Mgombea
Nafasi ya Ujumbe wa Baraza la Wawakilishi Jimbo la Mahonda kwa tiketi
ya CCM Balozi Seif Ali Iddi kwa niaba ya wagombea wenzake wa nafasi
mbali mbali akiwashukuru wanachama wa CCM wa Matawi yaliyomo ndani ya
Jimbo hilo katika Mikutano tofauti kwa kuwachaguwa katika kura za Maoni
zilizopita mwezi Agosti mwaka huu.
Wanachama
wa CCM wa Tawi la Kitope “B” wakiwa katika Mikutano ya kupongezwa baada
ya kuwachagua wagombea wao wa nafasi tofauti kwenye kura za Maoni.
Baadhi
ya wanachama wa Chama cha Mapinduzi wa Tawi la CCM Kazole wakiwa katika
Mikutano ya kupongezwa baada ya kuwachagua wagombea wao wa nafasi za
Uwakilishi, Ubunge na Udiwani ndani ya Jimbo la Mahonda.
Picha na –OPMR – ZNZ.
Usimamizi
na utatuzi wa changamoto zinazowakabili wananchi wa shehia na Wadi
zilizomo ndani ya Jimbo la Mahonda zitapatiwa suluhisho kwa kutumia
Ilani na CCM ya mwaka 2015 – 2020 endapo wananchi hao wataamua
kuwachagua Wagombea wa Nafasi zote za Uongozi ndani ya Jimbo hilo
kupitia CCM kwenye Uchaguzi Mkuu utakaofanyika mwishoni mwa mwezi huu.
Wagombea
hao walitoa kauli hiyo wakati wakizungumza na Wanachama wa CCM wa Matawi
yaliyomo ndani ya Jimbo la Mahonda katika mikutano tofauti ya
kuwashukuru baada ya uamuzi wao wa kuwateuwa kugombea nafasi hizo katika
kura za Maoni zilizopita mwezi Agosti mwaka huu.
Balozi
Seif Ali Iddi anayewania nafasi ya Uwakilishi alisema mambo watakayoyapa
kipaumbele endapo watachaguliwa kushika nyadhifa wazizoomba kwa kupitia
Ilani ya Uchaguzi ya CCM ni kuhakikisha wanasiamia upatikanaji wa
huduma za kijamii kama Maji, Umeme pamoja na Elimu katika Jimbo hilo.
Alisema
zipo baadhi ya shehia hasa zile zilizounganishwa katika Jimbo Jipya la
Mahonda ukiachilia mbali za Kitope hadi sasa bado zinakabiliwa na
ukosefu wa huduma hizo jambo ambalo ndani ya kipindi cha miaka mitano
zitapatiwa ufumbuzi unaofaa.
Balozi
Seif alisema huduma za kusambaza umeme ndani ya Jimbo zima zimeanza
rasmi katika vile vijiji ambavyo huduma hiyo haijafika zikianzia katika
Kijiji cha Matetema hadi Kichungwani.
Alifahamisha
kwamba huduma hizo zitakwenda sambamba na zile za Maji safi na salama
pamoja na uimarishaji wa Sekta ya Elimu kwa kuhakikisha kwamba wanafunzi
wa skuli zote zilizomo ndani ya Jimbo la Mahonda wanapata vikalio,
Maabara na Maktaba.
Akigusia
chuki zinazoendelea kuenezwa na baadhi ya wanasiasa kwa wapiga kura wa
Jimbo la Mahonda Balozi Seif alisema bila ya Chama cha Mapinduzi
kushinda kwenye Jimbo hilo wananchi wake wako hatarini na chuki za
upinzani.
Alisema
chuki hizo ziko wazi kutokana nabaadhi ya watu kuanza kupita maeneo
tofauti ya Jimbo hilo na kufanya zoezi la kuhakikishi pamoja na kupiga
picha mashamba yaliyomo ndani yake wakitaraji kurejeshewa.
Balozi
Seif alifahamisha kwamba upinzani umeahidi kwamba endapo utashika
madaraka ya Nchi jambo la kwanza ni kirejesha mashamba na Nyumba zote
zilizotaifishwa mara baada ya Mapinduzi ya Mwaka 1964.
Alitahadharisha
kwamba Wananchi wakifanya makosa ya kutoa kura kwa chama kisichokuwa
cha Mapinduzi waelewe kuwa wamejiangamiza wenyewe na wasije tafuta
mchawi.
Mh.
Bahati Ali Abeid Nassir anayewania nafasi ya Ubunge kupitia tiketi ya
Chama cha Mapinduzi alisema katika kukabiliana na changamoto ya ajira
hasa kwa Vijana ameahidi kushirikiana na Viongozi wenzake katika
kuwakusanya Vijana kuunda vikundi vya ujasiria amali kwa lengo la
kujiajiri wenyewe.
Mh.
Bahati alisema hakuna njia ya mkato katika kukabiliana na changamoto ya
ajira ambayo imekuwa ikiyakumba pia Mataifa mbali mbali Ulimwenguni
yakiwemo yale yaliyoendelea kiviwanda.
Alifahamisha
kwamba Vikundi hivyo vitapatiwa vifaa pamoja na zana zitakazowawezesha
kuendesha miradi yao ya kujitegemea kutegemea na maeneo wanayoishi kwa
vile Serikali kuu tayari imeshakusudia kuimarisha miundo mbinu mbali
mbali ya kiuchumi ikiwemi Utalii na Kilimo cha umwagiliaji.
Aliwatanabahisha
Wananchi hasa Vijana kuwa hadhari na ushawishi unaoendeleza kufanywa na
baadhi ya Watu hasa wanasiasa wa kuwarubuni vijana kwamba watawapatia
ajira endapo watawachagua katika kinyang’anyiro cha uchaguzi
kinachotarajiwa kufanyika Tarehe 25 Mwezi huu wa Oktoba.
Mh.
Bahati aliwakumbusha wazazi kwamba bado wana dhima ya kuwaelekeza watoto
wao juu ya Historia ya Taifa hili lililopatikana kwa njia ya Mapinduzi
kutoka mikononi mwa wakoloni waliokuwa wakiendeleza udhalimu dhidi ya
Wazawa wa Taifa hili.
Kwa
upande wake akitoa shukrani kwa wanachama hao wa CCM wa Matawi tofauti
ya Jimbo la Mahonda Bibi Hadia Juma Chum anayewania nafasi ya Udiwani
Wadi ya Fujoni.
Akigusia
chaguzi za maoni zilizomaliza mchakato wake Mh. Bahati alisema si vizuri
kwa wana CCM kwenda kwenye uchaguzi Mkuu wakiwa na vidonda vya uchaguzi
wa kura za Maoni.
Alisema
wakati wa makundi umekwisha na kufutwa kabisa na liliopo mbele kwa wana
CCM hao ni kuhakikisha Chama cha Mapinduz kinashinda ili kiendelee
kuongoza Dola.
Mh.
Bahati alifahamisha kwamba Vijana wa Chama cha Mapinduzi kusema kwamba
mgombea wa chama hicho hawamtaki waelewe kuwa wao ndio wenye matatizo.
Nao Nd.
Haji Hadhil Mkadam Mgombea nafasi ya Udiwani Wadi ya Mahonda na Bibi
Hadia Juma Chum anayewania Udiwani wadi ya Fujoni aliwaasa Wananchi hasa
Vijana kuelewa kwamba amani ya Nchi ndio hazina kubwa inayoringia
Tanzania katika nyanja ya Kimataifa.
Walisema
kuchezewa kwa amani hiyo ni kuliangamiza Taifa na watakaoathirika na
kudhalilika zaidi ni kundi kubwa la akina mama na Watoto mambo ambayo
kila mwananchi anapaswa kusaidia kupambana nayo.
Wagombea
Udiwani hao wa Wadi za Mahonda na Fujoni Nd. Haji Fadhil Mkadam na Bibi
Hadia Juma Chum walifahamisha kwamba kazi kubwa iliyopo kwa wananchi wa
Mahonda ni kushirikiana na wenzao Nchini katika kuisimamia CCM iendlee
kuongoza Dola ya Tanzania kwa kuwachagua wagombea wake.
Walisema
Chama cha Mapinduzi kinachotokana na mifupa ya Vyama vya TANU na ASP
ndicho Chama chenye dhamira sahihi ya kuendelea kuyalinda Mapinduzi ya
Zanzibar ya Mwaka 1964 yaliyozaa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.
Wagombea
hao wa nafasi tofauti za Uongozi Jimbo la Mahonda kupitia Chama cha
Mapinduzi tayari wameshakamilisha ziara ya kushukuru kwa Matawi ya CCM
ya Kinduni, Kitope “B”, Kazole, Matetema pamoja na Mkadini.
Matawi
mengine yaliyobaki ya CCM ambayo pia wataendelea na ziara hiyo ya
kushukuru ni pamoja na Zingwezingwe, Mangapwani, Kiomba Mvua pamoja na
Wadi ya Upenja ambayo kwa sasa imo ndani ya Jimbo Jipya la Kiwengwa.
Othman Khamis Ame
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269