Mkurugenzi
wa Mifumo ya Malipo wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Bernard Dadi
(kulia), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam
leo mchana, kuhusu benki hiyo kuanza kutumia mfumo wa malipo baina ya
benki na benki kwa masaa 24 kwa siku saba za wiki kwa mwaka
utakajulikana kama TISS. Kushoto ni Mkurugenzi wa Huduma za Kibenki,
Marcian Kobello.
Mkurugenzi wa Huduma za Kibenki, Marcian Kobello (kushoto), akizungumza katika mkutano huo.
Waandishi wa habari wakichukua taarifa hiyo.
Mkutano
na waandishi wa habari ukiendelea. Walioipa kamera mgongo kutoka
kushoto ni Meneja Msaidizi wa Idara ya Uhusiano wa benki hiyo, Vicky
Msima na kulia ni Kaimu Meneja Huduma za Kibenki, John Kayombo.
Na Dotto Mwaibale
BENKI
Kuu ya Tanzania (BoT), imesema kuanzia mwakawa fedha ujao itaanza
kutumia mfumo wa malipo baina ya benki na benki kwa masaa 24 kwa siku
saba za wiki kwa mwaka ambapo utakuwa ukijulikana kama TISS.
Hayo
yamesemwa Dar es Salaam leo mchana na Mkurugenzi wa Mifumo ya Malipo
BoT, Bernard Dadi na kuongeza mfumo huo utaweza kufanya kazi kwa ufanisi
iwapo wafanyabiasha na wananchi kwa ujumla watauchangamkia kwani kwa
sasa inapatikana kuanzia saa tatu asubuhi hadi saa mbili usiku kwa benki
za kibiashara zilizojiunga.
"Kwa
sasa kuna mfumo huu wa TISS ambao umekuwa ukifanya kazi siku za kazi
hadi saa mbili usiku na siku za mapumziko na sikukuu unafanya kazi
kuanzia saa tatu hadi saa nane, ila tunatarajia mwaka wa fedha ujao
utakuwa unafanya kazi kwa masaa 24," alisema.
Alisema
kimsingi mfumo huo una lengo la kuondoa mfumo wa kutumia hundi ambao
unatumia muda mrefu na wakati mwingine kuna makosa ambayo yanatokea ya
mtu anavyoandaa hivyo kuchelewa.
Naye
Mkurugenzi wa Huduma za Kibenki wa BoT, Marcian Kobello alisema uhaba
wa sarafu ya shilingi 500 mitaani unachangiwa na wananchi wenyewe ambao
wakienda benki hawachukui fedha hizo hivyo kusababisha zibakie huko
kwenye mabenki.
Alisema
sarafu za shilingi 500 zipo zaidi ya milioni 100 BoT lakini hadi sasa
ni milioni 20 ndizo zipo katika mzunguko hali ambayo inachangia
kuadimika kwa fedha hizo.
Alitoa
mwito kwa wananchi na wafanyabiashara kuchukua sarafu hizo katika
mabenki ili ziweze kufika katika mizunguko na dhana kuwa sarafu hiyo ina
madini ya fedha ni uongo kwani asilimia 94 ni chuma na asilimia 6 ni
nikoni.
Aliwataka
Watanzania kujenga utamaduni wa kupeleka fedha ambazo zimechakaa katika
mabenki ili waweze kubadilishiwa kwani utaratibu wa kuuza fedha haupo
kisheria pamoja na ukweli kuwa hakuna sheria inayokataza.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269