Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) inayodhaminiwa na bia ya Kilimanjaro sasa itaondoka nchini siku ya jumapili usiku kuelekea Istambul nchini Uturuki kwa kambi ya siku nane kujiandaa na mchezo dhidi ya Nigeria Septemba 05, 2015.
Awali Taifa Stars ilikua ipitie Muscat nchini Oman kucheza mchezo wa kirafiki na timu ya taifa ya nchi hiyo, lakini kutokana na shirkikisho la Soka la Oman kushindwa kukidhi mahitaji ya Kanuni za FIFA za uuandaaji wa mechi ya kimataifa ya kirafiki sasa mchezo huo hautakuwepo tena.
Stars inatarajiwa kuondoka jumapili usiku na shirika la ndege la Uturuki (Turkish Airlines) na kuwasili Istambul (Ataturk Airport) siku ya jumatatu majira ya saa 5 kamili asubuhi, kisha kuelekea Kocael katika hoteli ya Green Park Kartepe ambapo ndio itakua kambi yake ya wiki moja.(P.T)
UCHAGUZI WA TEFA WAAHIRISHWA
Shirikisho
la Mpira wa Miguu nchini (TFF) kupitia kwa Mwenyekiti wa Kamati ya
Uchaguzi Aloyce Komba imeitisha majalada ya kamati ya uchaguzi ya TEFA
na kamati ya uchaguzi ya DRFA baada ya kupokea malalamiko na rufaa
kutoka kwa wagombea.
Kamati ya
Uchaguz ya TFF imeyaomba majalada hayo ili ijiridhishe na kuona haki
inatendeka kwa wagombea wote na baadae tarehe mpya ya uchaguzi
itatolewa.
SAANYA KUCHEZESHA AZAM NA YANGA
Shirikisho
la Mpira wa Miguu nchini (TFF) limemteua mwamuzi wa kati Martin Saanya
kuchezesha mchezo wa Ngao ya Jamii jumamosi, badala ya mwamuzi Israle
Nkongo aliyekua amepangwa awali.
Mwamuzi
Israel Nkongo anasumbuliwa na matatizo ya misuli ya paja, ambayo
itampelekea kukaa nje ya uwanja kwa takribani siku kumi, hali
iliyopeleka TFF kumbadilisha mwamuzi huyo kuelekea kwenye mchezo huo wa
jumamosi.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269