Katibu
Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue (kushoto), akihutubia wakati
akifungua mkutano wa wadau wa takwimu Dar es Salaam leo asubuhi. Kulia
ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Profesa Adolph Mkenda na Mkurugenzi
Mkuu Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), Dk.Albina Chuwa. Mkutano huo
uliandaliwa na NBS.
Mkurugenzi Mkuu Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), Dk.Albina Chuwa akihutubia kwenye mkutano huo.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Profesa Adolph Mkenda akizungumza katika mkutano huo.
Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Dk.Rogers Dhliwayo akizungumza kwenye mkutano huo.
Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia nchini, Bella Bird akizungumza kwenye mkutano huo.
Mtafiti
kutoka Taasisi ya Utafiti wa Masula ya Uchumi na Kijamii (ESRF), Oswald
Mashindano (Ph.D), akizungumza katika mkutano huo.
Muongozaji wa mkutano huo, Maria Sarungi akitoa maelekezo.
Wadau mbalimbali wa masula ya takwimu wakiwa katika mkutano huo.
Mkutano ukiendelea.
Viongozi wakiwa Meza kuu.
Washiriki kutoka mashirika ya maendeleo ya kimataifa wakiwa kwenye mkutano huo.
Na Dotto Mwaibale
KATIBU
Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue amewataka watendaji wa Serikali kutoa
takwimu mbalimbali za maendeleo na kuziweka katika mitandao ili
wananchi waweze kuziona na kuhoji mipango ya maendeleo iliyofanyika hama
kukwama.
Hayo
aliyabainisha wakati akifungua mkutano wa wadau wa takwimu ulioandaliwa
na Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Dar es Salaam leo asubuhi kwa ajili
ya kukubaliana jinsi ya kushirikiana katika kuhakikisha takwimu za
viashiria vya Mpango wa Maendeleo Endelevu zinapatikana kwa wakati.
Alisema
takwimu mbalimbali ni lazima zioneshe mipango ya maendeleo iliyofanyika
au kumalizika badala ya kuwa siri na kuwafanya wananchi kushindwa
kuhoji.
"Takwimu
mbalimbali za maendeleo zikiwa wazi itasaidia wananchi kufahamu miradi
ya maendeleo iliyopo na iliyokwama jambo ambalo litasaidia kusukuma
maendeleo ya nchi" alisema Sefue.
Alisema
lengo la lengo la kuelimishana juu ya kukamilika kwa utekelezaji wa
Malengo ya Milenia (MDGs) na kuanza kwa Malengo mapya ya Maendeleo
Endelevu - Sustainable Development Goals (SDGs).
Aliongeza
kuwa utekelezaji wa Malengo ya Maendeleo ya Milenia - MDGs ulikuwa ni
wa miaka 15 kuanzia mwaka 2000 hadi 2015. Mpango huu wa MDGs unakamilika
mwaka huu na kuanza kwa mpango mpya wa Malengo ya Maendeleo Endelevu
(SDGs) ambao pia ni miaka 15 ijayo.
Alisema
Tanzania ni nchi ya kwanza kuanza kufanya vikao vya kutekeleza mpango
huo wa maendeleo jambo ambalo linaonesha kuwa na kasi ya kuyafikia
maendeleo hayo ya dunia.
Mkutano
huo ulioandaliwa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) ulihudhuriwa na
wadau wa takwimu takribani 100 kutoka Wizara, Idara, Wakala na Taasisi
za Serikali, Wadau wa Maendeleo, Wadau wa Sekta Binafsi pamoja na Wadau
wa Taasisi za Elimu ya Juu.
Septemba
mwaka huu, viongozi wa nchi mbalimbali duniani akiwemo Rais Jakaya
Kikwete walikutana nchini Marekani kwa ajili ya kutathmini utekelezaji
wa Malengo ya Maendeleo ya Milenia – MDGs ambapo ilionekana kwamba kuna
baadhi ya malengo yalikuwa yamefanikiwa na mengine hayakufanikiwa.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269