyika Ngurdoto, Arusha.
Kauli
hiyo imetolewa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa
na Serikali za Mitaa, Mh. Hawa Ghasia wakati akifungua warsha yenye
lengo la kujadili na kuielewa.
Ripoti
hiyo ambayo imejadiliwa kama “Mageuzi ya Kiuchumi kwa Maendeleo ya
Binadamu” ilizinduliwa rasmi mwezi machi mwaka huu wa 2015 inawasilishwa
kutokana na haja ya viongozi hao kutambua yaliyomo na namna ya kusonga
mbele katika mipango ya baadae.
Ripoti
hiyo ambayo ni matokeo ya utafiti wa Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na
Kijamii (ESRF) imelenga kusaidia kufahamu yaliyomo katika ripoti hiyo
ili kuwawezesha viongozi hao kupata uelewa mpana juu ya dhana hii ya
masuala ya Maendeleo ya Binadamu.
Warsha hiyo imewezesha na Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP).
Ghasia
alisema utafiti huo umelenga kuzijengea uwezo mamlaka za mikoa na
serikali za mitaa ili kuziwezesha kutoa huduma bora kwa wananchi.
Ripoti
hiyo ambayo imezungumzia masuala ya mageuzi ya kiuchumi kwa Maendeleo
ya Binadamu imetafakari kwa undani namna ya kufanya mageuzi ya kiuchumi
katika taifa ili kuleta maendeleo ya Binadamu.
Akizungumzia
maendeleo alisema mwanzoni mwa karne ya 21, mataifa mengi ya kiafrika
yalitengeneza Dira za Maendeleo kuwa mwongozo wa ujenzi wa uchumi na
maendeleo.
“Kwa
upande wa taifa letu, Dira ya Maendeleo ya mwaka 2025 inalenga katika
kulifanya taifa letu kuwa nchi ya uchumi wa kati wenye kutegemea zaidi
sekta ya viwanda na huduma.
“
Kwa maneno mengine, Dira ya Maendeleo ya Taifa 2025 inalenga siyo tu
katika ukuzaji wa uchumi bali kubadilisha muundo wa uchumi; kwa miaka
mingi uchumi wa Taifa letu umekuwa unategemea zaidi kilimo ambacho kina
tija ndogo.” alisema Ghasia.
Alisema kwamba Sera za Maendeleo ya taifa letu tangu uhuru zimekuwa zikiweka kipaumbele katika dhana ya Maendeleo ya Binadamu.
“Kwa
mfano, Azimio la Arusha la mwaka 1967, ambalo liliamua taifa lifuate
mfumo wa ujamaa na kujitegemea lilielekeza kwamba sera, mipango na
mikakati yote lazima zizingatie uboreshwaji wa maisha ya watu kwani
lengo la maendeleo ni watu.” Alisema.
Naye
Mkurugenzi Mtendaji wa ESRF, Dkt. Tausi Kida akizungumzia warsha hiyo
alisema kwamba utafiti huyo uliofanywa na taasisi yake uliwezekana kwa
kushirikiana na Wizara ya Fedha, Shirika la Maendeleo la Umoja wa
Mataifa (UNDP), Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (Idara ya uchumi), Ofisi ya
Taifa ya Takwimu (NBS) na ofisi ya Mtakwimu Mkuu wa serikali ya
Zanzibar.
Alisema Toleo hilo la Ripoti ya Maendeleo ya Binadamu ya Tanzania ya 2014 ni toleo la kwanza nchini.
Naye
Mratibu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa yaliyopo hapa nchini na
Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez,
alizungumzia umuhimu wa mabadiliko ya kiuchumi ili taifa liwe la kipato
cha kati.
Alisema
ipo haja kwa taifa hili kuhakikisha kwamba linatumia vyanzo vyake vya
kifedha kubadilika kutokana na hali halisi ilivyo kwa sasa.
Aidha
alisema ipo haja ya kuzingatia mipango madhubuti ya kuondoa umaskini
na kulinda mazingira, mambo ambayo yapo katika mpango mkakati wa Umoja
wa Mataifa wa UNDAP wa maendeleo kuanzia mwaka kesho hadi 2021.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269