Mratibu
Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la
Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez akizungumza wakati akizindua Malengo Endelevu 17 ya Maendeleo nchini
(SDG’s) Tanzania katika shule ya Uhuru mchanganyiko, katika hafla
ambayo pia benki ya Standard Chartered Tanzania ilishiriki na kugawa
vitu mbalimbali kwa ajili ya wanafunzi wa shule hiyo. (Picha na Zainul
Mzige wa Modewjiblog)
Na Mwandishi wetu
Mratibu
Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la
Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez, amesema uondoaji umaskini
nchini unawezekana kwa ushirikiano kati ya wadau mbalimbali wa
maendeleo.
Kauli hiyo ameitoa mwishoni mwa wiki wakati akizindua Malengo Endelevu 17 ya Maendeleo nchini
(SDG’s) Tanzania katika shule ya Uhuru mchanganyiko, katika hafla
ambayo pia benki ya Standard Chartered ilishiriki na kugawa vitu
mbalimbali kwa ajili ya wanafunzi wa shule hiyo.
Katika
hafla hiyo ambayo ilitengenezwa mahususi kuanzisha utekelezaji wa
Malengo Endelevu (SDG’s) yakiwemo ya elimu, afya na mazingira Standard
walipeleka miti 150 ya kupanda, kompyuta na pia kutumia muda kuangalia
afya za wanafunzi.
Alisema
katika kukabiliana na umaskini kwa kuangalia Maendeleo Endelevu hakuna
kitu kigumu ukilinganisha na ugumu wa mwanafunzi asiyeona kujifunza kwa
kupitia vitabu vya nukta nundu na asiyesikia kuwasiliana na mtu mwingine
lakini pamoja na ugumu huo watoto hao wanaweza.
Alisema
kwa ushirikiano wa wadau kama walivyofanya wao na benki ya Standard
Chartered Tanzania anaamini kwamba maendeleo yatafikiwa na Tanzania
itafanikiwa kuzika umaskini ifikapo mwaka 2030.
Alisema
kutiwa saini kwa Malengo Endelevu na viongozi wa nchi 190 kumeonesha
wazi nia ya seriakli mbalimbali duniani kushughulikia umaskini na
kuuzika kwa kutekeleza malengo hayo endelevu.
Mwakilishi
wa Mkurugenzi wa Benki ya Standard Chartered Tanzania, Charles
Katongole akitoa salamu za Mkurugenzi wake ambapo benki hiyo imeahidi
kushiriki kikamilifu katika kuhakikisha utekelezaji wa malengo mapya ya
Maendeleo Endelevu (SDG's) yanafanikiwa nchini Tanzania. Kushoto ni
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika
la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez, Mtaalam wa Mahusiano na
Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa (UN) Tanzania Hoyce Temu (kulia) pamoja
na Mkuu wa Mahusiano wa benki ya Standard Chartered Tanzania, Juanita
Mramba (wa pili kulia).
Naye
Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Benki ya Standard Chartered Tanzania,
Charles Katongole, alisema kwamba ni lengo la benki hiyo ni kurejesha
faida kwa jamii kupitia miradi yake mbalimbali na kwamba kusaidia shule
hiyo ya Uhuru mchanganyiko iliyoanzishwa 01-01-1921 awali ikiitwa
Government African secondary school kabla ya kuhamishiwa Mzumbe Morogoro
01-01-1953 na kubadilishwa jina kuwa Kichwele African boys middle
school ikiwa na madarasa ya V-VII, ni sehemu ya kurejesha faida kwa
jamii.
Alisema
ni lengo la benki hiyo kwa mwaka huu kuwezesha kupatikana kwa dola za
Marekani milioni 5 kusaidia mambo mbalimbali ya watoto kwa mwaka huu kwa
nchi za Afrika mashariki huku Tanzania pekee watoto milioni 10
wakifikiwa.
Benki
hiyo yenye matawi Dar es salaam, Mwanza na Arusha katika miradi yake ya
afya, vijana na elimu wamekusudia kushirikiana na Umoja wa Mataifa
kutekeleza malengo mbalimbali endelevu ikiamini kwamba jamii ikiboreshwa
itakuwa katika mfumo mzuri wa maendeleo na kupiga vita umaskini.
Malengo ya SDG’s yamepangwa kutekelezwa katika kipindi cha miaka 15.
Mwalimu
Mkuu wa Shule ya msingi Uhuru mchangayiko, Anna Mshana akitoa risala
fupi ya shule yake sambamba na changamoto zinazoikabili shule yake kwa
ugeni huo kutoka Umoja wa Mataifa na Benki ya Standard Chartered
Tanzania.
Mwalimu
Mkuu wa shule hiyo Anna Mshana alisema shule hiyo ambayo ilianzisha
kitengo cha wanafunzi wasioona 1962 na kubadilishwa kuwa Shule ya msingi
Uhuru mchanganyiko mwaka 1964, inakabiliwa na changamoto mbalimbali.
Miongoni
mwa matatizo ni miundombinu ya shule hiyo isiyokidhi mahitaji halisi,
ukosefu wa ukuta, mashine za kufundishia watoto wasioona, upungufu wa
mabweni, magodoro, vitanda na gari la kuwakimbiza hospitalini inapotokea
dharura.
Alisema
ingawa kuna taasisi hutoa msaada wa gari na matibabu kwa watoto mchana,
lakini nyakati za usiku kukitokea dhararu inabidi shule igharamie
ingawaje wakati mwingine hatuna fedha inakuwa ni changamoto kwetu.
Alisema
Shule ya msingi Uhuru mchanganyiko yenye kutoa elimu jumuishi ina
vitengo vya ufundi seremala (1975) wanafunzi wenye mahitaji maalumu
ulemavu wa akili (1984) na viziwi na wasioona (Deafblidn)
kilichoanzishwa mwaka 1994.
Wanafunzi ambao ni viziwi nao walipata fursa ya kuja kila kinachoendelea kutoka kwa mkalimani wao.
Mkuu
wa Mahusiano wa benki ya Standard Chartered Tanzania, Juanita Mramba
akitangaza wanafunzi 17 ambao walishiriki shindano la kuhifadhi malengo
mapya ya Maendeleo Endelevu (SDG's) wakati wa kukabidhi zawadi kwa
wanafunzi hao wa shule ya Uhuru mchanganyiko.
Mratibu
Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la
Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez akikabidhi zawadi zilizotolewa
na Benki ya Standard Chartered Tanzania kwa wanafunzi hao, sambamba na
Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Benki ya Standard Chartered Tanzania,
Charles Katongole.
Mwakilishi
wa Mkurugenzi wa Benki ya Standard Chartered Tanzania, Charles
Katongole akimkabidhi Mwalimu Mkuu wa Shule ya msingi Uhuru
Mchanganyiko, Anna Mshana (wa pili kushoto) moja kati ya kompyuta tano
zilizolotolewa na Benki hiyo ikiwa ni kama ishara ya utekelezaji wa
lengo namba nne “Quality Education” wakati wa uzinduzi wa Malengo mapya
ya Maendeleo Endelevu (SDG’s) uliofanywa na Benki ya Standard Chartered
Tanzania kwa kushirikiana na Umoja wa Mataifa katika shule ya msingi
Uhuru mchanganyiko jijini Dar mwishoni mwa wiki. Kulia ni Mratibu Mkazi
wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo
(UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez na kushoto ni Mjumbe wa Bodi ya Shule ya
msingi Uhuru Mchanganyiko, Bw. Abubakar Mwambungu wakishuhudia tukio
hilo.
Kompyuta tano zilizotolewa na Benki ya Standard Chartered Tanzania kwa shule ya Uhuru mchanganyiko.
Mwakilishi
wa Mkurugenzi wa Benki ya Standard Chartered Tanzania, Charles
Katongole (wa tatu kushoto), Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa
Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro
Rodriguez (katikati), Mwalimu Mkuu wa Shule ya msingi Uhuru Mchangayiko,
Anna Mshana (wa pili kushoto), Mjumbe wa bodi ya kamati ya Shule ya
msingi Uhuru Mchanganyiko, Abubakari Mwambungu (kushoto) pamoja na
baadhi ya wafanyakazi wa Benki ya Standard Chartered Tanzania katika
picha ya pamoja huku wakiwa wameshikilia miche ya miti mbalimbali
ikiwemo ya matunda ambapo zaidi ya miche 150 ya miti ilipandwa kuzunguka
mazingira ya shule hiyo kulinda mazingira ikiwa ni ishara kwa vitendo
ya utekelezaji wa lengo namba 13 "Climate Action" kati ya Malengo 17
mapya ya Maendeleo Endelevu (SDG’s) nchini Tanzania.
Pichani juu na chini baadhi ya wanafunzi na walimu wa shule ya msingi Uhuru mchanganyiko waliohudhuria uzinduzi huo.
Mwakilishi
wa Mkurugenzi wa Benki ya Standard Chartered Tanzania, Charles
Katongole sambamba na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na
Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez
wakishiriki zoezi la upandaji miti kuzunguka maeneo ya shule ya Uhuru
mchanganyiko jijini Dar mwishoni mwa wiki.
Mratibu
Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la
Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez akishiriki zoezi la upandaji
miti sambamba na baadhi ya wanafunzi wa shule Uhuru mchanganyiko.
Mwalimu
Mkuu wa Shule ya Msingi Uhuru Mchangayiko, Anna Mshana akitoa maelezo
kwa Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa
Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez (aliyeinama) na
Mkuu wa Mahusiano wa benki ya Standard Chartered Tanzania, Juanita
Mramba (kulia) walipotembelea darasa la awali la watoto wenye ulemavu wa
macho (upofu) katika shule hiyo. Nyuma ya Mwalimu Mkuu ni Mjumbe wa
Kamati ya Shule ya Msingi Uhuru Mchangayiko, Abubakar Mwambungu.
Mratibu
Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la
Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez akicheza na mtoto Fatuma Haji
wa darasa la awali katika shule hiyo ambaye ni mlemavu wa macho
alipotembelea darasa hilo kabla ya kuzindua wa Malengo mapya ya
Maendeleo Endelevu (SDG’s) hafla iliyoandaliwa na Benki ya Standard
Chartered Tanzania kwa kushirikiana na Umoja wa Mataifa katika shule ya
msingi Uhuru Mchanganyiko jijini Dar mwishoni mwa wiki.
Mwakilishi
wa Mkurugenzi wa Benki ya Standard Chartered Tanzania, Charles
Katongole, Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi
wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez, Mkuu wa
Mahusiano wa benki ya Standard Chartered Tanzania, Juanita Mramba pamoja
na ujumbe wao katika nyuso za masikitiko walipotembelea darasa la
watoto wenye ulamavu wa macho (vipofu) na matatizo ya kutosikia
(viziwi) katika shule ya msingi Uhuru mchanganyiko.
Mwakilishi
wa Mkurugenzi wa Benki ya Standard Chartered Tanzania, Charles
Katongole, Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi
wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez, Mkuu wa
Mahusiano wa benki ya Standard Chartered Tanzania, Juanita Mramba na
ujumbe wao katika picha ya pamoja na wanafunzi ambao ni walemavu wa
macho ambao pia ni viziwi katika shule ya msingi Uhuru mchanganyiko.
Walimu wa darasa la watoto wenye ulemavu wa macho ambao ni viziwi wakicheza ngoma na wanafunzi wao.
Maana ya ulemavu wa macho na kuwa kiziwi.
Mkutubi
wa maktaba ya shule ya Uhuru mchanganyiko, Masanja akitoa maelezo ya
namna mashine za kukuzia maandishi kwa wale wanafunzi wenye uono hafifu
katika shule hiyo kwa Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Benki ya Standard
Chartered Tanzania, Charles Katongole (kushoto) na Mratibu Mkazi wa
Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo
(UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez walipotembelea maktaba hiyo.
Mratibu
Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la
Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez akipitia Katiba maalum kwa
watu wenye ulemavu wa macho iliyopo kwenye maktaba ya shule hiyo.
Kushoto kwake ni Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Benki ya Standard Chartered
Tanzania, Charles Katongole.
Mratibu
Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la
Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez na Ujumbe wa Benki ya Standard
Chartered Tanzania ulioongozwa na Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Benki ya
Standard Chartered Tanzania, Charles Katongole wakitembelea mambweni ya
wanafunzi katika shule ya msingi Uhuru Mchanganyiko.
Mwakilishi
wa Mkurugenzi wa Benki ya Standard Chartered Tanzania, Charles
Katongole, Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi
wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez pamoja na baadhi
ya wafanyakazi wa Benki ya Standard Chartered Tanzania katika picha ya
pamoja na baadhi ya wanafunzi wa shule ya Msingi Uhuru Mchanganyiko.
Mwakilishi
wa Mkurugenzi wa Benki ya Standard Chartered Tanzania, Charles
Katongole (kulia) na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na
Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez
katika picha ya pamoja na wanafunzi wa shule ya msingi Uhuru
mchanganyiko Issa Abasi Wenge w darasa la pili (wa pili kushoto) mlemavu
wa ngozi na Fatuma Haji (wa pili kulia) wa shule ya awali mwenye
ulemavu wa macho.
Mwakilishi
wa Mkurugenzi wa Benki ya Standard Chartered Tanzania, Charles
Katongole (kulia) na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na
Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez na
Mwanafunzi Mariana Alex (Mariana the voice of the SDGs in TZ) wa darasa
la tano katika shule ya msingi Uhuru mchanganyiko jijini Dar. #TELLEVERYONE about the #GlobalGoals
Mtaalam
wa Mahusiano na Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa (UN) Tanzania Hoyce
Temu akiserebuka na baadhi ya wanafunzi wa shule ya Uhuru mchangayiko.
Bango lililoorodhesha Malengo 17 mapya ya Maendeleo Endelevu (SDG’s).
Siku
ilimazika kwa mechi ya kirafiki baina ya Shule ya msingi Uhuru
mchanganyiko na wafanyakazi wa Benki ya Standard Chartered Tanzania
katika viwanja vya shule ya sekondari Benjamin Mkapa ambayo ilizinduliwa
na Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Benki ya Standard Chartered Tanzania,
Charles Katongole (kulia) na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa
Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro
Rodriguez.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269