Mgombea
Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli
akiwaambia wananchi wa Karatu katika mkutano wa kampeni uliofanyika
katika uwanja wa Bwawani,kuwa mmoja wa viongozi wa upinzani anayempenda
kwa dhati, ni aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chadema, Dkt Wilbrod Slaa,amesema
kuwa ni kiongozi imara asiyependa kuyumbishwa na kwamba ni kiongozi
mwenye msimamo thabiti na mapenzi makubwa na nchi yake Tanzania.PICHA NA
MICHUZI JR-KARATU
Umati
wa Washabiki na wafuasi wa CCM waliokusanyika katika uwanja wa Bwawani
jioni ya leo kwenye mkutano wa kampeni jioni ya leo mjini
Karatu,wakishangilia mara baada kumsikiliza sera zake wakati akijinadi
na kuomba ridhaa ya kuiongoza nchi katika kipindi cha awamu ya tano kwa
nafasi ya Urais.
Mgombea
Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha Mapinduzi CCM
Dkt John Pombe Magufuli akiwanadi wagombea Viti vya Udiwani mbele ya
umati wa wakazi wa mji wa Karatu jioni ya leo kwenye mkutano wa hadhara
wa kampeni uliofanyika katika uwanja wa Bwawani mjini humo mkoani
Arusha.
Wabunge
wa viti maalum wanaowakilisha wanawake watarajiwa kutoka CCM kutoka
mkoa wa Arusha, kushoto ni Catherine Magige na Violet Mfuko.
Mgombea
Uubunge jimbo la Karatu Dk.Wilbald Slaa Lorri akimuombea kura Mgombea
Urais wa CCM Dkt Magufuli pamoja na yeye mbele ya wakazi wa mji wa
Karatu jioni ya leo kwenye mkutano wa kampeni,kulia kwake ni Wabunge
watarajiwa viti maalum wanaowakilisha wanawake mkoa wa Arusha, kushoto
ni Catherine Magige na Violet Mfuko wakishangilia.
Mgombea
urais wa Tanzania kupitia CCM, Dk John Magufuli pichani kushoto
akiungana na wasanii Chege na Temba kucheza muziki wakati wa mkutano wa
kampeni mjini Karatu, mkoani Arusha.
Mgombea
urais wa Tganzania kupitia CCM, Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia
wananchi katika mkutano wa kampeni mjini Mbulu, mkoani Manyara jioni ya
leo
Dkt. Magufuli akisisitiza jambo mbele ya maelfu ya wananchi wa Mbulu jijini jioni ya leo kwenye mkutano wa kampeni.
Mgombea
Urais wa CCM Dkt Magufuli akiwanadi wagombea ubunge na madiwani mbele
ya wakazi wa mji wa Mbulu kwenye mkutano wa kampeni jioni ya leo.
Dk
Magufuli akijinadi kwa wananchi katika Mji wa Haydom, wilayani Mbulu,
Manyara ambapo aliwataka wananchi kutowachagua wagombea wanaotoa rushwa
kwani wakikubali wanaweza wakawauza wao na Tanzania kwa ujumla
Wananchi
wa mji wa Haydom wakimshangilia Mgombea Urais wa CCM Dkt Magufuli
alipokuwa akimwaga sera zake za kujinadi na kuwaomba kura za ndio ifika
Oktoba 25 kwenye uchaguzi utakaofanyika mwaka huu kupitia ngazi ya
Urais,Ubunge na Udiwani.
Wakazi
wa Haydom wakifuatila hotuba ya Dk Magufuli alipokuwa akiwahutubia
kwenye mkutano wa kampeni mapema leo mchana mjini humo.
Mgombea
Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt.John Pombe Magufuli
akimnadi mgombea ubunge Jimbo la Mbulu Vijijini, Fratei Masay mjini
Haydom leo.
Washabiki na wafuasi wa CCM wakiwa na bango lao la ujumbe maridhawa kabisa.
Washabiki na wafuasi wa CCM wakishangilia ujio wa Dkt Magufuli na
kuwahutubia kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika jioni ya leo kwenye
uwanja wa Bwawani mjini Karatu,mkoa wa Arusha.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269