Waziri wa
Katiba na Sheria, Dk Asha-Rose Migiro akihutubia mkutano wa uzinduzi
wa Kampeni za Mgombea Ubunge wa Jimbo la Monduli Mkoani Arusha kwa
tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Namelok Sokoine.
gombea
bunge wa Jimbo la Monduli kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) Namelok
Sokoine akihutubia wananchi katika mkutano huo wa hadhara wa uzinduzi wa
kampeni zake.
MGOMBEA
jimbo la Monduli kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Namelok Sokoine,
akihutubia mkutano wa hadhara wakati wa uzinduzi wa kampeni zake
zilizofanyika katika viwanja vya Nanja Mnadani Monduli mkoani Arusha
Septemba 28,2015 ambapo pamoja na mambo mengine ameahidi kuendeleza yote
aliyoasisi, kusimamia na kutekeleza aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo,
Edward Lowassa.
Namelok Moringe Sokoine akiwasili katika uwanja huo wa Nanja tayari kwa uzinduzi wa kampeni.
Wazee wa Kimila wa Jamii ya Kimaasai wa Monduli wakiongoza dua maalim ya kumuombea Binti yao Namelok.
Mwalimu Lorinyu Nkoosi, mmoja wa waliochuana na Namelok Sokoine katika mchakato wa uteuzi ndani ya CCM akiongea.
Wananchi wa Monduli wakiwa katika mkutano huo.
Wajane
wa Waziri Mkuu wa Zamani wa Tanzania, Edward Moringe Sokoine ambao ni
mama wa Namelok Sokoine wakitambulishwa mkutanoni hapo na Mwenyekiti wa
kamati ya kampeni za CCM jimbo la Monduli, Paul Kiteleki.
Waziri wa
Katiba na Sheria, Dk Asha-Rose Migiro (kulia) akimkabidhi ilani ya
Chama cha Mapinduzi Mgombea Ubunge wa Jimbo la Monduli Mkoani Arusha kwa
tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Namelok Sokoine wakati wa uzinduzi
wa jkampebni zake uliofanyika Monduli jana.
Dk Asha-Rose Migiro akisalimiana na wamama wa kimaasai alipowasili mkutanoni hapo.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269