Mkurugenzi
wa Takwimu za Uchumi wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), Morrice Oyuke
(kulia), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam
leo, wakati akitoa taarifa za pato la taifa robo ya pili ya mwaka
kuanzia mwezi Aprili hadi Juni 2015. Kushoto ni Meneja Takwimu za Pato
la Taifa, Daniel Masolwa.
Mkutano na waandishi wa habari ukiendelea.
Waandishi wa habari wakichukua taarifa hiyo.
Wapiga picha wakichukua picha katika mkutano huo.
Na Dotto Mwaibale
OFISI
ya Taifa ya Takwimu imesema pato la taifa limeongezeka kwa asilimia 7.9
huku sekta ya madini na uzalishaji umeme ikifanya kuongezeka kwa pato
katika kipindi cha robo mwaka 2015 ikilinganishwa na kipindi cha mwaka
2014.
Akizungumza Dar es Salaam leo asubuhi wakati wakati akitoa taarifa za pato la taifa robo ya pili ya mwaka kuanzia mwezi Aprili hadi Juni 2015, Mkerugenzi
wa Takwimu za Uchumi wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Morrice Oyuke
alisema ongezeko hilo la takwimu ni la miezi mitatu ya mwaka huu.
Oyuke
alisema ongezeko hilo la pato la taifa linaenda sanjari na matokeo ya
thamani ya pato la taifa kwa mwaka huu ambalo lilikuwa ni trilioni 89.0
ambapo katika robo ya mwaka ni trilioni 45.5 ikilinganishwa na trilioni
39.0 katika mwaka 2014.
Alisema
thamani ya pato la taifa ya robo mwaka ya trilioni 45.5 ni kubwa hivyo
kusababisha pato la taifa la mwaka mzima linaweza kukuwa kama uchumi
hautotetereka.
"Kama
uchumi hautaweza kuguswaguswa na matatizo mingene inaweza ikasababisha
pato la taifa la mwaka huu likaongezeka badala ya ile iliyotegemewa hapo
mwanzo,"alisema.
Alisema ongezeko hilo la pato la taifa limechangiwa na sekta mbalimbali kufanya vizuri katika kipindi cha robo mwaka.
Alisema
sekta ambazo zimeongoza katika kipindi cha robo mwaka ni sekta ya
madini,umeme,kilimo na mifugo,viwanda na ujenzi na huduma za kitaalamu.
Alisema
sekta ya uzalishaji umemere imekuwa kwa asilimia 18.5 huku bidhaa za
viwandani ni asilimia 6.9 madini mawe na kokoto zimeongezeka asimilia
8.3 limeongezeka kutokana na shghuli za kiuchumi.
"Kutokana
na taarifa hii ya pato la taifa kwa robo mwaka taarifa hizi zitumike
katika kupanga na kurekebisha sera mbalimbali za maendeleo ya nchi,"
alisema.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269